Mbatia 'aipa' CCM ushindi kuongoza Halmashauri ya Uvinza

Mbatia 'aipa' CCM ushindi kuongoza Halmashauri ya Uvinza

Usitufanye sisi ni wajinga na hatuna Kumbukumbu. Hebu soma Taarifa hii hapa chini halafu ujipime ujinga wako

Feb 17, 2011

Nini hiki Upinzani ndani ya Upinzani!

Freeman Mbowe, Mkuu wa Kambi ya Upinzani (Chadema)

Hamad Rashid, aliyekuwa Mkuu wa Kambi ya Upinzani (CUF)

David Kafulila, Mbunge (NCCR Mageuzi)

BISHOP J. HILUKA

Dar es salaam

KUNA kila dalili kwamba vyama vya upinzani ndani ya bunge vimemeguka baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuchukua nafasi zote za juu za uongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni bila kuvihusisha vyama vingine.

Vyama hivyo vya upinzani vimeunda kambi mbili za upinzani katika Bunge la Jamhuri la Muungano baada Chadema kuunda kambi yake ikijitegemea kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wabunge huku Chama cha Wananchi (CUF) kikiungana na NCCR-Mageuzi, TLP na UDP kuunda kambi nyingine.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mambo ya Bunge wa chadema, John Mrema, nafasi ya Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe na makamu wake ni Naibu Katibu Mkuu wa chadema na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe. Nafasi ya Mnadhimu wa Kambi hiyo ni Mbunge wa Singida Kusini, Tundu Lissu.

Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, chama kinachofikisha asilimia 12 ya wabunge kina uwezo wa kuunda kambi ya upinzani bungeni. Chadema kimezidi asilimia hizo baada ya kupata wabunge 23 wa kuchaguliwa kwenye majimbo na 23 wa viti maalum. Hata hivyo, imezuka minong’ono kwa baadhi ya vyama vya upinzani vikidai kuwa Chadema kimehodhi kambi yote ya upinzani na kuviacha solemba vyama hivyo.

Awali ilielezwa kuwa CUF kilichokuwa kikishikilia uongozi wa kambi hiyo katika Bunge lililopita kingekiunga mkono Chadema katika kambi ya upinzani na katika nafasi ya mgombea wa nafasi ya Spika ambayo tayari inashikiliwa na Anne Makinda wa CCM.

Badala yake CUF waliamua kukaa kimya, ukimya wao ulitafsiriwa kuwa ulilenga kuiunga mkono CCM badala ya Chadema na ndivyo ilivyojidhihirisha baada Makinda kuzoa kura 265 huku mpinzani wake kutoka Chadema akiambulia kura 53 tu, wakati wabunge wa upinzani wapo kama 86 hivi.

Pamoja na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid kukanusha madai hayo lakini imezidi kujidhihirisha hata wakati wa kugombea nafasi ya Unaibu spika, ambapo Job Ndugai wa CCM alipata kura 276 kati ya 328 zilizopigwa (asilimia 84,2) na kumwacha Mustafa Akunay wa Chadema akiambulia kura 46 tu (idadi ya wabunge wa Chadema), sawa na asilimia 14, huku kura sita zikiharibika.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini ambaye pia ni naibu kiongozi wa upinzani bungeni, Zitto Kabwe alisema kuwa hoja ya kuhodhi kambi ya upinzani na kuifanya kuwa ya Chadema badala ya upinzani wote, siyo jambo la ajabu kwani ni utaratibu unaofanywa hata na nchi nyingine, chama chenye wabunge wengi ndicho kinachotoa waziri mkuu kwa hiyo hata Chadema kwa kuwa kina wabunge wengi kuliko vyama vingine vya upinzani kina haki ya kuunda kambi ya upinzani.

