Mbeki agrees to resign - Democracy at work

But he had been under pressure to quit after a judge ruled last week that he had instigated corruption charges against Zuma, AP said. African President Mbeki to quit

Duh! bonge la point, I mean this is wasup!
 
Mbeki akubali kuachia kiti ya urais Afrika Kusini

Andrew Msechu wa Gazeti la Mwananchi kwa msaada wa mashirika ya habari

RAIS Thabo Mbeki wa Afrika Kusini amekubali kujiuzulu, baada ya Kamati Kuu ya Chama cha African National Congress (ANC) nchini humo kumtaka aachie madaraka ya urais kabla ya kumalizika muda wake mwakani.

Hatua hiyo ya Mbeki inafuatia maamuzi ya chama hicho tawala yaliyotolewa jana, baada ya kumalizika kwa kikao chake cha dharura cha siku mbili, kilichoitishwa maalum kwa ajili ya kujadili hatima yake.

“Kufuatia uamuzi wa Kamati Kuu ya Chama cha ANC kumtaka Rais Mbeki aachie madaraka, rais amekubali na ataachia rasmi madaraka yake baada ya taratibu zote za kikatiba kukamilika,” ilieleza taarifa ya ofisi ya Mbeki.

Akitangaza uamuzi huo wa Kamati Kuu ya ANC mara tu baada ya kumalizika kwa mkutano wake wa siku mbili jana, Katibu Mkuu wa ANC, Gwede Mantashe alieleza kuwa Mbeki ambaye alichukua madaraka ya nchi hiyo baada ya Rais wa awali, Nelson Mandela kumaliza muda wake mwaka 1999 na akitkiwa kumaliza muda wake Aprili mwakani, alisema kuwa tangu awali Mbeki alipokea vizuri uamuzi huo na yuko tayari kutoa ushirikiano.

“Baada ya majadiliano magumu na ya muda mrefu, ANC imeamua kumwagiza rais Mbeki kuachia madraka kabla ya kumalizika kwa muda wake wa uongozi, mwenyewe hakushtuka na amekubali kutoa ushirikiano katika maamuzi hayo,” alisema Mantashe.

Aliongeza kuwa pamoja na kujiuzulu kwa Mbeki, ANC imeagiza mawaziri katika baraza la Mbeki kuendelea na nyadhifa zao katika kipindi chote cha mpito ili kulinda uimara wa serikali ya nchi hiyo, akiwemo rafiki yake wa karibu, Waziri wa Fedha, Trevo Manuel.

Kufuatia uamuzi huo wa ANC, Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Phumzile Mlambo-Ngcuka ambaye anatarajiwa kukaimu kwa muda urais pia ameonyesha dalili za kutaka kujiuzulu iwapo Mbeki ataachia madaraka.

Msemaji wa Ngcuka, Denzel Taylor alieleza jana kuwa makamu huyo wa rais anatarajiwa kuwasilisha barua yake ya kujiuzuu mara tu Mbeki atakapofanya hivyo.

“Ninawahakikishia kuwa makamu wa rais atajiuzulu iwapo rais ataamua kufanya hivyo. Hii inatokana na ukweli kuwa yeye ameteuliwa na rais na amekuwa akishirikiana naye kwa karibu, hivyo anaona kuwa ni suala sahihi na uamuzi mzuri kwake kujiuzulu pamoja na rais,” alisema.

Uamuzi huo wa ANC unatarajiwa kutekelezwa mapema iwezekanavyo na bunge la nchi hiyo ambalo linatawaliwa na wabunge wengi kutoka ndani ya hama hicho wanatarajiwa kumchagua rais mpya atakayemrithi Mbeki ndani ya siku 30 baada ya rais kutangaza rasi kujiuzulu.

Spika wa Bunge hilo, Beleka Mbete anaelezewa kwua mtu wa kaibu wa kiongozi mkuu wa chama hicho cha ANC, Jacob Zuma ambaye amekuwa katika mgogoro wa kisiasa wa muda mrefu na rais Mbeki tangu alipomuondoa katika adhifa wake wa makamu wa rais kufuatia tuhuma za rushwa katika ununuzi wa silaha mwaka 2005. Iwapo rais pamoja na makamu wake watajiuzulu, spika huyo ndiye anayetarajiwa kukaimu kwa muda nafasi ya rais, kabla ya kuitisha uchaguzi ndani ya bunge.

