muuza ubuyu
JF-Expert Member
- Nov 23, 2010
- 3,511
- 3,477
Habari wakuu,
Mwezi wa kumi na moja nina safari ya kwenda Lushoto kwa kutumia usafiri binafsi. Kiufupi mimi ni mgeni katika mkoa wa Tanga na sijui hali ya barabara mkoani humo. Ninaishi kwenye moja ya mikoa ya kanda ya magharibi mwa Tanzania.
Barabara ninayotaka kutumia ni ile ya kutoka Dodoma kwenda Morogoro. Ningependa kupita njia fupi pindi nitakapofika Dumila, yaani nitumie barabara ya Dumila - Handeni - Korogwe (wastani wa kilomita 230 kwa mjibu wa google map).
Kwa wenyeji wa mkoa huu au wale waliowahi kutumia barabara hiyo, ningependa kupata maelekezo yenu yatokanayo na uzoefu wenu, je barabara hii Dumila - Korogwe ni lami? Kama ni ya vumbi, inapitika wakati wa masika?
Asanteni sana.