Mbatia 'aipa' CCM ushindi kuongoza Halmashauri ya Uvinza

Mbatia 'aipa' CCM ushindi kuongoza Halmashauri ya Uvinza

Chadema inatengenezaje makubaliano na Sisimizi?, Chadema kila siku inajikweza kuwa ndio chama pekee cha Upinzan TANZANIA, Sasa leo inawekaje Makubaliano na "mapindikizi" ya CCM, au kwenye uwewzekano wa kunyakuwa madaraka huwa wanasahau Milopoko yao,Bora hiyo Halmashauri iongozwe na M23 au Intarahamwe wanaoua maadui zao kuliko hawa wanaolipua wanachama wao ili kupata Sympath ya kisiasa!
 
Na ni nani aliwaambia CDM wafanye makubaliano na NCCR?!!!
Tulishaamua kuwa nakuna tena mkataba na shetani... na hata mke wa Loti alipogeuka nyuma akawa chumvi, Loti hakuangaika kuizoa ile chumvi, eti kwa sababu "ilikuwa mke wake"... Vyama vyote vya siasa Tanzania vipo pamoja na vimeshikamana katika kuwadhulumu wananchi wa hii nchi, isipokuwa CDM peke yake.

Hivi CDM walisahahu NCCR walipoungana na CUF na CCM kubadilisha vifungu vya kanuni za bunge?!!!

Tusirudie tena hilo kosa....

Sizitaki Mbichi Hizo! sasa wewe unaongea kama nani? wenye chama wameona umuhimu wa kuungana. wewe sijui unafikiria nini. eti CDM ndo chama pekee hakidhulumu wananchi, hayo mamilioni ya ruzuku wanayojikopesha viongozi wako siyo kudhulumu wananchi? hizo siyo pesa za walipa kodi?
 
Na ni nani aliwaambia CDM wafanye makubaliano na NCCR?!!!
Tulishaamua kuwa nakuna tena mkataba na shetani... na hata mke wa Loti alipogeuka nyuma akawa chumvi, Loti hakuangaika kuizoa ile chumvi, eti kwa sababu "ilikuwa mke wake"... Vyama vyote vya siasa Tanzania vipo pamoja na vimeshikamana katika kuwadhulumu wananchi wa hii nchi, isipokuwa CDM peke yake.

Hivi CDM walisahahu NCCR walipoungana na CUF na CCM kubadilisha vifungu vya kanuni za bunge?!!!

Tusirudie tena hilo kosa....

Maneno mazito sana haya mkuu Tuko...
 
Last edited by a moderator:
unatehemea nini kama kazi ya chdm ni kuwatukana mbatia na lipumba. nimewahi sema kuwa kwa mtindo huu chdm haitofika popote. juzi star tv lissu alivishambulia sana cuf na nccr. kama chdm hawatumii mbinu ya kuvisogeza karibu cuf na nccr, unategemea nini kitatokea? mbatia yuko sahihi kufanya vile. nashauri mmgombea wa nccr ajitoe kwenye uenyekiti ili kura zote za nccr zipelekwe ccm. pipooooooz..........
 
unatehemea nini kama kazi ya chdm ni kuwatukana mbatia na lipumba. nimewahi sema kuwa kwa mtindo huu chdm haitofika popote. juzi star tv lissu alivishambulia sana cuf na nccr. kama chdm hawatumii mbinu ya kuvisogeza karibu cuf na nccr, unategemea nini kitatokea? mbatia yuko sahihi kufanya vile. nashauri mmgombea wa nccr ajitoe kwenye uenyekiti ili kura zote za nccr zipelekwe ccm. pipooooooz..........

Kitatokea kilichotokea Arusha kwenye kura za udiwani
 
Mbatia analipa fadhila kwa Mwenyekiti wa CCM-Taifa kwani suala la kuteuliwa kuwa Mbunge si dogo kwake.Hapo ndipo ninapokubaliana na Kafulila kwamba Mwanaume aliyeshindwa na Mwanamke katika nafasi ya Ubunge hawezi kukiongoza chama ipasavyo!
tena mwenyekiti wa chama...
 
jamani kumbukeni Mbatia ni mbunge wa kuteuliwa na mwenyekiti wa ccm, privileges kama hizi hutokea mara chache sana na kwa watu maalumu.
 