Hatua hiyo ya ANC inafuatioa tuhuma na lawama dhidi ya Mbeki kuwa amekuwa akishinikiza mashtaka ya rushwa dhidi ya Zuma kwa maslahi yake, ikiwemo kumzuia kuwania urais wan chi hiyo baada ya muda wake kumalizka.

Hali ya kisiasa ilizidi kuwa mbaya zaidi kwa Mbeki, baada ya mahakama kuu nchini humo kutupilia mbli mashtaka ya rushwa yaliyofunguliwa dhidi ya Zuma na jaji wa mahakma hiyo kudai kuwa hayana msingi na kuwa upo ushaidi unaoonyesha wazi kuwa yametawaliwa na shinikizo la kisiasa.

Hata hivyo Mbeki alikanusha tuhuma kuwa aliingilia kati kesi ya rushwa iliyokuwa inamkabili Zuma Ijumaa wiki hii na kuwashutumu watu wanaoendesha kampeni ndani ya chama chake cha ANC, wakimtaka ajiuzulu na kuwaonya watu waliokuwa wakiezungumza matusi dhidi yake.

Zuma anapwa nafasi kuba katika siasa za nchi hiyo na anatarajiwa kumrithi Mbeki, baada ya kumwangisha katika nafasi y urais wa ANC Novemba mwaka jana.

Mbeki amekuwa akishiriki katika utatuzi wa migogoro ya kisiasa katika nchi nyingi za Afrika, ikiwemo SudaN, Ivory Coast na hivi mwanzoni mwa wiki hii alikamilisha kazi ya usuluhishi wa mgogoro wa Zimbabwe baada ya kuwezesha kufikiwa muafaka wa kuwa na serikali ya pamoja baina ya Zanu-PF na chama cha upinzani cha movement for Deocratic Change (MDC).
 
Hali ya South Africa Inatisha sana. Kuna wasiwasi kuwa SA itapitia njia ile ile ya Zimbabwe pamoja na wao kubadilisha viongozi. Tatizo la Afrika ya Kusini linatokana na attitude za watu wengi kudhani kuwa Uhuru ungewafanya waishi kama makaburu bila kufanya kazi yoyote; yaani niweke kwa lugha nyingine, ni kuwa Uhuru unewafanya wachukua nafasi zilizokuwa za makaburu automatically. Ni kutokana na dhana hiyo ndiyo maana wanawachukia watu waliotoka nchi za je na kupata kazi nzuri hapo SA bila kuangalia kuwa ni kwa nini hawa wakuja wanapewa kazi huku wao a kuzaliwa wakirukwa. Tatizo hili pia lipo kwa baadhi ya ndugu zetu waamerika weusi, na wamekuwa wanachukia watu weusi hasa wale wa Jamaika, Haiti na Afrika kwa kisingizio hicho hicho kuwa wanapoingia USA huwa wanachukulia opportunities zao.
 
Hali ya South Africa Inatisha sana. Kuna wasiwasi kuwa SA itapitia njia ile ile ya Zimbabwe pamoja na wao kubadilisha viongozi. Tatizo la Afrika ya Kusini linatokana na attitude za watu wengi kudhani kuwa Uhuru ungewafanya waishi kama makaburu bila kufanya kazi yoyote; yaani niweke kwa lugha nyingine, ni kuwa Uhuru unewafanya wachukua nafasi zilizokuwa za makaburu automatically. Ni kutokana na dhana hiyo ndiyo maana wanawachukia watu waliotoka nchi za je na kupata kazi nzuri hapo SA bila kuangalia kuwa ni kwa nini hawa wakuja wanapewa kazi huku wao a kuzaliwa wakirukwa. Tatizo hili pia lipo kwa baadhi ya ndugu zetu waamerika weusi, na wamekuwa wanachukia watu weusi hasa wale wa Jamaika, Haiti na Afrika kwa kisingizio hicho hicho kuwa wanapoingia USA huwa wanachukulia opportunities zao.

acha kurahisisha mambo wewe, unaelewa na unachokisema au unaandika tuu.... hivi kwa unafikiri matatizo ya AK au huko marekani yanatokana nna hayo uliyoyandika? hivi kweli hivi ndivyo unavyoweza kuelezea jambo gumu kama hilo kwa kifupi hivyo? ni rahisi hivyo?..........
 
acha kurahisisha mambo wewe, unaelewa na unachokisema au unaandika tuu.... hivi kwa unafikiri matatizo ya AK au huko marekani yanatokana nna hayo uliyoyandika? hivi kweli hivi ndivyo unavyoweza kuelezea jambo gumu kama hilo kwa kifupi hivyo? ni rahisi hivyo?..........

