Mbeya imepotea na Mark Mwandosya?

Mbeya imepotea na Mark Mwandosya?

hicho kiwanda cha chai nasikiwa wananchi wanauza bei ya aibu sana. nilikuwa naongea nao mwaka jana wanasema sema Tanga wanauza mara mbili yao na Kenya kama 3x. inatakiwa vipatikane viwanda vya chai,cocoa na kahawa ambavyo vitatoa brand kama Africafe hapo ndiyo kilimo kitakuwa na tija. kwenye mpunga watu wamejitahidi sana. Badala ya kumlilia Mwandosya tushauri wabunge waungane kutetea maslahi ya mkoa. labda kwa umoja wao wanaweza fika influence ya Mwandosya.
Kweli mkuu
Sera ya kubinafsisha viwanda vya Mwalimu na kuwapa matapeli huu ndio mfano wake mbaya.
Matapeli wanaoendesha kiwanda hicho wanawakamua wananchi mpaka wengine wanajitoa kuendeleza chai.
 
Katika swala la kusuasua kwa maendeleo ya nchi hii na sio Mbeya tu sababu kubwa ni mosi,ccm na sera zake ziliyofeli.Pili ni ubinafsi uliowajaa viongozi wa ccm na siasa zao za maji taka.Viongozi wa ccm hawataki kushirikiana na wapinzani kuleta maendeleo na hili wamekuwa wakilifanya kama mkakati wao wa kisiasa.Serikali kuu imekuwa ikizuia ama kuchelewesha miradi mikubwa katika maeneo yaliyo na upinzani.Sasa cha kujiuliza ni kuwa wanamkomoa nani na sisi wananchi tumulaumu nani? je tumlaumu mbunge anayepigania maendeleo yetu na akakwamishwa kwa wazi kabisa na serikali kuu ya ccm au tuilaumu na kuichukia serikali ya ccm inayokwamisha na kuzuia maendeleo kwa sababu ya siasa za maji taka? Wenye akili tunaelewa nini cha kufanya
 
Tuko pamoja mkuu.
Mwanzoni nilitegemea ile misa ya kuwashukuru wanambeya iliyofanywa na wakina Mwakyembe na Mwandosya baada ya kutoka Apollo ingekuwa na matokeo chanya kwa mkoa wa Mbeya.

Lakini hali imekuwa ni tofauti na matarajio ya wengi. Kwani waliofanya siasa za kimafia kwa icons wa Mbeya, leo wanapata uungwaji mkono na baadhi ya viongozi kutoka Mbeya!

Hili jambo linastaajabisha sana, hasa kwa viongozi wanaofahamu nafasi zao za kisiasa katika nchi hii!

Jifunzeni kwa mkoa wa Shinyanga na kanda ya ziwa kwa ujumla, mwaka 2010 wabunge wengi wa upinzani walitoka huko na kura nyingi za urais kwa upande wa upinzani zilitoka kanda ya ziwa lakini wabunge wa viti maalum wengi walitoka kwa wenye chama!

Hilo siyo jambo la kushangaza kwani inafahamika ubinafsi ni hulka yao, lakini 2015 Shinyanga, Simiyu na Mwanza hawakufanya ajizi na 2020 hawataambulia hata udiwani!

Watanzania wana chama kimoja cha siasa ambacho ni CCM, hivi vingine ni vyama vya kikabila, kikanda na kidini. Nasema hivi kwa sababu CCM haina mwenyewe, bali ina wapangaji na hawa wapangaji wanaondoka kila baada ya miaka 10 ili kupisha wapangaji wengine.

Kwa hiyo leo kwa mwingine, kesho inaweza kuwa kwako. Kinachohitajika ndani ya CCM ni uvumilivu wa kisiasa basi.!!
Haifai hata kuchangamana nao!
Inafaa kuwapatia elimu na kuwafahamisha kile kinachoendelea kwenye siasa za Tanzania, kwani vijana wengi hawajitambui.
Hoja yako imepotezwa na ubaguzi wako wa kikanda na kidini. Kwa taarifa yako Mimi naishi na kufanya kazi wilaya ya Magu. Kwa kilichotokea uchaguzi wa 2015 mikoa yenu ya usukumani hakipishani na chuki uijengayo hapa. Bukoba na Mara kwani sio kanda ya Ziwa? Mbona walichagua upinzani kwa kishindo?

Ktk mikoa ambayo wapiga kura ni duni kifikra(hasa elimu ya uraia) ni hiyo mikoa uliyoitaja. Vibiriti, Chumvi ndio vilikua bora kwenu. CCM kwangu sina imani nayo hata kidogo and napigia chapuo Mbeya upinzani uchaguliwe ili serikali yenu itambue.

Tangu enzi za Nyerere serikali imekua ikiitenda mbeya isivyo. Rejea Nyerere kumuweka John Mwakangale(Mungu amrehemu) ambaye shule ilikua tatizo almradi tu afanikishe malengo yake kisiasa. Njoo kwa kwa Kikwete na picha yake na John Mwakipesile utaelewa.

Mbeya watu wake hata wawe duni kiasi gani visasi wanajua kuvifuga na hawasahau. Huyu bwana wa Ss no wonder siku akienda huko labda afanye makubwa yatayowapooza watu dhidi ya kutengwa na serrikali watamuelewa.
 
1011273_10204474974252892_1059767986913548766_n.jpg

Mkuu matatizo ya Mark Mwandosya na Mkoa wa Mbeya yalianza na Mtandao wa Kikwete.
Kosa ilikuwa kuwa wa tatu katika kinyang'nyiro cha urais mwaka 2005.

Jamaa alipgwa vita na Lowasa , alipigwa vita na Mkuu wa Mkoa Mwakipesile, alipigwa vita na hata CCM yenyewe mpaka ikawa mbaya.
Watu wa Mbeya nawafahamu, vijana kuingia kushabikia CHADEMA ilikuwa a direct reaction kwa nguli wao kupigwa vita vya wazi wazi.
Nakumbuka Waziri Mkuu Lowasa wakati huo alipotembelea Mbeya, Mwandosya aliimbiwa "Raisi...raisi....raisi..." na vijana wa Mbeya mjini.
Kitendo hicho kilimuudhi sana Lowasa, lakini hiyo ilielezea jinsi Mwandosya alivokubalika sana mkoani Mbeya, tena na makabila yote mkoani.

The powers that be wakati huo waliamua kumdhibiti Mwandosya kisiasa.
Kugombea NEC mwaka 2007 walimwekea kijana mdogo anaitwa Thomas Mwang'onda, mtoto wa kigogo wa sekta ya intellijensia, Abson Mwang'onda.

Fedha nyingi sana zilitumika kumnadi Thomas, kiasi kufikia bilioni moja.
Lakini kijana Thomas aliangukia pua!
Mwandosya aliwahi kulalamika katika kitabu kimoja jinsi alivyokuwa akipigwa rafu, na serikali yake, na chama chake CCM!
Hatuwezi kuunganisha , lakini mara Mwandosya aliyekuwa akionekana fit na anafanya mazoezi kila alipopata wasaa mitaani, akaanza kuugua.
Wengine wanadai aliwekewa sumu kama ile ya Dr Harrison Mwakyembe, lakini hilo halijathibitishwa.

Kugombe tena mwaka 2015 ilikuwa just going through the motions, Mwandosya alisha umizwa vibaya.
Mwishoni alipoishiwa nguvu masikini Mwandosya akaamua kurudi kupumzika kijijini kwake Lufilyo, Zaidi ya kilometa 100 toka hata mjini tukuyu.

Kwa maoni yangu serikali ya CCM ndiyo iliyo utoa mkoa wa Mbeya kwenda CHADEMA, kwa kumdhibiti kipenzi cha wana Mbeya, Prof Mark mwandosya.
Mategemeo ni ingalau Mheshimiwa John Pombe Magufuli atupie jicho mkoa huu wenye potential kubwa sana,
Mkuu mabadiliko hutokea baada ya mmoja kufanya makosa makosa ya ccm ndo faida kwa chadema nao chadema wakifanya makosa tunaweza kushuhudia chama kingne kikiweka ngome
 
Achia tu hao wapinzani wapindue sugu ataung'arisha kama walivyoona inafaa na kwetu pia inafaa tu!kwani mby nini bana.
Mbeya nini, sumu ishasambaa Njombe, Iringa na Ruvuma, maneno yenu yanazalisha kanda nyingine itakayowasumbua bila kujua muendelee kuropoka tu bila kutumia busara
 
masopakyindi ,

..hivi Mwakyembe na Mwandosya walipewa sumu?

