Mbagala inahitajika underground train sio Mkulupuko za mwendokasi

Hata mimi nilikuwa nafikiri kitu kama hicho. Ubarikiwe sana kwa kuleta hii hoja.
Rais wa Ufaransa aalikwe Tz kama alivyofanya Kenyata. Huenda akatusaidia katika hili.
 
Mwendokasi ni vitu viwili. Miundombinu na uendeshaji.

Miundombinu ipo haina shida. Tatizo lipo kwenye uendeshaji uliogubikwa na rushwa toka mwanzo. Kuna ma bus yapo bandarini hayajalipiwa kodi hadi leo. Zama zile yangeingia bure.

Lakini kitu kingine ni vita kubwa kati ya wala rushwa wa awamu ya nne na hawa wa awamu ya tano.

Wazamani hawataki kuachia mkate.
Hapo nilipopigia mstali ndio nina tatizo napo. Mbagala Kilwa road wasiitibue. Matatizo waliokuwa wanayapata Mbagala kabla ya kuboresha hiyo barabara wanayajua wenyewe. Mbagala ilikuwa eneo duni hapa Dar
 
Write your reply...

ila kwa mbagala wakileta ule upuuzi wa kimara,watadoda mapemaaa

Dart ongezeni mabasi yawe mengi,kwani mna matatizo gani??..miundombinu inaharibika hairekebishwi aaagriiih
Hujaona KADHIA INAYOKUJA WEWE. Kwanza watasimamisha yale mabasi ya Kisemvule - Gerezani na yaendayo Kisewe. Itakuwa ni basi za mwendokasi tu (viti watu kumi kukaa mwisho) wengine mtasimama mwanzo mwisho. Wale maninja wa kuingia dirishani ndio viwanja vyao vinatayarishwa
 
Ndoto za maendeleo ni NZURI kuliko kupiga siasa hasi
Hebu rudi kaangalie gharama za kujenga Treni ya chini ni kiasi gani!!..
Ulishawahi soma utafiti wa kwanini mwendokasi ndio suluhisho Tz?
 
Mwendokasi imeshathibitisha kushindwa katika awamu za mwanzo ukiangalia usafiri wa shida wanaopata Kimara. Japo hapa siasa zitaletwa kutetea hoja, lakini ukweli ndio huo. Nashangaa jitihada zinazoendelea kuleta huo mwendokasi kwa wakazi wa Mbagala. Tayari kituo cha gerezani kinaimalishwa na kule Mbagala rangi3 ili kuegesha mabasi hayo. Sasa hii sijui ni kuweka sawa ili 2020 itumike kuombea kura/la kwa wakazi wa Mbagala. Harafu wakazi wa huko nawashangaa! yaani kimya wakati wanasogezewa janga. Sasa hivi usafiri Mbagala kuja mjini ni mzuri mara 10 ya ule wa Kimara na Mbezi.

Ningekuwa mimi kwenye kiti cha maamuzi NINGESIMAMISHA KWANZA HUU MRADI NA KUTAFAKARI NJIA NZURI ZAIDI YA USAFIRI WA MWENDOKASI ambao sio mwingine zaidi ya underground train( treni ya chini kwa chini kwa route ya Mbagala). Hata kama itachukua miaka kumi kukamilisha ni kheri kuliko mkurupuko huu.
Network ya mwendokasi jijini haifai hususani Mbagala kwa sababu: inasababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara iliopo kwa kuchimba mashimo yalioinuka (matuta) kwenye barabara iliopo. hii inaongeza kwa uchakavu wa magari na ucheleweshaaji wa magari mengine yanayotumia njia hiyo mfano gari/roli litalazimika kusimama kila kituo watu wavuke. sasa kuna magari makubwa yanaitegemea Kilwa road kupeleka na kutoa bidhaa katika viwanda vilivyopo Mbagala na njia ya Kilwa road kwa ujumla.. Shughuli za viwandani zitacheleweshwa na mashimo haya mafundi watakubariana na mimi, kuwa gari lazima litaenda service mapema kulinganisha na yale yanayopita njia isiyokuwa na mashimo. Haya Ndio maandalizi ya kuelekea 2025 ya viwanda!
Ningekuwa mimi kwenye kiti cha maamuzi, fungu la kujenga mwendokasi Mbagala ningelitumia kutengeneza njia au barabara ingine kuu ya kuingia Mbagala kupitia Tandika Buzza. hii ingesaidia sana kupunguza msongamano wa magari na kuboresha usafiri wa mabasi uliopo sasa. Eneo lililopo kwa ajili ya kujenga mwendokasi njia ya Kilwa road ndio ningelitumia kujenga TRENI YA CHINI KWA CHINI. Na hii ndio ningeiita mwendokasi mana hakuna trafik light za kupunguza kasi kama ilivyo kwa huu mkurupuko wa sasa. Mtanisamehe natumia jina mkurupuko mana naona ni kama vile uchunguzi yakinifu haukufanyika na kuona TATIZO KAMA HILI LINALOJITOKEZA SASA.
Njia karibu zote zinazoingia mjini kwa sasa zimejengewa njia mbadala. mfano kwa mtu wa Kimara Mbezi ya kule badala ya kutegemea Morogoro road anaweza zunguka Madale au Segerea, Gongolamboto badala ya njia ya airport anaweza zungukia Tabata. Sasa ni muhimu njia ya Kilwa road ipatiwe mbadala wa kuzungukia Tandika Buza. Itasaidia sana sana kuliko huu mkurupuko wa mwendokasi mnaotaka kuuweka. Na nyie wakazi wa Mbagala mmezidi ukimya hamuoni mkurupuko huu unaenda kuwadodesha.
Kilwa road imetulia wahusika msiiharibu na mkurupuko wenu wa mwendokasi. Sawazisheni pale Bandarini kuingia mjini iwe njia nne. Baada ya hapo fuateni mawazo yangu msiitibue Kilwa road please!!!
Wewe jamaa upo sawa kichwani. Underground train kwa uchumi gani. Hizo pesa za kujenga flyover na reli SGR inawatoa jasho watanzania.