Hivi wana jf na Chadema mlitegemea nini hapo,Mbatia kuipa CDM uongozi? hili suala lilikuwa wazi iwe hivyo chini ya M/kiti Mbatia,NCCR ingekuwa inaongozwa na mtu tofauti anayejua na kuheshimu upinzani hapo ingepasa tulalamike lkn kwa Mbatia,tuseme tu ila tusiumize vichwa CDM wajipange uchaguzi ujao wafanye kweli wakae chonjo na huyo mlipa fadhila.
wakuu naomba mnijibu mbona chadema hawajaishirikisha nccr kuunda kambi ya upinzani bungeni?
 
Kama unataka kupotosha, jua unapotosha tu waliozaliwa baada ya 2010... Vyama vyote vya upinzani vyenye wabunge ndivyo vilivyokataa kujumuishwa kwenye kambi rasmi ya upinzani. JF yenyewe inatosha kukukumbusha, nenda kwenye previous threads kama umesahau...

Usitufanye sisi ni wajinga na hatuna Kumbukumbu. Hebu soma Taarifa hii hapa chini halafu ujipime ujinga wako

[h=2]Feb 17, 2011[/h] [h=3]Nini hiki Upinzani ndani ya Upinzani![/h]

Freeman Mbowe, Mkuu wa Kambi ya Upinzani (Chadema)



Hamad Rashid, aliyekuwa Mkuu wa Kambi ya Upinzani (CUF)



David Kafulila, Mbunge (NCCR Mageuzi)

BISHOP J. HILUKA

Dar es salaam


KUNA kila dalili kwamba vyama vya upinzani ndani ya bunge vimemeguka baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuchukua nafasi zote za juu za uongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni bila kuvihusisha vyama vingine.



Vyama hivyo vya upinzani vimeunda kambi mbili za upinzani katika Bunge la Jamhuri la Muungano baada Chadema kuunda kambi yake ikijitegemea kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wabunge huku Chama cha Wananchi (CUF) kikiungana na NCCR-Mageuzi, TLP na UDP kuunda kambi nyingine.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mambo ya Bunge wa chadema, John Mrema, nafasi ya Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe na makamu wake ni Naibu Katibu Mkuu wa chadema na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe. Nafasi ya Mnadhimu wa Kambi hiyo ni Mbunge wa Singida Kusini, Tundu Lissu.


Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, chama kinachofikisha asilimia 12 ya wabunge kina uwezo wa kuunda kambi ya upinzani bungeni. Chadema kimezidi asilimia hizo baada ya kupata wabunge 23 wa kuchaguliwa kwenye majimbo na 23 wa viti maalum. Hata hivyo, imezuka minong'ono kwa baadhi ya vyama vya upinzani vikidai kuwa Chadema kimehodhi kambi yote ya upinzani na kuviacha solemba vyama hivyo.


Awali ilielezwa kuwa CUF kilichokuwa kikishikilia uongozi wa kambi hiyo katika Bunge lililopita kingekiunga mkono Chadema katika kambi ya upinzani na katika nafasi ya mgombea wa nafasi ya Spika ambayo tayari inashikiliwa na Anne Makinda wa CCM.

Badala yake CUF waliamua kukaa kimya, ukimya wao ulitafsiriwa kuwa ulilenga kuiunga mkono CCM badala ya Chadema na ndivyo ilivyojidhihirisha baada Makinda kuzoa kura 265 huku mpinzani wake kutoka Chadema akiambulia kura 53 tu, wakati wabunge wa upinzani wapo kama 86 hivi.

Pamoja na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid kukanusha madai hayo lakini imezidi kujidhihirisha hata wakati wa kugombea nafasi ya Unaibu spika, ambapo Job Ndugai wa CCM alipata kura 276 kati ya 328 zilizopigwa (asilimia 84,2) na kumwacha Mustafa Akunay wa Chadema akiambulia kura 46 tu (idadi ya wabunge wa Chadema), sawa na asilimia 14, huku kura sita zikiharibika.



