Mbagala inahitajika underground train sio Mkulupuko za mwendokasi

Mcharo son

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Posts
6,129
Reaction score
5,076
Mwendokasi imeshathibitisha kushindwa katika awamu za mwanzo ukiangalia usafiri wa shida wanaopata Kimara. Japo hapa siasa zitaletwa kutetea hoja, lakini ukweli ndio huo. Nashangaa jitihada zinazoendelea kuleta huo mwendokasi kwa wakazi wa Mbagala. Tayari kituo cha gerezani kinaimalishwa na kule Mbagala rangi3 ili kuegesha mabasi hayo. Sasa hii sijui ni kuweka sawa ili 2020 itumike kuombea kura/la kwa wakazi wa Mbagala. Harafu wakazi wa huko nawashangaa! yaani kimya wakati wanasogezewa janga. Sasa hivi usafiri Mbagala kuja mjini ni mzuri mara 10 ya ule wa Kimara na Mbezi.

Ningekuwa mimi kwenye kiti cha maamuzi NINGESIMAMISHA KWANZA HUU MRADI NA KUTAFAKARI NJIA NZURI ZAIDI YA USAFIRI WA MWENDOKASI ambao sio mwingine zaidi ya underground train( treni ya chini kwa chini kwa route ya Mbagala). Hata kama itachukua miaka kumi kukamilisha ni kheri kuliko mkurupuko huu.
Network ya mwendokasi jijini haifai hususani Mbagala kwa sababu: inasababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara iliopo kwa kuchimba mashimo yalioinuka (matuta) kwenye barabara iliopo. hii inaongeza kwa uchakavu wa magari na ucheleweshaaji wa magari mengine yanayotumia njia hiyo mfano gari/roli litalazimika kusimama kila kituo watu wavuke. sasa kuna magari makubwa yanaitegemea Kilwa road kupeleka na kutoa bidhaa katika viwanda vilivyopo Mbagala na njia ya Kilwa road kwa ujumla.. Shughuli za viwandani zitacheleweshwa na mashimo haya mafundi watakubariana na mimi, kuwa gari lazima litaenda service mapema kulinganisha na yale yanayopita njia isiyokuwa na mashimo. Haya Ndio maandalizi ya kuelekea 2025 ya viwanda!
Ningekuwa mimi kwenye kiti cha maamuzi, fungu la kujenga mwendokasi Mbagala ningelitumia kutengeneza njia au barabara ingine kuu ya kuingia Mbagala kupitia Tandika Buzza. hii ingesaidia sana kupunguza msongamano wa magari na kuboresha usafiri wa mabasi uliopo sasa. Eneo lililopo kwa ajili ya kujenga mwendokasi njia ya Kilwa road ndio ningelitumia kujenga TRENI YA CHINI KWA CHINI. Na hii ndio ningeiita mwendokasi mana hakuna trafik light za kupunguza kasi kama ilivyo kwa huu mkurupuko wa sasa. Mtanisamehe natumia jina mkurupuko mana naona ni kama vile uchunguzi yakinifu haukufanyika na kuona TATIZO KAMA HILI LINALOJITOKEZA SASA.
Njia karibu zote zinazoingia mjini kwa sasa zimejengewa njia mbadala. mfano kwa mtu wa Kimara Mbezi ya kule badala ya kutegemea Morogoro road anaweza zunguka Madale au Segerea, Gongolamboto badala ya njia ya airport anaweza zungukia Tabata. Sasa ni muhimu njia ya Kilwa road ipatiwe mbadala wa kuzungukia Tandika Buza. Itasaidia sana sana kuliko huu mkurupuko wa mwendokasi mnaotaka kuuweka. Na nyie wakazi wa Mbagala mmezidi ukimya hamuoni mkurupuko huu unaenda kuwadodesha.
Kilwa road imetulia wahusika msiiharibu na mkurupuko wenu wa mwendokasi. Sawazisheni pale Bandarini kuingia mjini iwe njia nne. Baada ya hapo fuateni mawazo yangu msiitibue Kilwa road please!!!
 
Angalizo Mchambue hoja sio uwasilishaji wa hoja(kiswahili kigumu na simu zetu za tecno ndio shida zaidi)
 
Underground Train? Kama hali iko hivi kwa kutekeleza miradi iliyopo...wakianza na hiyo underground train ...underground...underground....Mkuu unataka tufike kilo ngapi au tufe kabisa?
Talatibu ndio mwendo, wajipange wakiacha MIKURUPUKO mambo yataenda
 
Mcharo son umefanya tafiti kuhusu underground train gharama ya ujenzi?mawazo matupu bila kufanya tafiti ni sawa na kupiga kelele...

