Mkuu matatizo ya Mark Mwandosya na Mkoa wa Mbeya yalianza na Mtandao wa Kikwete.
Kosa ilikuwa kuwa wa tatu katika kinyang'nyiro cha urais mwaka 2005.
Jamaa alipgwa vita na Lowasa , alipigwa vita na Mkuu wa Mkoa Mwakipesile, alipigwa vita na hata CCM yenyewe mpaka ikawa mbaya.
Watu wa Mbeya nawafahamu, vijana kuingia kushabikia CHADEMA ilikuwa a direct reaction kwa nguli wao kupigwa vita vya wazi wazi.
Nakumbuka Waziri Mkuu Lowasa wakati huo alipotembelea Mbeya, Mwandosya aliimbiwa "Raisi...raisi....raisi..." na vijana wa Mbeya mjini.
Kitendo hicho kilimuudhi sana Lowasa, lakini hiyo ilielezea jinsi Mwandosya alivokubalika sana mkoani Mbeya, tena na makabila yote mkoani.
The powers that be wakati huo waliamua kumdhibiti Mwandosya kisiasa.
Kugombea NEC mwaka 2007 walimwekea kijana mdogo anaitwa Thomas Mwang'onda, mtoto wa kigogo wa sekta ya intellijensia, Abson Mwang'onda.
Fedha nyingi sana zilitumika kumnadi Thomas, kiasi kufikia bilioni moja.
Lakini kijana Thomas aliangukia pua!
Mwandosya aliwahi kulalamika katika kitabu kimoja jinsi alivyokuwa akipigwa rafu, na serikali yake, na chama chake CCM!
Hatuwezi kuunganisha , lakini mara Mwandosya aliyekuwa akionekana fit na anafanya mazoezi kila alipopata wasaa mitaani, akaanza kuugua.
Wengine wanadai aliwekewa sumu kama ile ya Dr Harrison Mwakyembe, lakini hilo halijathibitishwa.
Kugombe tena mwaka 2015 ilikuwa just going through the motions, Mwandosya alisha umizwa vibaya.
Mwishoni alipoishiwa nguvu masikini Mwandosya akaamua kurudi kupumzika kijijini kwake Lufilyo, Zaidi ya kilometa 100 toka hata mjini tukuyu.
Kwa maoni yangu serikali ya CCM ndiyo iliyo utoa mkoa wa Mbeya kwenda CHADEMA, kwa kumdhibiti kipenzi cha wana Mbeya, Prof Mark mwandosya.
Mategemeo ni ingalau Mheshimiwa John Pombe Magufuli atupie jicho mkoa huu wenye potential kubwa sana,