Inanitatiza kidogo, iweje suala la kambi ya upinzani bungeni kuhodhiwa na Chadema liwe 'issue' ya kuwafanya wapinzani wasishirikiane? Au kuna ajenda nyingine zaidi ya hiyo? Mbunge wa Wawi, Ahamed Rashid anaposema kuwa wameamua kuunda kambi yao kwa kushirikiana na NCCR-Mageuzi baada ya Chadema kushindwa kutimiza sharti la kushirikisha vyama vingine kwenye kambi ya upinzani ni jambo la kushangaza kwa kuwa hata wao hawakuvishirikisha vyama vya NCCR-Mageuzi na Chadema walipounda kambi ya upinzani bungeni mwaka 1995.

Inaposemwa kuwa uwepo wa Serikali kivuli ya Chadema bila ushirikiano na CUF ni kitu kibaya, wanasahau kuwa ni CUF hiyo hiyo iliyowahi kuvizunguka NCCR-Mageuzi na Chadema kikaungana na UDP na kuunda Serikali kivuli. Hatukusikia malalamiko kutoka Chadema wala NCCR-Mageuzi. Mimi nadhani kuna viongozi ambao wanataka kuhubiri na kuendeleza tofauti ambazo zinapaswa kupigwa vita, na kinachojitokeza sasa ni Upinzani ndani ya Upinzani!

Mbunge wa Vunjo ambaye pia ni mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema alisema haoni kama kuna tatizo kwa kambi yote ya upinzani kwenda Chadema, na kusisitiza kuwa Chadema wana vijana wengi wazuri ambao wataleta changamoto kubwa Bungeni. Pia sheria za Bunge zinawaruhusu, hivyo hakuna sababu ya kuwalalamikia kwani huwezi kumlazimisha mtu akupende.

kinyang’anyiro cha uspika kilichompa ushindi wa kishindo Anne Makinda wa CCM, kimeonesha kuwepo kwa dalili ya kutokujitosheleza kwa kambi nzima ya upinzani. Wapinzani wanahitaji kuungana ili kuwa na nguvu zaidi kama kweli wana nia ya kuleta changamoto kwa serikali.

Kwa hali hii inanifanya nidhani kuwa pengine baadhi ya wapinzani hawajajitambua na hawajui wanataka nini au wapo kwa makusudi fulani. Ukiangalia hata kwenye majimbo mengi kufuatia uchaguzi wa wabunge utagundua kuwa wapinzani wangeweza kupata wabunge wengi zaidi, pengine ni zaidi ya wabunge 100! Mfano katika mkoa wa Dar e Salaam ambapo wapinzani wameshinda majimbo mawili tu; Kawe na Ubungo, lakini kwa mujibu wa matokeo halisi ni kwamba wameshinda pia majimbo ya Segerea, Kinondoni na Temeke ambako kura za ubunge zilikuwa nyingi kwa wapinzani kuliko kwa CCM.

Hii inadhihirishwa na matokeo kutoka majimbo mbalimbali ambapo wapinzani waliongoza lakini ni CCM iliyoibuka kidedea.

Ni wakati sasa wa watu wanaojiita wapinzani kuamua kuwa wapinzani au kujiunga na CCM.

Sasa we kilaza huoni kuwa hii taarifa yako imekukaanga?!!! COUGH NA NCCR waliwapigia CCM kura kwenye uspika na unaibu (hapo ni kabla mawaziri vivuli wa kambi ya upinzani hawajachaguliwa)... Hamad Rashid alisema COUGH hawawezi kujiunga na kambi ya CDM hadi CDM watakakubali kushirikisha vyama vingine. CDM wasingeweza kushirikisha vyama vingine kwa sababu NCCR walikataa kutokana na Mbatia kugoma kutokana na ugomvi wake na Mdee ulioibuka kwenye kampeni, akidai Mdee alisema yeye Mbatia ni shoga. Mbatia alikimbillia mahakamani na akakataa suluhu hadi alipokuja kukubali kufuta kesi mwaka juzi...
 
Mods please tunaomba mchunguze ukweli wa thuma hizi kama kweli kulikuwa na hayo makubaliano na kama kweli yamevunjwa
Na kana kwamba haitoshi ithibitishwe pia kwamba ni Mwenyekiti Mbatia ndio katoa amri makubaliano hayo yavunjwe

Vinginevyo mleta mada @Malemo achukuliwe hatua za kinadhamu kwa kuleta habari za kizushi na kichochezi kama alivyo adhibiwa Mwampambwa

Matokeo ya Arusha yanakufanya utokwe povu mpaka unatia huruma.
 
kama NCCR ilikubali kuipa chadema ushirikiano kwenye vikao kisha ikawageuka basi haifai kuthaminiwa na wananchi ila kama chadema iling'ang'ania uenyekiti tu bila kuisikiliza NCCR kwakuwa ina madiwani wengi huu ni uroho wa wazi wa madaraka na kama ndo chadema ilivyo ctaona tofauti kati yake na Nyinyiemu.
Kambi rasmi ya upinzani bungeni chadema ilishirikisha chama gani??
 
Kitendo cha Mkiti wa NCCR James Mbatia kukataa makubaliano yaliyokuwa yamefikiwa kati ya NCCR na CHADEMA kuongoza halmashauri ya Uvinza yamesababisha CCM kutumia mwanya huo na kutwaa nafasi ya Makamu Mkiti wa Halmashauri hiyo.

Kwa upande wa nafasi ya Mkiti uchaguzi umeahirishwa hadi utakapotangazwa tena baada ya vyama vyote vitatu kushindwa kupata theluthi mbili ya kura.

Katika nafasi ya Mkiti vyama vyote vitatu viliweka wagombea ambapo CCM ilipata kura 8 CHADEMA kura 7 na NCCR kura 6.

Nafasi ya Makamu Mkiti mgombea wa CCM hakuwa na mpinzani na alipita bila kupingwa.

Katika makubaliano ya awali ngazi ya wilaya na mkoa vyama vya NCCR na Chadema vilikubaliana kuachiana nafasi ambapo ilukubaliwa CHADEMA igombee nafasi ya Mkiti na NCCR Makamu Mkiti.

Katika hali ya kushangaza siku ya kurudisha fomu vyama vyote viwili vilirudisha fomu nafasi ya Mkiti na NCCR ikakataa kugombea nafasi ya Makamu Mkiti hivyo mgombea wa CCM akapita bila kupingwa.

Inadaiwa Mkiti wa NCCR James Mbatia ndiye aliingilia kati kuvunja makubaliano ya vyama hivyo na hatimaye ushindi ukawa upande wa CCM

Pole sana Molemo. Ninasikitika kuwa hadi leo hujafahamu kuwa Mbatia ni CCM!!!! Hivi hujashangaa mbio zake za Kawe? Alitumika sana 2010!! Na kwa shukrani alipewa ubunge wa viti maalum na Rais mwenyewe ambaye ndiye mwenyekiti wa CCM. Kwa mantiki hii hutategemea hata siku moja NCCR Mageuzi iungane na upinzani wa kweli. Kwa kifupi NCCR Mageuzi=UDP=CUF=CMM na vingine vingi tu. Kumbuka kuwa Chama cha upinzani cha makamanda na wazalendo wa kweli ni CDM pekee na nidyo maana kinawindwa hata kwa mabomu!!! Wengi wa CDM hawahongeki na wale wanaohongeka wanaondoka kwa aibu. Ni mpaka kieleweke.
 
NCCR nawapongeza kwa msimamo wao, walimlaghai mbatia akafuta kesi ya kawe kwa makubaliano mtaunda kambi ya upinzani ya pamoja na NCCR chadema mkawageuka Leo mnataka tena mpewe Meya kwa mgongo wa NCCR, bora kila mtu afe kivyake, hawa Chadema siku zote huwa wanaangalia Maslahi ya kisiasa kwa upande wao NCCR wameng'amua Hilo, CUF waliisha ng'amua siku nyingi.
 