Gharama Za ujenzi wa mwendokasi na matokeo yake inasaidia zaidi kwa sasa,kinachotokea kule kimara ni uhaba wa buses ambao ni tatizo dogo sana sijui wahusika wanakwama wapi,

Nimetumia sana mwendokasi route ya kimara hadi town ni kweli usiopingika inaokoa wakati sana tena kuliko unavyofikiri!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reli hii hii iliyopo ingetandazwa ifike Mbagala.
Huko Mbezi pia inatakiwa reli, hasa kikikamilika kituo cha mabasi ya masafa marefu.
Treni ya Pugu inataikiwa ifike Mbezi Bus Terminal.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwendokasi imeshathibitisha kushindwa katika awamu za mwanzo ukiangalia usafiri wa shida wanaopata Kimara. Japo hapa siasa zitaletwa kutetea hoja, lakini ukweli ndio huo. Nashangaa jitihada zinazoendelea kuleta huo mwendokasi kwa wakazi wa Mbagala. Tayari kituo cha gerezani kinaimalishwa na kule Mbagala rangi3 ili kuegesha mabasi hayo. Sasa hii sijui ni kuweka sawa ili 2020 itumike kuombea kura/la kwa wakazi wa Mbagala. Harafu wakazi wa huko nawashangaa! yaani kimya wakati wanasogezewa janga. Sasa hivi usafiri Mbagala kuja mjini ni mzuri mara 10 ya ule wa Kimara na Mbezi.

Ningekuwa mimi kwenye kiti cha maamuzi NINGESIMAMISHA KWANZA HUU MRADI NA KUTAFAKARI NJIA NZURI ZAIDI YA USAFIRI WA MWENDOKASI ambao sio mwingine zaidi ya underground train( treni ya chini kwa chini kwa route ya Mbagala). Hata kama itachukua miaka kumi kukamilisha ni kheri kuliko mkurupuko huu.
Network ya mwendokasi jijini haifai hususani Mbagala kwa sababu: inasababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara iliopo kwa kuchimba mashimo yalioinuka (matuta) kwenye barabara iliopo. hii inaongeza kwa uchakavu wa magari na ucheleweshaaji wa magari mengine yanayotumia njia hiyo mfano gari/roli litalazimika kusimama kila kituo watu wavuke. sasa kuna magari makubwa yanaitegemea Kilwa road kupeleka na kutoa bidhaa katika viwanda vilivyopo Mbagala na njia ya Kilwa road kwa ujumla.. Shughuli za viwandani zitacheleweshwa na mashimo haya mafundi watakubariana na mimi, kuwa gari lazima litaenda service mapema kulinganisha na yale yanayopita njia isiyokuwa na mashimo. Haya Ndio maandalizi ya kuelekea 2025 ya viwanda!
Ningekuwa mimi kwenye kiti cha maamuzi, fungu la kujenga mwendokasi Mbagala ningelitumia kutengeneza njia au barabara ingine kuu ya kuingia Mbagala kupitia Tandika Buzza. hii ingesaidia sana kupunguza msongamano wa magari na kuboresha usafiri wa mabasi uliopo sasa. Eneo lililopo kwa ajili ya kujenga mwendokasi njia ya Kilwa road ndio ningelitumia kujenga TRENI YA CHINI KWA CHINI. Na hii ndio ningeiita mwendokasi mana hakuna trafik light za kupunguza kasi kama ilivyo kwa huu mkurupuko wa sasa. Mtanisamehe natumia jina mkurupuko mana naona ni kama vile uchunguzi yakinifu haukufanyika na kuona TATIZO KAMA HILI LINALOJITOKEZA SASA.
Njia karibu zote zinazoingia mjini kwa sasa zimejengewa njia mbadala. mfano kwa mtu wa Kimara Mbezi ya kule badala ya kutegemea Morogoro road anaweza zunguka Madale au Segerea, Gongolamboto badala ya njia ya airport anaweza zungukia Tabata. Sasa ni muhimu njia ya Kilwa road ipatiwe mbadala wa kuzungukia Tandika Buza. Itasaidia sana sana kuliko huu mkurupuko wa mwendokasi mnaotaka kuuweka. Na nyie wakazi wa Mbagala mmezidi ukimya hamuoni mkurupuko huu unaenda kuwadodesha.
Kilwa road imetulia wahusika msiiharibu na mkurupuko wenu wa mwendokasi. Sawazisheni pale Bandarini kuingia mjini iwe njia nne. Baada ya hapo fuateni mawazo yangu msiitibue Kilwa road please!!!
Mbona wewe ndio umekurupuka?

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Mcharo son umefanya tafiti kuhusu underground train gharama ya ujenzi?mawazo matupu bila kufanya tafiti ni sawa na kupiga kelele...

