Mbatia ataka majina ya waliofisadi mabilioni ya Benki kuu yawekwe hadharani, asema wale waliosimamishwa Hazina ni dagaa tu

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia ameitaka serikali kutaja hadharani majina ya waliofisadi mabilioni ya fedha za benki kuu yaliyotajwa katika ripoti ya CAG.

Mbatia amesema kuwasimamisha maofisa wachache wa wizara ya fedha waliogawana fedha hizo kama posho haitoshi, wale ni dagaa tu tunataka papa watajwe hadharani.

Source: ITV habari!
Mbatia wewe si "mwenzetu" ? tusipangiane majukumu, hata wale waliochukua hela za Escrow Stanbic kwenye sandarusi waliwahi kutangazwa ? Muache mama aendelee kuijenga mama Tanzania !🤸🤣🐒
 
Si awataje tu kwani anaogopa nini? Mama hana mambo ya kutekateka watu, Kama anawajua awataje na mzigo waliochukua.
 
Back
Top Bottom