Ukosefu wa Ajenda za Pamoja Unadumaza Mkoa wa Mbeya

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Tangu Uhuru Mkoa wa mbeya umekuwa na maendeleo makubwa ambayo yaliasisiwa na wawakilishi wa mkoa kipindi hicho akina John Mwakangale (Mbunge wa mbeya mjini 1960's) Eli Anangisye (Mbunge wa Rungwe mashariki) watu hawa walikuwa mashuhuri na wachapa Kazi waliacha historia katika mkoa.

Kuibuka kwa kizazi Cha pili Cha akina Professa Mark Mwandosya, David Mwakyusa na wengi ilikuwa chachu ya kuufanya mkoa wa Mbeya kuwa mfano wa kuigwa kwa mambo ya utetezi wa mkoa waliyoyafanya.

Mpaka sasa kizazi cha akina Joseph Mbilinyi, Mary Mwanjelwa, Tulia Akson, Sophia Hebron,Mwakyembe, Mwambalaswa na wengineo wote hawa kuna mchango wameuonesha japo bado hawaleti ushawishi unaostahili.

Hapo mwanzo Wana Mbeya na viongozi wao walikuwa na ajenda za maendeleo ambazo wote walizipa kipaumbele haijalishi walikua na tofauti gani za kisiasa wote waliimba wimbo mmoja ndio maana serikali ilileta maendeleo kukawa na Viwanda, Shule za kutosha vyuo vya ufundi na elimu na mengine mengi.

Kwa maendeleo haya ilitarajiwa mkoa wa Mbeya uimarike zaidi kufikia miaka ya sasa ambapo kuna uwanja wa ndege, Reli, Viwanda barabara na ardhi ya kutosha.

Mgawanyiko wa Viongozi katika ajenda za maendeleo umeathiri sana maendeleo ya mkoa mfano Viwanda vimekua Vikifungwa ama kuzalisha kwa kiwango cha chini jambo ambalo limepelekea kudorola kwa uzalishaji.

Ukijiuliza Wakulima wa chai kule Rungwe Wanafaidika na viwanda vilivyopo, jibu ni hapana kwa sababu wazungu wamepewa hivyo Viwanda na Wakulima wamebaki Kama watumwa sio sawa na zamani ambapo kulikwepo na ushirika Kama Kyela Rungwe Cooperative Union (KYERUCU) ambapo mkulima hakupata faida Kupitia Ushirika huo lakini shughuli za ushirika zilichochea maendeleo ya jamii.

Kwasasa mkulima anauza zao la chai lakini kwa bei ya chini shilingi 350 kwa kilo bei ambayo ni ya chini kwa wakati huu ambao pembejeo zinapatikana kwa gharama kubwa.

Kufa kwa kiwanda cha Zana za Kilimo Mbeya ambacho kiliuzwa kwa kampuni la CMG Lililokua likimilikiwa na kada wa Chama cha Mapinduzi Christopher Mwita Gachuma Kiwanda hicho hakizalishi hata fyekeo kwa miaka 20 sasa na kuua maendeleo ya kilimo kutokana na gharama za Kilimo kuwa kubwa.

Mwaka 2012 Wakati wa Maadhimisho ya mei mosi Rais wa awamu ya nne Jakaya kikwete alipokuwa akihitubia umati wa wafanyakazi katika uwanja wa Sokoine alisema " Ukanda wa kusini una mazao mengi ya kilimo serikali imetambua changamoto ambazo Wakulima wanazipata ikiwemo masoko ndio maana tunataka kuufanya Uwanja wa ndege wa songwe uwe wa kimataifa mkulima atoke na mboga, matunda na mazao mengine ya mau maua asubuhi akauze Amsadarm Uholanzi moja kwa moja".

Mpaka sasa Uwanja umekamilika kwa asilimia kubwa lakini hakuna hiyo ajenda kwa uongozi wa mkoa na wanasiasa wameshindwa kuishinikiza serikali ili iweze kuangalia ni kwa namna gani Inaweza kuwasaidia wakulima kwa kuwekeza ipasa vyo katika utafutaji masoko ya mazao.

Vivutio vya utalii vya Kimaajabu kama daraja la Mungu, ziwa Kisiba na Ngosi, Milima ya Livingstone na hifadhi ya kitulo, Pamoja na makumbusho ya kimisionari havijapewa uzito wa kutangazwa badala yake Viongozi wanatangaza vyama Kuliko fursa zilizopo Mkoani Mbeya.

Kuna wakati Viongozi wenyewe hurumbana kuhusu miradi ya maendeleo ambayo serikali kuu inataka kuwekeza mkoani Mbeya, Kama inavyotokea Sasa chuo Kikuu cha afya cha Muhimbili kinasuasua kujenga kampasi mpya mkoani Mbeya kwa sababu ya kukosa eneo tengefu la kujenga.

Baadhi ya Viongozi wamekuwa wakikataa kutoa ardhi katika maeneo yao kwa ajili ya uwekezaji wa chuo hicho kikubwa Cha masuala ya afya hapa nchini.

Jambo ambalo lilimpelekea mkuu wa chuo hicho Rais mstaafu Jakaya kikwete kutishia kuhamishia mradi huo mkoa mwingine iwapo serikali ya mkoa wa Mbeya itashindwa kutoa eneo la ardhi ya kutosha ujenzi.

Ukienda mkoa wa Kilimanjaro utalii ni ajenda mabango yamejaa barabarani kutangaza vivutio lakini mkoani Mbeya hakuna ajenda hiyo.

Kuna mambo mengi yamekosa ajenda mkoani Mbeya lakini hayo ni machache tu ya mfano, Rai kwa Wananchi Viongozi na Wanasiasa wabadilike Mbeya inataka ajenda kuliko marumbano.

1671263224032.jpg
 
Back
Top Bottom