Mbunge wa Kigoma Kaskazini ambaye pia ni naibu kiongozi wa upinzani bungeni, Zitto Kabwe alisema kuwa hoja ya kuhodhi kambi ya upinzani na kuifanya kuwa ya Chadema badala ya upinzani wote, siyo jambo la ajabu kwani ni utaratibu unaofanywa hata na nchi nyingine, chama chenye wabunge wengi ndicho kinachotoa waziri mkuu kwa hiyo hata Chadema kwa kuwa kina wabunge wengi kuliko vyama vingine vya upinzani kina haki ya kuunda kambi ya upinzani.


Inanitatiza kidogo, iweje suala la kambi ya upinzani bungeni kuhodhiwa na Chadema liwe 'issue' ya kuwafanya wapinzani wasishirikiane? Au kuna ajenda nyingine zaidi ya hiyo? Mbunge wa Wawi, Ahamed Rashid anaposema kuwa wameamua kuunda kambi yao kwa kushirikiana na NCCR-Mageuzi baada ya Chadema kushindwa kutimiza sharti la kushirikisha vyama vingine kwenye kambi ya upinzani ni jambo la kushangaza kwa kuwa hata wao hawakuvishirikisha vyama vya NCCR-Mageuzi na Chadema walipounda kambi ya upinzani bungeni mwaka 1995.


Inaposemwa kuwa uwepo wa Serikali kivuli ya Chadema bila ushirikiano na CUF ni kitu kibaya, wanasahau kuwa ni CUF hiyo hiyo iliyowahi kuvizunguka NCCR-Mageuzi na Chadema kikaungana na UDP na kuunda Serikali kivuli. Hatukusikia malalamiko kutoka Chadema wala NCCR-Mageuzi. Mimi nadhani kuna viongozi ambao wanataka kuhubiri na kuendeleza tofauti ambazo zinapaswa kupigwa vita, na kinachojitokeza sasa ni Upinzani ndani ya Upinzani!

Mbunge wa Vunjo ambaye pia ni mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema alisema haoni kama kuna tatizo kwa kambi yote ya upinzani kwenda Chadema, na kusisitiza kuwa Chadema wana vijana wengi wazuri ambao wataleta changamoto kubwa Bungeni. Pia sheria za Bunge zinawaruhusu, hivyo hakuna sababu ya kuwalalamikia kwani huwezi kumlazimisha mtu akupende.

kinyang'anyiro cha uspika kilichompa ushindi wa kishindo Anne Makinda wa CCM, kimeonesha kuwepo kwa dalili ya kutokujitosheleza kwa kambi nzima ya upinzani. Wapinzani wanahitaji kuungana ili kuwa na nguvu zaidi kama kweli wana nia ya kuleta changamoto kwa serikali.



Kwa hali hii inanifanya nidhani kuwa pengine baadhi ya wapinzani hawajajitambua na hawajui wanataka nini au wapo kwa makusudi fulani. Ukiangalia hata kwenye majimbo mengi kufuatia uchaguzi wa wabunge utagundua kuwa wapinzani wangeweza kupata wabunge wengi zaidi, pengine ni zaidi ya wabunge 100! Mfano katika mkoa wa Dar e Salaam ambapo wapinzani wameshinda majimbo mawili tu; Kawe na Ubungo, lakini kwa mujibu wa matokeo halisi ni kwamba wameshinda pia majimbo ya Segerea, Kinondoni na Temeke ambako kura za ubunge zilikuwa nyingi kwa wapinzani kuliko kwa CCM.


Hii inadhihirishwa na matokeo kutoka majimbo mbalimbali ambapo wapinzani waliongoza lakini ni CCM iliyoibuka kidedea.


Ni wakati sasa wa watu wanaojiita wapinzani kuamua kuwa wapinzani au kujiunga na CCM.
 