Tunaomba maelezo yako wewe kuhusu hili suala, maana unaona kuwa kichuguu ameandika kiurahisi.
 
Hali ya South Africa Inatisha sana. Kuna wasiwasi kuwa SA itapitia njia ile ile ya Zimbabwe pamoja na wao kubadilisha viongozi. Tatizo la Afrika ya Kusini linatokana na attitude za watu wengi kudhani kuwa Uhuru ungewafanya waishi kama makaburu bila kufanya kazi yoyote; yaani niweke kwa lugha nyingine, ni kuwa Uhuru unewafanya wachukua nafasi zilizokuwa za makaburu automatically. Ni kutokana na dhana hiyo ndiyo maana wanawachukia watu waliotoka nchi za je na kupata kazi nzuri hapo SA bila kuangalia kuwa ni kwa nini hawa wakuja wanapewa kazi huku wao a kuzaliwa wakirukwa. Tatizo hili pia lipo kwa baadhi ya ndugu zetu waamerika weusi, na wamekuwa wanachukia watu weusi hasa wale wa Jamaika, Haiti na Afrika kwa kisingizio hicho hicho kuwa wanapoingia USA huwa wanachukulia opportunities zao.

Nadhani hapo umekiri (pengine bila hata kutambua) kuwa Miafrika Ndivyo Tulivyo!!!!!
 
acha kurahisisha mambo wewe, unaelewa na unachokisema au unaandika tuu.... hivi kwa unafikiri matatizo ya AK au huko marekani yanatokana nna hayo uliyoyandika? hivi kweli hivi ndivyo unavyoweza kuelezea jambo gumu kama hilo kwa kifupi hivyo? ni rahisi hivyo?..........

Ungesaidia sana mjadala huu kama ungetoa maelezo yako kwa nini unapinga niliyosema.

Mojawapo ya sababu za Zuma kumshinda Mbeki ni kwa sababu alipiga kampeini akiwaahidi watu kuwa akichaguliwa atahakikisha kuwa serikali inawapatia mambo mengi bure kwa maana ya kuwa tangu wapate Uhuru bado hawajayaona matunda ya Uhuru huo, jambo ambalo inawezekana kuwa ni kweli, ingawa hakuwa anasema ukweli kuhusu sababu inayowafanya wasione matunda ya Uhuru wakati watu wanotoka nchi za nje wakifika afrika ya kusini wanapata kazi nzuri na kuishi vizuri. Alichukulia kampeini yake kama ni vita ya kugombea Uhuru tena- yaani kuwang'oa makaburu na masapota wake akina Mbeki, na alikuwa akitumia kaulimbiu ya "Give me my Machine Gun."

Hili wimbi la wangeni kuuwawa huko Afrika ya Kusini ni kutokana na sababu za aina hiyo hiyo; ila kama mwenzetu wewe unajua undani wa tatizo la huko basi tuambie.

Kushindwa kwa Mbeki kwenye uchaguzi, kunatokana zaidi na msimamo wake wa kutotaka kuyumbisha misingi ya uchumi wa nchi huyo. Kwa hiyo hakuwanyang'anya wazungu mashamba wala kuwafukuza. Badala yake, serikali yake imekuwa kidogo kidogo inanunua mashamba kutoka kwa wazungu na kuyagawa kwa waafrika lakini kama ilivyotokea Zimbabwe ni wachache sana wamekuwa wanalima mashamba hayo wanapopewa bure na serikali.
 