Gharama Za ujenzi wa mwendokasi na matokeo yake inasaidia zaidi kwa sasa,kinachotokea kule kimara ni uhaba wa buses ambao ni tatizo dogo sana sijui wahusika wanakwama wapi,

Nimetumia sana mwendokasi route ya kimara hadi town ni kweli usiopingika inaokoa wakati sana tena kuliko unavyofikiri!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mambo mengine hayahitaji utafiti. Basi la mwendokazi linalopita hizo njia, halitakuwa na kasi kama lingepita chini kwa chini kama treni. Kweli underground train inaweza kuwa na gharama zaidi, lakini ni kheri kusubiri uwezo UPATIKANE kuliko kukurupuka. Nani alijua kama raisi Magufuri angeweza kununua ndege kwa kasi hii. Wengine wangesema nchi haina pesa.
 
Mbona wewe ndio umekurupuka?

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Fafanua zaidi...... kupendekeza njia mbadala ya Mbagala kuachana figisu hizi za usafiri wa mwendokasi nimekurupuka. Wewe sio mtumiaji wa mabasi haya na hautimii route hiyo. Sikiliza wanaotumia .
 
Kuna mambo mengine hayahitaji utafiti. Basi la mwendokazi linalopita hizo njia, halitakuwa na kasi kama lingepita chini kwa chini kama treni. Kweli underground train inaweza kuwa na gharama zaidi, lakini ni kheri kusubiri uwezo UPATIKANE kuliko kukurupuka. Nani alijua kama raisi Magufuri angeweza kununua ndege kwa kasi hii. Wengine wangesema nchi haina pesa.
Mipango ya nchi ndio inatekelezwa, kabla I huu mradi wa mwendokasi kuanza kuna watu walizunguka uko duniani wakala posho na gharama mob za vikao wakaja na huo muarobaini,Leo ghafla tu waje na underground train lol hakuna nchi inaendeshwa hivyo...

Idea ya kununua ndege inamanufaa zaidi kwa sababu ni kweli shirika lilikua kama mfu, angalia wameshapata deal ya watalii 10000 kutoka China ambao kila week wanakuja 262, hao unawafuata mwenyewe unawaleta hadi Tz, unapiga pesa ya nauli na bado unapiga pesa ya utalii wao. ..hii ndio akili kubwa

Nikukumbushe sekta ya utalii tu mwaka jana imeingizia taifa $2.44bln ambayo ni zaidi ya tsh5 trillions, hapo ni wageni 1.5M ndio waliozuru,Hawa wakihamasishwa wakafika 2M ni possible kupata zaidi ya $3.5B

Basi wasitishe kwanza, kuliko kutuletea mashimo kwenye Kilwa road yetu pendwa. Kwanza wafikilie kujenga road ingine ya kuchimba mashimo. Hatuna haraka. Hata wakiacha ni bora zaidi!1
 
Usiseme Hamna haraka,iyo kilwa road itajengwa two flyovers haina taa haina sehemu ya watembea kwa miguu itaboreshwa zaidi itapendeza zaidi

Ukitaka uzuri sharti uzurike,miaka mitatu kama hao wachina wakiwa makini mradi umeisha unasahau mashimo na vumbi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiseme Hamna haraka,iyo kilwa road itajengwa two flyovers haina taa haina sehemu ya watembea kwa miguu itaboreshwa zaidi itapendeza zaidi

Ukitaka uzuri sharti uzurike,miaka mitatu kama hao wachina wakiwa makini mradi umeisha unasahau mashimo na vumbi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye kila kituo cha mwendokasi kuna mashimo (matuta). sasa utajenga flyover kila kituo!! No kuna round about kibao Kilwa road, hizo zote zitageuka kuwa njiapanda za mataa. Kusimama kila wakati hakuna mwendokasi hapo! Underground train NDIO SULUHISHO MBAGALA nchi yetu sio masikini. Na korosho ndio zinapita njia hiyo SITAKI ICHIMBWE MASHIMO PLEASE!!
 
Mwendokasi ni vitu viwili. Miundombinu na uendeshaji.

Miundombinu ipo haina shida. Tatizo lipo kwenye uendeshaji uliogubikwa na rushwa toka mwanzo. Kuna ma bus yapo bandarini hayajalipiwa kodi hadi leo. Zama zile yangeingia bure.

Lakini kitu kingine ni vita kubwa kati ya wala rushwa wa awamu ya nne na hawa wa awamu ya tano.

Wazamani hawataki kuachia mkate.
 
Write your reply...

ila kwa mbagala wakileta ule upuuzi wa kimara,watadoda mapemaaa

Dart ongezeni mabasi yawe mengi,kwani mna matatizo gani??..miundombinu inaharibika hairekebishwi aaagriiih
 
Back
Top Bottom