Mbeya: Barabara yapigwa sementi badala ya lami

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
HOT NUUZ!! SAKATA LA KUTENGENEZA BARA BARA YA LAMI KWA KUTUMIA CEMENT: MKURUGENZI WA JIJI ASEMA BARABARA IMETENGEWA MILIONI 400 KWA AJILI YA UKARABATI

Hii ndio Bara bara ya Mbalizi Road Maeneo ya Hospitali ya wazazi Meta Jijini Mbeya, Ikiwa imezibwa viraka kwa kutumia Cement

Baadhi ya Viraka vikiwa vimezibwa

Mafundi wakiwa bize wanahangaika kuziba viraka hivyo

Wafanya kazi wa Jiji wakiendelea kukoroga zege tayari kupeleka kuziba viraka katika bara bara ya lami

Shughuli ya kuziba viraka kwa kutumia cement imekamilika, Inasubiri kukauka magari yaanze kupita

Mafundi wakiendelea kuziba mashimo ya Bara bara kwa Kutumia Cement

Mkurugenzi wa Jiji La Mbeya akiongea na waandishi wahabari

Mmoja wa Waheshimiwa Madiwani akihoji juu ya uzibaji wa viraka vya bara barani, na kusema kama vinafaa akawambie wananchi nao waanze kuziba bara bara hizo kwa kutumia Cement

****************************

Mbona post yako haina maoni?, tatizo ni nini hapo?, ni kuziba viraka kwa sement?! Au ni barabaa kuharibika? Au unadhani sementi haijengi barabara?!, nijuavyo mimi siyo lami tu ndiyo hutengeneza barabara: baadhi ya brbr za ulaya hutengenezwa kwa material mbadala kama vile crankers na au polymers(soil binders) na brbr huwa imara kuliko lami. Hata south africa sasa wanatumia polymers. Sementi hutengeneza brbr imara zaidi kuliko lami; mf: brbr za kiwanda cha sement -songwe mbeya zimejengwa kwa sement na hubeba mitambo mizito zaidi. Kwa hiyo barabara ikitengenezwa kwa sement bila uchakachuaji huwa imara zaidi.
 
Kama uwekaji wa cement ndiyo hatua ya mwisho katika ujenzi/ukarabati huo, basi kwa ufahamu wangu, pia naweza kupata mashaka. Lakini kama utumiaji huo wa cement ni sehemu ya process, hapo hakuna tatizo.
Nakumbuka Wakati inajengwa na wachina barabara ya Sam Nujoma, kuna layer iliwekwa cement kuanzia Mwenge hadi Ubungo.
 
Mi naona haina taabu, kama lami ni ishu saruji inaweza kutumika kuziba viraka, kama ilivyo pale Kitonga.
 
Mbona post yako haina maoni?, tatizo ni nini hapo?, ni kuziba viraka kwa sement?! Au ni barabaa kuharibika? Au unadhani sementi haijengi barabara?!, nijuavyo mimi siyo lami tu ndiyo hutengeneza barabara: baadhi ya brbr za ulaya hutengenezwa kwa material mbadala kama vile crankers na au polymers(soil binders) na brbr huwa imara kuliko lami. Hata south africa sasa wanatumia polymers. Sementi hutengeneza brbr imara zaidi kuliko lami; mf: brbr za kiwanda cha sement -songwe mbeya zimejengwa kwa sement na hubeba mitambo mizito zaidi. Kwa hiyo barabara ikitengenezwa kwa sement bila uchakachuaji huwa imara zaidi.

Mengine (matumizi ya cement badala ya lami) sina uhakika nayo so siwezi kuyaongelea, ila hapo kwenye ubluu hapo ndo najua hapa kwetu ni ngumu kutokea kwenye mambo ya utengenezaji barabara. Hata kama sio mkandarasi mwenyewe atakayechakachua basi vibarua watachakachua!
Kwenye miradi mingi ya barabara watu wanauza hadi kokoto zilizopaswa kutumika kutengenezea, je cement sasa!?