Lakini hii nayo ni substandard ya CDM, inabidi viongozi wa ngazi ya juu watueleze. Tushakubaliana kuwa vyama vyote vingine ni CCM-B ndio maana hata Bungeni hatujaungana na vyama hivi. Sasa hili la makubaliano ya kuongoza Halmashauri ya Uvinza inatokea wapi? Nampongeza Mh. Mbatia kwa kutukumbusha anawakilisha wing ipi.

Kitakachotokea ni kuwa makamu mweyekiti ataendelea kuula na kuwa ndiye mwenyekiti.
 
Tukiwambia vyama vyao wanasumbuliwa na njaa na uroho wa madaraka utawasikia wanapiga kelele.

Nafasi ya mwenyekiti wa halmashauri wanataka kutoana macho utafikiri fisi waliorushiwa mfupa. Wako radhi kukosa vyote kwa sababu njaa na uroho wa madaraka vimewatangulia mpaka hekima na busara vinawakimbia.

Badala ya kuwafikiria wananchi kwanza, kwa sasa wanachofikiria ni pesa na madaraka.

Kuna vyama vingine vinajinadi ni vyama vya demokrasia na maendeleo wakati hawawezi hata kusimamia jina la chama chao.

Ulaghai haufichwi and CCM claims vindicated.
 
aisee hawa jamaa wa chadema huwa nacheka sana na kuwashangaa sana hivi karibuni Tundu Lisu alisema chama pinzani Tanzania ni cdm pekee vingine ni ccmb sasa imakuwaje wanapotaka vyeo wanaenda kwa hao hao ili wawaunge mkono? halafu kwa nini wasingegombea umakamo na nccr wagombee umwenyekiti kwa hiyo wanataka wao wawe na power kuliko wengine mimi nawashauli waache kulialia na wajue mtenda akitendewa huhisi kuonewa
 
Mbatia anaiua NCCR Kigoma ambapo ndio paliifanya NCCR iendelee kuwepo sasa kwa mikono yake mwenyewe, Mwenyekiti ameamua kukimaliza chama chake kwa mikono yake mwenyewe.

Kwa hali hiyo tusishangae NCCR ikazikwa rasmi Kigoma mwaka 2015.
 
jamani kumbukeni Mbatia ni mbunge wa kuteuliwa na mwenyekiti wa ccm, privileges kama hizi hutokea mara chache sana na kwa watu maalumu.

mkuu, suala la meya wa uvinza halina uhusiano na ubunge wa mbatia. CHADEMA walilikoroga tangia mwanzo sasa hawana budi kulinywa tu
 
Mbatia anaiua NCCR Kigoma ambapo ndio paliifanya NCCR iendelee kuwepo sasa kwa mikono yake mwenyewe, Mwenyekiti ameamua kukimaliza chama chake kwa mikono yake mwenyewe.

Kwa hali hiyo tusishangae NCCR ikazikwa rasmi Kigoma mwaka 2015.

CHADEMA bana, hivi leo hii mnahitaji huruma za mbatia? nyie si ndio mlisema kuwa mna uwezo wa kusimama peke yenu na kwamba hamhitaji mbeleko ya vyama vingine. poleni sana
 
NCCR-Mageuzi ni chama cha kisiasa kilichoundwa na CCM ikiwa ni kuwaridhisha donors kuwa wameridhia matakwa yao, kwa kuwa licha ya kuundwa tume na rais Mwinyi chini ya uangalizi wa Nyerere (RIP), ililazimika kuunda vyama vya kuzugia ikiwemo NCCR.
 
Kwanini CDM hawaku compromise na kuwaachia NCCR?angalau NCCR tunawaona wabunge wake wanaguswa na matatizo ya wananchi na wangewasaidia kuliko kuwaachia CCM waendeleze propaganda zao kuwa sie wananchi tunawakubali!Kwa utaratibu huu ni kweli mnatukatisha tamaa sana wananchi kwani watawala wanazidi kuwa na kiburi kwa kuwa na uhakika wa kututawala milele wao na vizazi vyao!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Ni kweli inavyoonekana NCCR wataunga mkono CCM kwenye nafasi ya Mkiti pia.

cdm siku zote tujipange wenyewe , tusitegemee hivi vyama vya ruzuku , dawa pekee ni kushinda kila kitu kwenye uchaguzi .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom