Mbatia: Hatujasusia bunge, tuna hasira na mtu ambaye hata jina lake siwezi kulitaja

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968

Mbunge wa Vunjo James Mbatia amesema wao hawajasusia bunge ila wana hasira na mtu ambaye hata jina lake hawezi kulitaja, na huwa wanaingia akiwepo mwenyekiti mwingine wa bunge na wanashiriki kwenye kamati.

Pia amesema wazanzibar walishapiga kura wakitaka waongozwe na serikali ya umoja wa kitaifa na wanaolaumu chama cha wananchi CUF kwa kinachoendelea Zanzibar hawafikirii vizuri
 
Kwahiyo chuki zake binafsi zipo juu ya haki za wananchi kupata uwakilishi? .... No nimesahau hata hao wananchi wanaoweza kumchagua awe mwakilishi wao nao hawaitaki hiyo haki so endeleeni tu na maigizo. Pongezi leo zimuendee mbunifu wa vazi jeusi.
 
Kwa hiyo ukimchukia mkeo unachukia na watoto? Wananchi wamekutuma bungeni uwawakilishe, wewe hasira zako kwa naibu spika unatuletea sisi,? Kweli Dr slaa alikuwa kichwa
huyu jamaa anamatatizo ya kisaikolojia, kwanza alianza kumsumbua halima mdee kwa kumfungulia kesi zisizokuwa na kichwa wala miguu hadi JK akaingilia kati ka kumpatia ubunge wa viti maalum, sasa kaanza kumshambulia Dr.Tulia bila sababu yeyote, ila nakumbuka lyatonga alishawahi kusema huyu jamaa kichwani haziko sawa na anahitaji kupimwa. Yeye muda wote ni hasira tu na wanawake hata mifano yake utasikia akisema "tanzania mama yetu"
 
Hahahahah daa et jamaa ana hasira na kina mama .unamanisha nn labda
 
Ni muda mrefu sisi wazalendo tumekuwa tukijua kilichopo nyuma ya pazia kwa matendo na mbwembwe zinazofanywa na wanaojiita wapinzani.

Ukweli ni kwamba, vituko vyote vya wapinzani ni baada ya kugundua kuwa Kagame alikuwa anawatumia kama toilet paper wakati wa JK na sasa hana time nao.

Na kibaya zaidi ni kule kujua kuwa siri zote walizokuwa wakimpa Kagame dhidi ya serikali ya JK ambazo kisheria ni vitendo vya kigaidi, zimefichuka na zimekabidhiwa kwa JPM.

Kwa hiyo wanajua bila ya shaka kuwa it is just a matter of time they shall start to pay the price for their betraya.

Kwa hiyo wanachokifanya kwa sasa ni kutafuta sympath ya umma ili wakianza kushughulikiwa, wathibitishe kuwa JPM ni dikteta.
 
huyu jamaa anamatatizo ya kisaikolojia, kwanza alianza kumsumbua halima mdee kwa kumfungulia kesi zisizokuwa na kichwa wala miguu hadi JK akaingilia kati ka kumpatia ubunge wa viti maalum, sasa kaanza kumshambulia Dr.Tulia bila sababu yeyote, ila nakumbuka lyatonga alishawahi kusema huyu jamaa kichwani haziko sawa na anahitaji kupimwa. Yeye muda wote ni hasira tu na wanawake hata mifano yake utasikia akisema "tanzania mama yetu"
Aisee nimecheka sana, binadamu mnajua kufikiri.
 
Mbunge wa Vunjo James Mbatia amesema wao hawajasusia bunge ila wana hasira na mtu ambaye hata jina lake hawezi kulitaja, na huwa wanaingia akiwepo mwenyekiti mwingine wa bunge na wanashiriki kwenye kamati.
Pia amesema wazanzibar walishapiga kura wakitaka waongozwe na serikali ya umoja wa kitaifa na wanaolaumu chama cha wananchi CUF kwa kinachoendelea Zanzibar hawafikirii vizuri

Unapandisha nyongo bure.wivu umekutawala
 
huyu jamaa anamatatizo ya kisaikolojia, kwanza alianza kumsumbua halima mdee kwa kumfungulia kesi zisizokuwa na kichwa wala miguu hadi JK akaingilia kati ka kumpatia ubunge wa viti maalum, sasa kaanza kumshambulia Dr.Tulia bila sababu yeyote, ila nakumbuka lyatonga alishawahi kusema huyu jamaa kichwani haziko sawa na anahitaji kupimwa. Yeye muda wote ni hasira tu na wanawake hata mifano yake utasikia akisema "tanzania mama yetu"
Hahahaha. Mkuu unaweza kufafanua kidogo unaposema ana hasira na wanawake.
 
Sasa mtu mmoja ndio anaewaendesha mpaka waache majukumu yao ya msingi mara wazibe midomo mara manguo meusi mara wazire bunge. Huyo mtu kweli mmoja anawasababishia kuwa na hasira kiasi hiki.
Kweli siasa zetu ni za ajabu sana hizi.
 
Nadhani watu hamsomi hata historia za nchi nhinginezo ndo maana uwezo wenu wa kufikiri umeishia apo. Historia syo lazma uende secondary au chuo, soma vitabu, magazeti sikiliza radio TV na Internet muone amani kwa nchi zingine ilivobaki historia wajomba.

Sent from my TECNO 7C using JamiiForums mobile app
 
Leo mnamchukia NS lakin baadaye mtamuelewa tu tena awe na msimamo hivyohivyo asichezewe na mtu yoyote ili mladi tu asivunje sheria.
 
Back
Top Bottom