Nionavyo mleta mada kinachomsumbua ni kutumia simenti badala ya lami. Hilo si tatizo kabisa, na mfano wa karibu ni pale mlima Kitongo, ile lami ilishindwa kuhimili uzito wa magari makubwa na ikawa kama inasambaa na kutengeneza mifereji yapitamo matairi. Lakini walipotengeneza kwa simenti barabara sasa iko salama. na kama kitonga bado ingekuwa na lami, hizi mvua za majuzi zingeing'oa kabisa. Kitaalam maji na hasa yatuamayo kwenye lami huleta madhara kwa kudhoofisha nguvu ya lami.
Kwenye matumizi ya simenti kinachojalisha ni matumizi ya ratio sahihi kwa matumizi husika. Nawasilisha.
 
Bara nyingi ulaya ni asphalt si tarmac ,isitoshe kwa mujibu wa ushahidi picha ni inaonesha jamaa wanajaribu ku maintain uharibikaji wa barabara hamna mbaya kama italeta athari chanya hapo ndugu yetu.
 
tambueni kuwa matakwa ya ujenzi pale ni lami, kinyumechake ingejengwa kwa siment toka mwanzo na ni yote kukidhi matakwa ya udongo husika, ene wei iangaliwe BOQ tujue kama mkandarasi ameelekezwa kutumia simenti kwa gharama ya lami, au simenti kwa gharama pungufu ya lami. ni nini mshauri mwelekezi aliagiza kifanyike. mimi nadhani inawezekana wanambeya mmeibiwa! watu wamevunja sheria lakini wamefuata kanuni!!! bananeni kitaeleweka tu.
 
kuna aina ya rami ambayo huwa tayari kwa matumizi na inafungwa ktk ujazo tofauti kwenye mifuko kama ya cement, unaponunua ni kujaza tu ktk sehemu husika na kuishindilia. Mfaano mmojawapo ni MATREX hi ni nzuri na inadumu kuliko hata cement ambayo inaweza kukatika iwapo mahala husika patakuwa na uzito kuzidi uwezo wake.
 
Tatizo ni kuziba mashimo ya lami kwa simenti.......lami na simenti vina elasticities tofauti na hivyo mashimo yatarejea punde tu....ni sawa na kuziba pancha kwa bati

Kwa waliosoma Arts kuanzia Form I ni ngumu kuelewa "elasticity"!

Cement haiwezi kuziba "kiraka" cha barabara ambayo imetengenezwa awali kwa kiwango cha lami - Ni uendawazimu and mostl likely UJINGA!
 
Mi nahisi nimekuelewa tofauti kidogo mleta mada.

Nazani tatizo kubwa hapa nikujenga kwa cement wakati wamepewa fungu(fedha ) za kujenga kwa rami.

Minaomba wataalam watujuze tofauti ya gharama ya ujenzi wa barabara kwa kutumia rami na kutumia cement kipi kinagharama zaidi??
 
Mkuu,

Hakuna ujenzi hapo........ni ukarafyati(sio ukarabati)
 
Kwanza hata ukiangalia ni kichekesho. Sawa na suruali yako nyeusi lkitatuka uiwekee kiraka cha kaki!!!!!!! Inashangaza. Haitakuwa na uwiano sahihi. tutambue kwamba hivi vvitu viwili yaani cement na lami haviendani, hivyo baada ya muda mfupi ukipita hapo na gari utahiisi either umeingia kwenye shimo, ama umepanda tuta kutegemeana na kipi kitatitia zaidi.
 
kuna aina ya rami ambayo huwa tayari kwa matumizi na inafungwa ktk ujazo tofauti kwenye mifuko kama ya cement, unaponunua ni kujaza tu ktk sehemu husika na kuishindilia. Mfaano mmojawapo ni MATREX hi ni nzuri na inadumu kuliko hata cement ambayo inaweza kukatika iwapo mahala husika patakuwa na uzito kuzidi uwezo wake.
 
jamani angalieni bara bara ya lami hiyo ....itawekwaje viraka vya sementi? eti hadi ulata wanafanya...ulaya gani? kuweka viraka ka cement kwenye bara bara ya lami? sijaona
 
Hii hata kabla ya kuangalia hizo picha nilianza kucheka kwa kukumbuka "Visa vya Pwagu na Pwaguzi" pale walipotengeneza barabara kwa kuweka mkaa badala ya lami.
waMbeya, "manyoya hayo, kuku kaliwa zamani".
 
Back
Top Bottom