Himidini
JF-Expert Member
- May 8, 2013
- 5,534
- 4,193
^^
Nimepokea simu toka kwa rafiki yangu kipenzi,
Huyu tumekua nae,tumecheza nae,tumesoma nae ananijua vizuri nami namjua vizuri
...
Lakini simu yake haikuwa ya furaha siku zote,iliambatana na kulia.Kilio cha mtu mzima,kilio cha mwanaume..kilio kilichonikumbusha niliyopitia.
...
Pamoja na kuwa na watoto wawili na mkewe,lakini hilo halikumzuia mkewe kumuacha mumewe,kukimbia na watoto na rafiki yangu kubaki bila kujua afanye nini!
...
Shemeji yangu huyu ambae nilimheshimu sana,aliyesifika kwa sifa za kuweza kumuita mke mwema,alianza visa na vituko vya hapa na pale.Viburi na ugomvi usio na sababu ulizidi kila uchao.Hata hivyo juhudi za majirani na wazazi wa pande zote walifanikiwa kusuluhisha.Ugomvi ukapoa,amani ikarejea na familia ikatulia
...
Kumbe maji yaliyotulia yana kina kirefu na ukitaka kujua urefu wa maji muulize chura.Na siku zote mambo huwa kinyume na yanavyoonekana.
Rafiki yangu alipokuwa safari ya kikazi Zanzibar (anafanya utalii) mkewe aliyemuacha mwanza,,aliuza kila kitu cha ndani,,akabeba watoto na kutoweka kusikojulikana.
...
Mume aliporudi akakuta ndani patupu.Akauliza kwao,hakuna,ndugu na jamaa wapi! Akaenda kijijini wapi!
Akalia, Akatulia
...
Juma lililopita akaambiwa na msamaria alipoolewa! Kapata tajiri,,amewekwa ndani,,mume mpya anasema anampenda atalea watoto.
Rafiki yangu anafanya utaratibu wa kuwarudisha watoto hata ikibidi kisheria,awapeleke kwa babu na bibi zao. Ni watoto wawili.
...
Naam sauti ya majonzi na huruma ya rafiki yangu imenikumbusha,mchoro wa katuni ktk gazeti moja la Kenya lililoonyesha masikini akiambiwa na tajiri ambae alimtapeli mchumba wake kwa kumwonyesha PESA,, tajiri huyo alimkebehi masikini kwa kusema ' I TOLD YOU,,I WILL CALM HER DOWN'
...
Nimeamini mbele ya pesa,kila goti la mwanamke litapigwa