Nampongeza mh mbatia kwa kulipa fadhira ya kupewa ubunge vitu maalum na hivyo kuepushwa kufa kwa njaa. Kwa hatua hiyo mbatia inajimaliza na kumaliza chama chake. Hongera mbatia kwa kuwaonyesha watanzania ya kuwa, CHADEMA ni wapinzani pekee.
kumbe mbatia ni viti
maalum!! mpe ongera.
 
Mbatia analipa fadhila kwa Mwenyekiti wa CCM-Taifa kwani suala la kuteuliwa kuwa Mbunge si dogo kwake.Hapo ndipo ninapokubaliana na Kafulila kwamba Mwanaume aliyeshindwa na Mwanamke katika nafasi ya Ubunge hawezi kukiongoza chama ipasavyo!

hata mimi naunga mkono hoja, pili [kafulila][machali] [mkosamali] tunawakaribisha cdm mwachieni mbatia chama chake ccm [c]
 
sasa munalalamika nyinyi,si muliona kujitenga katika bunge ndio dili oneni sasa "vita vya panzi neema kwa kunguru"Chadema roho mbaya zetu ndio zinazowauwa na mutaendelea kulia kila siku mpaka mutakapo amua kushirikiana na wenzenu
Kitendo cha Mkiti wa NCCR James Mbatia kukataa makubaliano yaliyokuwa yamefikiwa kati ya NCCR na CHADEMA kuongoza halmashauri ya Uvinza yamesababisha CCM kutumia mwanya huo na kutwaa nafasi ya Makamu Mkiti wa Halmashauri hiyo.

Kwa upande wa nafasi ya Mkiti uchaguzi umeahirishwa hadi utakapotangazwa tena baada ya vyama vyote vitatu kushindwa kupata theluthi mbili ya kura.

Katika nafasi ya Mkiti vyama vyote vitatu viliweka wagombea ambapo CCM ilipata kura 8 CHADEMA kura 7 na NCCR kura 6.

Nafasi ya Makamu Mkiti mgombea wa CCM hakuwa na mpinzani na alipita bila kupingwa.

Katika makubaliano ya awali ngazi ya wilaya na mkoa vyama vya NCCR na Chadema vilikubaliana kuachiana nafasi ambapo ilukubaliwa CHADEMA igombee nafasi ya Mkiti na NCCR Makamu Mkiti.

Katika hali ya kushangaza siku ya kurudisha fomu vyama vyote viwili vilirudisha fomu nafasi ya Mkiti na NCCR ikakataa kugombea nafasi ya Makamu Mkiti hivyo mgombea wa CCM akapita bila kupingwa.

Inadaiwa Mkiti wa NCCR James Mbatia ndiye aliingilia kati kuvunja makubaliano ya vyama hivyo na hatimaye ushindi ukawa upande wa CCM
 
Safi sana NCCR-M, hawa CHADEMA wamesha sema kuwa Tanzania nzima wao tu ndio wapinzani, ila vyama vingine vyote ni CCM-B. Sasa iweje leo wajikombe kombe kwa vyama vingine?

"Sijawahi kuona chama chenye pepo mtaka vyeo kama CHADEMA." By Mwigulu Nchemba.
 
NCCR-Mageuzi ni chama cha kisiasa kilichoundwa na CCM ikiwa ni kuwaridhisha donors kuwa wameridhia matakwa yao, kwa kuwa licha ya kuundwa tume na rais Mwinyi chini ya uangalizi wa Nyerere (RIP), ililazimika kuunda vyama vya kuzugia ikiwemo NCCR.

Huu ni uongo mkubwa sana. Kumbuka hata waliounda Chadema ni zao la NCCR. Acheni kupotosha jamii na kupakazia vyama vingine kwa maslahi ya chama chenu.
 