Hivi mnajua kuwa Zuma hajui kuandika wala kusoma, ila anajua kumwaga sahihi tu. Kazi ipo pale kweli kweli
 
I'm really conflicted; ni kipi bora,

a. Kuacha Kamati ya Chama imuondoe Rais aliyependekezwa na Bunge
b. Kuacha Bunge limpigie kura ya kutokuwa na imani naye
c. KUacha amalize muda wake wa kikatiba ili mtu mwingine aweze kuingia madarakani.

Kesi mbili ni za mfano: Kesi ya Musharraf wiki chache zilizopita na kesi ya Mbeki. Katika yote mawili ni nani anaibuka mshindi?

a. Je Pakistan (ukizingatia habari za leo) is better off kuliko wakati wa Musharraf? Je mjane wa Benazir ataweza kweli kuisimamia Pakistani hivyo?

b. Je mrithi wa Mbeki (japo kwa muda mrefu) atalleta kitu gani kipya kwenye uongozi?

Nina wasiwasi kuwa bado hatujaweza kuweka suala zima la mfumo mzuri wa utawala na kuwajibishana kuwa ni msingi wa utawala bora wa nchi na maendeleo yake. On the other hand je kuwa na utaratibu wa "kuitisha uchaguzi wa mapema" ili kuziba nafasi ni mtindo mzuri wa kuwa na serikali inayofanya kazi. Mfano mzuri ni Israeli.
 
Hivi mnajua kuwa Zuma hajui kuandika wala kusoma, ila anajua kumwaga sahihi tu. Kazi ipo pale kweli kweli

Yombayomba,

Are U sure? nijuavyo Zuma hana University degree ila kutokujua kusoma wala kuandika hilo si kweli!!
 
I'm really conflicted; ni kipi bora,

a. Kuacha Kamati ya Chama imuondoe Rais aliyependekezwa na Bunge
b. Kuacha Bunge limpigie kura ya kutokuwa na imani naye
c. KUacha amalize muda wake wa kikatiba ili mtu mwingine aweze kuingia madarakani.

Kesi mbili ni za mfano: Kesi ya Musharraf wiki chache zilizopita na kesi ya Mbeki. Katika yote mawili ni nani anaibuka mshindi?

a. Je Pakistan (ukizingatia habari za leo) is better off kuliko wakati wa Musharraf? Je mjane wa Benazir ataweza kweli kuisimamia Pakistani hivyo?

b. Je mrithi wa Mbeki (japo kwa muda mrefu) atalleta kitu gani kipya kwenye uongozi?

Nina wasiwasi kuwa bado hatujaweza kuweka suala zima la mfumo mzuri wa utawala na kuwajibishana kuwa ni msingi wa utawala bora wa nchi na maendeleo yake. On the other hand je kuwa na utaratibu wa "kuitisha uchaguzi wa mapema" ili kuziba nafasi ni mtindo mzuri wa kuwa na serikali inayofanya kazi. Mfano mzuri ni Israeli.

Pamoja na hilo, pengine ni veme tukajiuliza pia katika kesi ya Zuma, tatizo la Mbeki (na lilimwondoa) ni lipi hasa?

Je, pamoja na udhaifu wake (ni upi?), Mbeki kafanya yepi mema kwa ajili ya SA?

Mpinzani wake (Zuma), ni mtuwa kaliba gani? Amefanya nini hasa kwa kipindi chake uongozini?

Mbeki ni serious thinker, ametawaliwa na sifa za usomi. Zuma ni mtu wa watu wa hali ya chini, kujichanganya kwake na wenyeji kunamfanya akubalike vema miongoni mwa laymen na watu wa chini. Lakini hizi ndo sifa za kiongozi bora? Watu wetambao hawana upeo wa kumchagua kiongozi bora, wanajuaje kiongozi bora? Je kiongozi bora ni yule anayecheka cheka tu na watu?

PLSE tuangalie haya, tuache ushabiki kwanza.
 
hilo la kutokujua kusoma na kuandika na kujua kuweka sahihi si siri, uliza wasauzi waliko kwenye ANC na serikalini wanalijua hilo
 
Mbeki ni serious thinker, ametawaliwa na sifa za usomi. Zuma ni mtu wa watu wa hali ya chini, kujichanganya kwake na wenyeji kunamfanya akubalike vema miongoni mwa laymen na watu wa chini. Lakini hizi ndo sifa za kiongozi bora? Watu wetambao hawana upeo wa kumchagua kiongozi bora, wanajuaje kiongozi bora? Je kiongozi bora ni yule anayecheka cheka tu na watu?
PLSE tuangalie haya, tuache ushabiki kwanza.