..kwa mtizamo wangu kilichozima ndoto za Prof.Mwandosya ni maradhi yaliyompata.

..lakini hata kama angekuwa imara kiafya na ccm wakampitisha angepata wakati mgumu sana kwasababu siamini kama anaendana na siasa za wakati huu za hapa Tz.

..siasa za Tz na wapiga kura zinahitaji mgombea MACHACHARI kama JPM. Prof.Mwandosya yuko baridi na ni msomi-msomi sidhani kama waTz wangempa kura mgombea wa aina hiyo.
 
Mbeya nini, sumu ishasambaa Njombe, Iringa na Ruvuma, maneno yenu yanazalisha kanda nyingine itakayowasumbua bila kujua muendelee kuropoka tu bila kutumia busara
Mkuu kwani siasa nayo ugomvi?Ina maana wewe hutaki wapinzani nao watawale siku moja?nini basi maana ya vyama vingi! Kubali kataa one day yes!wajipange tu mbona unawaita sumu unataka tuwaue?Mie kwangu boss kubwa anachama chake na mie changu,watoto chao na maisha yanasonga bila shari.
 
Ubaguzi wangu uko wapi hapo?
Hakuna chuki zaidi ya ukweli. Mwaka 2010 tuliwapokea, mwaka 2015 tukawakataa na mwaka 2020 hata udiwani hawatapata!

Hivi wewe kipindi Ukerewe, Ilemela, Nyamagana, Meatu, Maswa Mashariki na Maswa Magharibi zinaenda upinzani mwaka 2010 huko Kagera na Mara walikuwa na majimbo mangapi ya chadema?

Hapa bado hujaangalia kura za urais na idadi ya madiwani kwa kila jimbo. Ninavyokwambia tuliwapokea kwa mikono miwili namaanisha lakini sasa hivi tumewakataa!

kama kigezo cha elimu ya uraia ni kuichagua chadema na kuikataa CCM ni sawa, sisi tuna fikra duni na hatuna elimu ya uraia.
Sanduku la kura litaamua, maneno matupu hayasaidii!

Siasa bila mikakati ni sawa na kazi bure. Kinachotakiwa ni nyinyi kujipanga bila kujali itikadi za vyama, kusimamisha watu wenye sifa za kuweza kushika nyadhifa zozote iwe ndani ya chama au serikalini.

Hili la kupandikiziwa watu wasiojielewa hata sisi lilikuwepo, ni mbinu ya kisiasa inayotumiwa na vyama vyote ili mamlaka kutoka juu iweze ku-dominate sehemu fulani bila ya kuwa na ugumu wowote. Sasa subiri uone sisi mwaka 2020 tutakavyosimamisha wawakilishi wetu.

Kinachotakiwa ni kufahamu kuwa nyanda za juu kusini hasa Mbeya ni potential kwa siasa za Tanzania. Sasa kutokana na nafasi yenu ya kisiasa ndani ya nchi hii mmejipanga vipi?

Kumuelewa au kutomuelewa kwa kipindi hiki haitasaidia kwa sababu yeye tayari ni rais na kumbebesha makosa ya viongozi waliopita mtakuwa mnamuonea.

Lakini jukumu bado lipo kwenu, huyu kiongozi amekuja na atapita, atakuja mwingine atapita vile vile. Msisubiri kufanyiwa makubwa na serikali kuu, kinachotakiwa ni kujiimarisha kisiasa haya mengine yatakuja tu.
Kushindwa kwa upinzani ktk uwakilishi bungeni huko kwenu inaeleweka ni nyota ya ukabila wa magufuri dhidi ya vyama vingine, mastermind wa kuchafua images zao ni chama chako cha ccm. Nyamagana mlipiga kampeni Usukuma wa mabula dhidi ya Ujaluo wa Wenje hadharani.