NCCR nawapongeza kwa msimamo wao, walimlaghai mbatia akafuta kesi ya kawe kwa makubaliano mtaunda kambi ya upinzani ya pamoja na NCCR chadema mkawageuka Leo mnataka tena mpewe Meya kwa mgongo wa NCCR, bora kila mtu afe kivyake, hawa Chadema siku zote huwa wanaangalia Maslahi ya kisiasa kwa upande wao NCCR wameng'amua Hilo, CUF waliisha ng'amua siku nyingi.
Uko sahihi, makubaliano ya kufutwa kwa kesi ya Kawe ilikuwa ni pamoja na chadema kuacha kuitukana NCCR na viongozi wake, lakini hawa jamaa waliendelea tu.
 
Tusiwe wepesi wa kusahau! Haya makubaliano tuliyakataa tangu tulipoona tunakuwa na kura za kutosha kuongoza upinzani bungeni. Wenzetu walilalama sisi tukaweka pamba masikioni sasa tunapiga mayowe ya nini? Hebu turuhusu vichwa vyetu vifanye kazi. Katika hili niko pamoja na Mbatia maana kama tunaamini kuwa ushirikiano ni muhimu acha hili liwe fundisho!! Namwomba Punda aahirishe kabisa uchaguzi wa M/kiti wa hiyo halmashauri! Nyam...baff!
 
Hilo limepita, chadema chapa mwendo msimwamini mtu, vyama vingine ni mamluki tu. jipangeni kwa uchaguz serikali za mitaa
 
Kitendo cha Mkiti wa NCCR James Mbatia kukataa makubaliano yaliyokuwa yamefikiwa kati ya NCCR na CHADEMA kuongoza halmashauri ya Uvinza yamesababisha CCM kutumia mwanya huo na kutwaa nafasi ya Makamu Mkiti wa Halmashauri hiyo.

Kwa upande wa nafasi ya Mkiti uchaguzi umeahirishwa hadi utakapotangazwa tena baada ya vyama vyote vitatu kushindwa kupata theluthi mbili ya kura.

Katika nafasi ya Mkiti vyama vyote vitatu viliweka wagombea ambapo CCM ilipata kura 8 CHADEMA kura 7 na NCCR kura 6.

Nafasi ya Makamu Mkiti mgombea wa CCM hakuwa na mpinzani na alipita bila kupingwa.

Katika makubaliano ya awali ngazi ya wilaya na mkoa vyama vya NCCR na Chadema vilikubaliana kuachiana nafasi ambapo ilukubaliwa CHADEMA igombee nafasi ya Mkiti na NCCR Makamu Mkiti.

Katika hali ya kushangaza siku ya kurudisha fomu vyama vyote viwili vilirudisha fomu nafasi ya Mkiti na NCCR ikakataa kugombea nafasi ya Makamu Mkiti hivyo mgombea wa CCM akapita bila kupingwa.

Inadaiwa Mkiti wa NCCR James Mbatia ndiye aliingilia kati kuvunja makubaliano ya vyama hivyo na hatimaye ushindi ukawa upande wa CCM

Huu uongo wako na wenyewe unachangia kutoelewana kwa vyama. Kwanza hadi sasa hakuna mshindi na uchaguzi umeairishwa. Badala ya kurusha shutuma za kijinga ungetoa nafasi vyama hivi vikajadiliana na kufikia makubalianao kabla ya uchaguzi kurudiwa.
Pili, kwa mujibu wa mtu aliyemnukuu Mhe. Kafulila, mazungumzo yalikuwa yakiendelea kati ya makatibu wakuu wa vyama; Sam Ruhuza (NCCR) na Wilbroad Slaa (CHADEMA). Wewe ukaamua kuweka ukweli huo kando ili umpake matope Mbatia. Dhambi yenu hii ndiyo inayoharibu maelewano.
 
Back
Top Bottom