Huu ulinganisho unakaribia kidogo na ule wa Mkapa na Kikwete (technocrat vs populist). Hebu tulitafakari tena hili, hata hapa kwetu bongo linatuhusu sana.
 
hilo la kutokujua kusoma na kuandika na kujua kuweka sahihi si siri, uliza wasauzi waliko kwenye ANC na serikalini wanalijua hilo






Zuma's Education Gap May Mar South African Leadership (Update1)

By Mike Cohen


May 13 (Bloomberg) -- Jacob Zuma's education consisted of tailing his mother as she cleaned homes on South Africa's east coast, tending relatives' cattle and cadging lessons from neighbors who could afford to go to school.

Now Zuma, 66, is poised to become his country's president - - and one of the world's least-educated leaders.

During his five-decade rise through the ranks of the ruling African National Congress party, Zuma taught himself enough to become a savvy politician. ``When you speak with the man, you find he's no fool,'' said Frank Mdlalose, who cut a peace deal with him when they were in rival parties in the 1990s.

Yet his lack of formal education still shows: Testimony at an adviser's bribery trial depicted him as having no financial acumen. At a trial that acquitted him of rape, he said that, to reduce the risk of AIDS after unprotected sex, he took a shower.

At a time when South Africa faces a mounting trade deficit and power shortages hold down production from its mines and factories, there are doubts about Zuma's ability to run Africa's largest economy.

``I don't think he's perceptive or knowledgeable in the way you would hope your president would be,'' said Gavin Woods, an opposition-party lawmaker who has known Zuma since 1991. ``I don't think he has any real considered opinions on anything from health to economics to education.''

Master's Degree

In his lack of education, Zuma is far more typical of countrymen who came of age before apartheid ended than are the nation's two post-apartheid leaders. Former President Nelson Mandela, 89, is a lawyer; the incumbent, Thabo Mbeki, 65, has a master's degree in economics from the University of Sussex and quotes Shakespeare and Yeats.

Zuma, by contrast, is a product of South Africa's history and of the systematic denial of educational opportunity for South Africa's blacks. For more than three centuries after European settlers arrived in South Africa in 1652, white rulers viewed blacks only as laborers and denied them proper schooling.

Among these overlords was Cecil Rhodes, prime minister of England's Cape Colony, now the country's southwestern region. His will established Oxford University's Rhodes Scholarships with a fortune made exploiting black laborers in South Africa's diamond mines.

``Nine-tenths of them will have to spend their lives in manual labor, and the sooner that is brought home to them, the better,'' Rhodes said in 1893.

Black Reserve

That year, Rhodes established the country's first exclusively black reserve in the eastern Glen Grey district. Families were allocated eight acres (3.2 hectares) of land that they were forbidden to sell and only eldest sons could inherit, stripping their relatives of assets.

Residents were forced to pay hut taxes and all males who didn't find work outside the reserve within a year also had to pay a labor tax, a measure Rhodes said would serve as a ``stimulus to these people to make them go on working.'' He sought the closure of missionary-run schools in the area, saying they could turn blacks into anti-government agitators.

Zuma was born in 1942, six years before the whites-only National Party rose to power and began enshrining such attitudes into the apartheid system under then-Prime Minister Hendrik Verwoerd. The system mandated separate black schools.

No Mathematics

``What is the use of teaching a Bantu child mathematics when it cannot use it in practice?'' Verwoerd told parliament in 1954, using apartheid's term for black. ``Education must train and teach people in accordance with their opportunities in life.''

In those days, many black children attended no more than three hours of classes a day. Where Zuma grew up, in the rolling northeastern hills of Nkandla in KwaZulu-Natal province, schools had no running water or electricity and few books. Many teachers had barely finished school themselves.

Most families were poor and lived in circular mud-and- thatch huts. Zuma's father, a policeman, died when his son was young. His mother didn't make enough as a maid to put him in school.

``I educated myself,'' Zuma told Bloomberg Television in an interview earlier this year. ``I started by asking other kids as they came back from school with their books and slates'' to pass on what they learned.