2010 inaeleweka fika uchaguzi ulikua Juma dhidi ya Peter ndio maana kura na viti vingi vilipatikana. Mkoa wa mbeya kuendelea ni juhudi binafsi za wanambeya as serikali ni wazi iliiona mbeya ya muhimu Joyce Banda aliposema ni sehemu ya Malawi.
 
Kwan alikuwa profesa wa engineering MIT au hapa udsm katika nchi ambayo bajeti yake ya utafiti ni 1/5 ya bajeti ya Kenya ya utafiti? Kuwa mwanataaluma sio Ishu ktk nchi hii, ukitaka kufanya mabadiliko ya kweli inabidi uingie kwenye siasa ili wababaishaji wote wasipate fursa ya kutuongoza. Baada ya Mwalimu Nyerere, ungetegemea tupate vichwa kweli kutuongoza, lakini wapi.

Mkuu acha kufeli,mchizi alipata 5.0GPA undergrad pale FoE akaenda Birmingham,peleka wazungu to the end akapata uprofessor at very young age,he was the youngest electrical professor ever...

Dogo alikua hafai kabisa hata kwa kuchomelea....tumepita FoE tunamjua sana...dogo alikua genius Luhanga anasubiri sana...Luhanga alipita stages one by one,Mark aliruka ujinga wote,na marks zake were perfect scores....
 
1011273_10204474974252892_1059767986913548766_n.jpg

Mkuu matatizo ya Mark Mwandosya na Mkoa wa Mbeya yalianza na Mtandao wa Kikwete.
Kosa ilikuwa kuwa wa tatu katika kinyang'nyiro cha urais mwaka 2005.

Jamaa alipgwa vita na Lowasa , alipigwa vita na Mkuu wa Mkoa Mwakipesile, alipigwa vita na hata CCM yenyewe mpaka ikawa mbaya.
Watu wa Mbeya nawafahamu, vijana kuingia kushabikia CHADEMA ilikuwa a direct reaction kwa nguli wao kupigwa vita vya wazi wazi.
Nakumbuka Waziri Mkuu Lowasa wakati huo alipotembelea Mbeya, Mwandosya aliimbiwa "Raisi...raisi....raisi..." na vijana wa Mbeya mjini.
Kitendo hicho kilimuudhi sana Lowasa, lakini hiyo ilielezea jinsi Mwandosya alivokubalika sana mkoani Mbeya, tena na makabila yote mkoani.

The powers that be wakati huo waliamua kumdhibiti Mwandosya kisiasa.
Kugombea NEC mwaka 2007 walimwekea kijana mdogo anaitwa Thomas Mwang'onda, mtoto wa kigogo wa sekta ya intellijensia, Abson Mwang'onda.

Fedha nyingi sana zilitumika kumnadi Thomas, kiasi kufikia bilioni moja.
Lakini kijana Thomas aliangukia pua!
Mwandosya aliwahi kulalamika katika kitabu kimoja jinsi alivyokuwa akipigwa rafu, na serikali yake, na chama chake CCM!
Hatuwezi kuunganisha , lakini mara Mwandosya aliyekuwa akionekana fit na anafanya mazoezi kila alipopata wasaa mitaani, akaanza kuugua.
Wengine wanadai aliwekewa sumu kama ile ya Dr Harrison Mwakyembe, lakini hilo halijathibitishwa.

Kugombe tena mwaka 2015 ilikuwa just going through the motions, Mwandosya alisha umizwa vibaya.
Mwishoni alipoishiwa nguvu masikini Mwandosya akaamua kurudi kupumzika kijijini kwake Lufilyo, Zaidi ya kilometa 100 toka hata mjini tukuyu.

Kwa maoni yangu serikali ya CCM ndiyo iliyo utoa mkoa wa Mbeya kwenda CHADEMA, kwa kumdhibiti kipenzi cha wana Mbeya, Prof Mark mwandosya.
Mategemeo ni ingalau Mheshimiwa John Pombe Magufuli atupie jicho mkoa huu wenye potential kubwa sana,
Autupie jicho kivipi?uende ccm au?halafu we lijamaa inaonekana utawala huu unakuchefua na mda si mrefu utaitukana ccm waziwazi...ulitoa sana povu enzi za m.kw.ere,au ndio wapiga dili wenyewe?!!!
 
