Mbeya: Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani acheni Rushwa, simamieni sheria

Mwanongwa

Senior Member
Feb 15, 2023
169
198
Wananchi wanaotumia Barabara ya Mbeya - Chunya wamelitaka Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani, askari wake kuacha kuchukua rushwa na badala yake wasimamie sheria.

Wananchi hao wamelalamikia kitendo cha mabasi ya Mbeya -Chunya kuzidisha abiria kinyume cha utaratibu.

Mabasi yanayotoka Mbeya Mjini kwenda Wilayani Chunya yamekuwa na utaratibu wa kuzidisha abiria na pindi abiria wanapolalamika wamekuwa wakitolewa kauli chafu na makondakta wa mabasi hayo.

Mabasi aina ya Coastal yana uwezo wa kubeba abiria 29 lakini yamekuwa yakibeba abiria zaidi ya 40.

Askari wa kituo cha ukaguzi cha Isanga Mbeya Mjini na Kawetele Mbeya Vijijini wamekuwa wakichukua rushwa na kuruhusu gari hizo kuendelea na safari.

Kwa mfano siku ya leo tarehe 21 Machi 2023 basi aina ya Coastal (WASAFI) lilizidisha abiria likitokea Mbeya Mjini kwenda Chunya lilipofika kwenye vituo hivyo vya ukaguzi konda alishuka na kwenda kwa askari ambao walikuwa wanasimama ubavuni mwa gari na kuwapatia elfu mbili mbili.

Hali hiyo imekuwa kero kwa wasafiri maana imekuwa ikihatarisha usalama wao na ikumbukwe kuwa barabar hiyo ndiyo yenye kona Kali ambazo kwasasa mkoa umezigeuza kuwa vivutio.

Mabasi hayo hayaanzi safari pale stand ya Airport ya zamani mpaka wahakikishe yamejaa, huku kwenye eneo ambalo wanatakiwa kukaa abiria wa nne wanalazimisha wakae watano.

Tukiachana na mwendo kasi na ubovu wa vyombo vya usafi, chanzo kingine cha ajali ni gari kuzidisha mzigo/abiria tofauti na uwezo wake.

IMG_20230321_093805_0.jpg
 
Rushwa ya polisi haiwezi kwisha maana ni mfumo wa maisha yao. Kwa nchi hii ni ngumu kutenganisha upolisi na rushwa.

Waendesha vyombo vya usfiri na wangaikaji wengine watakubaliana na mimi.

Kuna wakati raia inabidi achague kati ya rushwa na uhai wake.

Hii ni nchi nzima sio huko mbeya tu
 
Wananchi wanaotumia Barabara ya Mbeya - Chunya wamelitaka Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani, askari wake kuacha kuchukua rushwa na badala yake wasimamie sheria...
Tanzania hii wenye uwezo wa kutokomeza rushwa ni
1rais
2 makamu wa rais
3 waziri mkuu
4 spika
5 jaji mkuu

Bahati mbaya hawa wote wako likizo tuwasubili warudi

Dawa nyingine ni kuwaomba matajiri kupeleka mafali kwa wingi
 
Back
Top Bottom