Zuma joined the ANC in 1958, became active in its anti- apartheid guerilla campaign and was convicted of conspiring to overthrow the state in 1963. He served 10 years in prison on Robben Island, four miles off Cape Town.

Prison `University'

The prison became known as ``the university,'' because its inmates included black intellectuals willing to educate prisoners like Zuma as they toiled in its lime quarry. The teachers included Mandela and Govan Mbeki, the current president's father.

``I was not shy to ask people what I didn't understand,'' Zuma said. ``Everything I did was to learn, to learn more all the time, until I succeeded.''

``He was a very keen student, a very bright student,'' said Ebrahim Ebrahim, an ANC member who shared a cell with Zuma and later served in the parliament. ``When he arrived on the island, he couldn't read or write. He has overcome that. When he left the island, he was even reading Tolstoy.''


When Zuma was released in 1975, the education system hadn't changed much. One in 20 black children made it to high school in the 1970s as millions protested in shantytowns under the slogan ``liberation before education.''

Mandela Presidency

After prison, Zuma's political skills and prison-yard tutoring helped him rise in the ANC while in exile. By 1990, with international pressure to end apartheid increasing, the government secretly brought Zuma back to help coordinate talks with the ANC that culminated in democratic elections in 1994 and Mandela's presidency.

Zuma became economic-affairs minister for the KwaZulu-Natal province, where he helped end the Zulu nationalist Inkatha Freedom Party's violent conflict with the ANC, which claimed about 10,000 lives.

``He's very intelligent,'' said Mdlalose, then KwaZulu- Natal's governor and an IFP member who since has quit that party. ``He was a significant peace broker.''

Some fellow lawmakers, including Woods, were less impressed.

``When he answered questions in parliament, he'd always pause, and in a seemingly relaxed way, he'd laugh and quickly go on about an issue which often had nothing to do with what was being asked,'' said Woods, a member of the opposition National Democratic Convention. ``He would fiddle and fudge.''

Zuma Fired

Mbeki made Zuma deputy president after succeeding Mandela in 1999. The president fired Zuma six years later in response to allegations that his friend and financial adviser, Schabir Shaik, tried to solicit a bribe for him.

Shaik's 2005 corruption trial put Zuma's lack of financial smarts on full display. An audit showed he was broke and indebted to several banks, relying on Shaik to pay his children's school fees and other expenses.

``Zuma's financial affairs were largely managed'' by the adviser, High Court Judge Hillary Squires said in convicting Shaik and sentencing him to 15 years in prison. ``Every now and then, some sudden and unexpected expenditure by Zuma, or occasionally by his wife, would cause a temporary crisis in the management of his finances, until other arrangements could be made by Shaik.''

Zuma, who is due to stand trial himself Aug. 14 on charges of taking 783 bribes from Shaik and his companies, has denied wrongdoing and defended his adviser's payments as loans.

Rape Trial

During his April 2006 rape trial, Zuma's testimony outraged many for the ignorance it suggested, including the judge. Zuma said his 31-year-old accuser, whom he knew was HIV positive, wanted to have sex with him.

``In the Zulu culture, you don't leave a woman'' who is aroused, Zuma testified. ``If you do, then she will even have you arrested and say that you are a rapist.'' Zuma, the former head of South Africa's AIDS program, said he didn't use a condom because he didn't have one handy and took a shower to ``minimize the risk of contracting the disease.''

``It is totally inexcusable that a man should have unprotected sex with any person other than his regular partner, and definitely not with a person who is to his knowledge is HIV- positive,'' High Court Judge Willem van der Merwe said in his acquittal ruling. ``I do not even want to comment on the effect of a shower after having unprotected sex.''

Zuma `Erred'

The next day, Zuma said he ``erred'' and apologized: ``I should have known better, and I should have acted with greater caution and responsibility.''

The trials had little impact on Zuma's ascension in the ANC. In December, the party elected him over Mbeki as its leader, making him the frontrunner to be selected as president by the National Assembly after next year's parliamentary elections.

Since then, Zuma has struggled to convey consistent messages. After winning the divisive party race, he tried to be conciliatory, calling Mbeki a ``comrade, friend and brother.'' Then, egged on by cheering supporters, he performed his signature tune: ``Bring me my machine gun,'' he sang in Zulu.

