Mbeya: Raia wa Rwanda ashikiliwa kwa kusafirisha Dawa za Kulevya

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,420
5,780

Unga.JPG

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili akiwemo raia wa nchini Rwanda, Assouman Gahigiro [48] na Winny Bruno [31] mkazi wa Kiwira Wilaya ya Rungwe kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya Bhangi kilogramu 20.

Watuhumiwa walikamatwa Januari 27, 2024 katika kizuizi cha Polisi cha Kayuki kilichopo barabara kuu ya Kyela – Tukuyu ambapo watuhumiwa walikuwa abiria kwenye gari iliyokuwa ikitokea Kyela kuelekea Mbeya Mjini, Askari waliokuwepo eneo hilo walilisimamisha gari hilo na kufanya ukaguzi na ndipo walibaini Bhangi iliyokuwa imefichwa kwenye vifungashio vya Nylon na kuwekwa ndani ya begi la nguo.

IMG_8246.JPG

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na upelelezi kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji ili kubaini uhalali wa mtuhumiwa Assouman Gahigiro kuwepo nchini wakati taratibu nyingine za kumfikisha mahakamani kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya zikiendelea.

Sambamba na hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mkazi wa Mbezi Jijini Dar es Salaam Maulusi Samweli @ Mtui [35] kwa tuhuma za kupatikana na nyara za serikali meno mawili ya Tembo yenye uzito wa kilogramu 10 bila kuwa na kibali.

Mtuhumiwa alitiwa mbaroni Januari 27, 2024 katika msako uliofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Uhifadhi [TANAPA] katika Kijiji cha Mlungu kilichopo Kata ya Miyombweni, Wilaya ya Mbarali na kumkamata mtuhumiwa akiwa ameficha meno hayo kwenye mfuko wa sandarusi akiwa kwenye harakati za kutafuta wateja.

Upelelezi uliofanywa awali umebaini kuwa mtuhumiwa ni mwindaji haramu, msafirishaji na muuzaji wa nyara za serikali, atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
 
Back
Top Bottom