Autupie jicho kivipi?uende ccm au?halafu we lijamaa inaonekana utawala huu unakuchefua na mda si mrefu utaitukana ccm waziwazi...ulitoa sana povu enzi za m.kw.ere,au ndio wapiga dili wenyewe?!!!
Mi mwana CCM damu damu na uzuri wa demokrasia ni kusema kila kinachoenda kombo ili hata JPM apate habari, kwa nyie mnao mdanganya.
JPM rais wa wote.
Sinyi sumu wala sijinyongi, CCM pamoja na mapungufunyake ni.mbere kwa mbere!
 
Attachments

Mkuu acha kufeli,mchizi alipata 5.0GPA undergrad pale FoE akaenda Birmingham,peleka wazungu to the end akapata uprofessor at very young age,he was the youngest electrical professor ever...

Dogo alikua hafai kabisa hata kwa kuchomelea....tumepita FoE tunamjua sana...dogo alikua genius Luhanga anasubiri sana...Luhanga alipita stages one by one,Mark aliruka ujinga wote,na marks zake were perfect scores....
Mi hapo sijaona cha ajabu. Labda ungenitajia patents zake ndo ningeona maajabu. Uprofessor wa science and technology ni products na patents, sio sifa za kusema nilikuwa wa kwanza darasani.

Hiyo ndo tofauti ya MIT na vyuo vingine .
 
Mi mwana CCM damu damu na uzuri wa demokrasia ni kusema kila kinachoenda kombo ili hata JPM apate habari, kwa nyie mnao mdanganya.
JPM rais wa wote.
Sinyi sumu wala sijinyongi, CCM pamoja na mapungufunyake ni.mbere kwa mbere!
Mbona wakati wa jk ulikuwa unatetea kila ujinga!!sio bure dili zako ovu zimeminywa
 
Haya ni maneno tu baada ya kushindwa uchaguzi lakini hayawezi kubadilisha uhalisia.

Kwanini hivyo viti havikupatikana Arusha ambako kuna wakina Peter pia na mgombea urais ndipo alipotoka?

Huwezi kuelezea mafanikio ya chadema kuelekea chama kikuu cha upinzani bila kutaja nafasi ya kanda ya ziwa [hasa usukumani] katika uchaguzi mkuu wa 2010.

Hiyo yote itabaki historia lakini kuwa na mikakati imara ya kisiasa itakuja kuwapa faraja siku za mbeleni.

Mtumieni Mwandosya na wengine mnaoamini watawasaidia, siyo kuamini vinara wa upinzani ambapo kwa mara ya kwanza mliamini ndiyo waliokwamisha baadhi ya miradi iliyotakiwa kufanyika Mbeya.
Tutawatumia upinzani hili ndilo chaguo letu, nyinyi huko kwenu watumieni ccm. Huu ni uhuru wetu kama nyinyi mlivyo amua kuchagua ccm na msukuma mwenzenu. Na sie huku tutaendelea na upinzani as nafsi zetu zinakongwa nao.
 
Mbona wakati wa jk ulikuwa unatetea kila ujinga!!sio bure dili zako ovu zimeminywa
Usiwe na wasi mkuu, hivi kwa umri uliofikia umewahi kusikia mfanya biashara aliyekufa kwa kukosa biashara.
Hata sasa tunamtetea JPM katika kila kitu.
Nyie wajinga wajinga ndo msiolielewa hilo kuwa kelele zenu za mlango hazitunyimi usingizi.
 
nafikiri mjinga ni wewe uliyedhani utaendelea kupiga dili kwa vile una kadi ya ccm,sasa hivi unaisoma namba huishi kukosoa lakini kwa watu kama sisi tunaotunza kumbukumbu hutotupata na unafiki wako wa kukosoa utawala huu(haimaanishi naunga mkono baadhi ya matendo ya awamu hii)..usirudie kuleta ujinga wako humu sababu bado tuna kumbukumbu za upuuzi wako wa kutetea kila kitu cha magamba ukiwa unapiga dili..
 
Back
Top Bottom