He has said the government may make it easier for employers to fire staff and then pledged not to erode worker rights. He advocated public debate on reintroducing the death penalty and then said he opposed capital punishment. He promised to protect the criminal justice system's integrity as the ANC set about disbanding the agency investigating him, known as the Scorpions.

`Flawed Character'

Zuma ``does not encourage confidence in his understanding of policy, appearing as he does in the short term to be making policy pronouncements on-the-hoof depending on who he wishes to appease,'' Barney Pityana, vice chancellor of the University of South Africa in Pretoria, said in a March 31 address to the Law Society of South Africa. ``He remains a flawed character.''

The legacy of educational neglect that produced Zuma has endured in the post-apartheid era, even as the government allocates more than a fifth of its budget to schools, colleges and universities, one of the world's highest proportions.

While schooling is mandatory from age 7 to 15, almost half of the nation's children don't finish high school, according to South Africa's education department. A third of the 564,775 pupils who took final-year examinations last year failed. Almost 5 million adults are illiterate. There aren't enough teachers: In 2006, 6,000 joined the profession and over 20,000 left it. Colleges are filled to capacity.

`Huge' Education Problem

``The nature of the problem is so huge and is so complex,'' says Anil Kanjee, an education analyst at the Human Sciences Research Council in Pretoria. ``You are looking at something that will take a generation at least to see any significant change.''

The Mnyakanya Secondary School, near Zuma's homestead in Nkandla, illustrates the challenge.

Zuma and Mandela coaxed phone company Telkom South Africa Ltd. into sponsoring a school laboratory and mining company Gold Fields Ltd. into building 12 classrooms, a library and an auditorium -- facilities that are the pride of the district. An educational trust Zuma set up helps support about 60 percent of the school's 685 pupils.

All that has delivered only limited benefits. Many of the Mnyakanya's pupils walk for up to two hours to and from classes and live in a society blighted by unemployment, poverty and AIDS. Of the 111 pupils who took final-year examinations last year, 50 passed. The school is short-staffed.

Lack of Rural Teachers

``Some of the educators don't want to live in the rural areas,'' said William Vilakazi, 38, the deputy principal. ``They would have to reside in places that don't have electricity. At the moment, we have six posts vacant.''

Zuma has promised to make education a priority. He plans to increase teachers' pay; scrap fees at 60 percent of government schools by 2009, up from 40 percent now; and employ 80,000 tutors to teach illiterate adults.

``A nation with less education will remain with problems forever,'' Zuma said. ``We need to do radical programs to ensure our population is educated. I believe it's a wise and strategic investment.''

He added that ``I have experience of how it looks like if you don't have education.''

To contact the reporter on this story: Mike Cohen in Cape Town at mcohen21
 
hilo la kutokujua kusoma na kuandika na kujua kuweka sahihi si siri, uliza wasauzi waliko kwenye ANC na serikalini wanalijua hilo

Kaka Yombayomba maneno yako si ya kweli!..Jacob Zuma au Msholozi kama anavyojulikana kwao Natal Kwa Zulu ni mpiganaji ambaye hana Elimu kubwa,Lakini ukweli wa mambo ni kwamba anajua kusoma na kuandika.Kuhusu formal Education huyu Muungwana aliishia darasa la TATU.Lakini ANC ilimpa nafasi ya kujiendeleza,na hivi leo ni mtu ambaye anajua kusoma na kuandika.Lakini bado Elimu yake ni suala kubwa katika Uongozi Mkubwa kama Rais wa Nchi.

Namfahamu Mzee Zuma Personal,na kwa wale wenye kumbukumbu Nzuri,Zuma alikuwa ni mmoja kati ya watu waliokuwa karibu na Mzee Mwakalindile na Maftah kwenye Ubalozi wetu Mozambique.Zuma ni mmoja wa Viongozi walioshiriki kwenye Mkataba wa NKOMATI huko Maputo,ambako alilazimika kuondoka Maputo 1984 na kuhamia Lusaka na baada ya Mwaka mmoja tu 1985 alikuwa Chief Intelligent Officer katika ofisi za ANC - Lusaka na kipindi hicho alikuwa anafanya kazi na Thabo Mbeki.

Kutokana na mazoea yake kwa Watanzania,Zuma pia alikuwa mara kwa mara anakuwa Ubalozini kwetu Lusaka kama ilivyokuwa Maputo..Hapo alijenga Urafiki wa karibu na Maofisa Ubalozi Ami Mpungwe na Capt Abuu Ibrahim.Kumbuka wakati Mandela anapewa Nchi pia Zuma alikuwa mmoja kati ya Manaibu Rais 5.Kutokana na kazi alizofanya mpaka kusaini Nkomati Accord huwezi kuniambia kuwa Zuma hajui kusoma.
 
Niliwahi kusema na leo najiuliza,

1-Je, tunaunganisha vipi na mambo yanayoendelea hapa nyumbani?
2-Je, yanayotokea Afrika Kusini yana uhusiano wowote na ziara ya Zuma Tanzania hivi karibuni?
3-Je, Tanzania tunaye Zuma wetu atakayemuondoa JK madarakani?

Maswali hayo yanatokana na tetesi nilizozigusia wakati katika ile mada ya Kubenea v/s Lowassa

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/17756-kubenea-vs-lowasa-12.html#post284754
 
Niliwahi kusema na leo najiuliza,

1-Je, tunaunganisha vipi na mambo yanayoendelea hapa nyumbani?
2-Je, yanayotokea Afrika Kusini yana uhusiano wowote na ziara ya Zuma Tanzania hivi karibuni?
3-Je, Tanzania tunaye Zuma wetu atakayemuondoa JK madarakani?

Maswali hayo yanatokana na tetesi nilizozigusia wakati katika ile mada ya Kubenea v/s Lowassa

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/17756-kubenea-vs-lowasa-12.html#post284754

Baada ya kusoma tena kwa undani habari za huyu Mzee Zuma naona tunafundishwa aina mbili kubwa za wapiganaji: Wapiganaji wa kitabuni (ama ofisini, wao hukaa kurudia nadharia walizosoma na kunukuu maandishi ya wanafalsafa wahutubiapo, aghalabu hayana mvuto sana kwa wananchi wa "kawaida"), na wapiganaji wa "uwanjani" (au wa kwenye field) ambao wanashiriki bega kwa bega na wapambanaji wa mstari wa mbele. Ni wachache sana wenye uwezo wa kuingia nyanja zote mbili, ya kitabu na ya uwanjani kama Mzee Mandela, ambaye kwa Afrika hana mshindani. Huyu mzee Zuma inaonekana alipatia umaarufu katika uwanja wa mapambano, na hata awe na kasoro gani, ni vigumu sana kumfuta kwenye nyoyo za wananchi wa kawaida, maadamu walichokuwa wanakipigania bado kinahitaji mtu wa kukisimamia na kukamilisha lile lengo lao la mapambano. Hawa "wasomi" kina Mbeki na wenzie watakubalika miongoni mwa wazungu na wale wachache walioona kurasa za vitabu, ambao takwimu za "kukua kwa uchumi" wanazielewa, lakini si kwa wapiga kura walio wengi, ndio maana ukishindanisha Mbeki na Zuma wapiga kura hawapepesi macho, ni Zuma tu! Kwa maslahi ya nchi yao, ingewafaa wananchi hao kutafuta namna ya kuhakikisha kuwa wapiganaji wa aina zote mbili wanakuwapo ndani ya serikali kwa kuwa wanategemeana. Kuna hatari sana ya kuwa na kiongozi anayepelekwa tu na upepo wa kelele za kushangiliwa na wananchi, anaweza kujikuta anaendesha nchi kiholela na kuipeleka pabaya. Vivyohivyo ni hatari sana kuwa na kiongozi anayeangalia nadharia za vitabuni tu na kupuuza sauti za wananchi, anaweza kujikuta wananchi wanashindwa kujizuia wanafanya fujo (kama zile za xenophobia tulizosikia), na hata migogoro dhidi ya tabaka tawala, mapinduzi na umwagaji damu. Viongozi wa aina ya Zuma si wa kupuuzwa na kuitwa majina mabaya kama hayo ya "illiterate" nk, badala yake ni wa kutumiwa optimally, wanao mchango mkubwa kwa taifa kama energy waliyo nayo itachotwa na kutumiwa ipasavyo.
 
Back
Top Bottom