Hapa mkianzisha underground train mtamtukana Magu mchana na usiku.

Nchi haina huo uwezo wa kugharamia ujenzi wa hiyo makitu.
 
Kabla hujanipeleka kwenye tafiti zako tupitie kwanza tafiti za UTAJIRI WA NCHI YETU. ndio twende unakotaka niende. Narudia kusema kama pesa hakuna sasa, hakuna HARAKA. Sitisha mkurupuko weka miundombinu isiyokuwa na mashimo. Tutaelewana tu taratibu
 
Wewe jamaa upo sawa kichwani. Underground train kwa uchumi gani. Hizo pesa za kujenga flyover na reli SGR inawatoa jasho watanzania.

Hapa mkianzisha underground train mtamtukana Magu mchana na usiku.

Nchi haina huo uwezo wa kugharamia ujenzi wa hiyo makitu.
Nipo sawa mkuu, Magufuri alipoanza kununua ndege kuna waliosema kama wewe. Haraka haraka haina baraka.
 
TUKITAKA MAENDELEO TUANGALIE THE BEST WAY! No matter what comes! penye nia pana njia. Tena bila mateso kama haya ya mkurupuko
 
Nipo sawa mkuu, Magufuri alipoanza kununua ndege kuna waliosema kama wewe. Haraka haraka haina baraka.
Hiyo project usifananishe na ndege mkuu.

Haya mabasi na njia hizo hazina shida tatizo ni usimamizi mbovu na wahusika kushindwa kufanya maamuzi sahihi. Wanasubiri hadi Magufuli aingilie kati.
 
Simuelewi mtu anayetaka kuchimba mashimo kwenye the only road kama kilwa road! Jaribu kunisoma vizuri. Unaweza kuona hazipo LAKINI..........
 
Mkuu unasema wananchi tumetulia doro,unataka tuandamane au...Tuandamane ujenzi Wa barabara ya mwendo kasi
 
Majiji yote makubwa duniani usafiri wa kuaminika ni usafiri wa treni. Uzuri wa treni ni uwezo wake mkubwa wa kubeba abiria wengi kwa wakati mmoja. Ilibidi kuwe na treni katika njia zote kuu, halafu haya mabasi ya mwendokasi yawe ndio yanaingia huko ndani ndani kuwaleta abiria kwenye vituo vya treni. Sio lazima zipite underground zinaweza tu kuwa treni za kawaida ila ziende route zile zenye watu wengi. Na ziwe na muda maalum ambao zinapita. Mbona tatizo la foleni na usafiri litakua historia?
 
Serikali ilishindwa kuplan mipango miji mda mrefu. Kupanga barabara na huduma zingine za jamii nk nk.ni sawa na kuoa halafu unajenga nyumba ya vyumba viwili then unazaa watoto 10.

Tunafikiria leo pasipo kuangali kesho watu wanaongezeka na huduma zaidi zinahitajika.mfano tungekua na barabara 4 zinaenda na 4 zinarudi tusingekuwa na hii shida.

Mwisho wa siku tunajenga na kuvunja ambayo ni gharama sana kuhamisha vitu na watu kwa kuwafidia.kuleta mwendokasi mbagala wajipange
 
Mkuu unasema wananchi tumetulia doro,unataka tuandamane au...Tuandamane ujenzi Wa barabara ya mwendo kasi
Kuna njia nyingi za kupiga kelele sio lazima kuandamana. Mfano nimetoa wazo. Je umelionaje? Wakati wa uchaguzi utawachagua hao wanaokurupuka! Mbagala wameandamana sana enzi za njia mbili. Ikinyesha mvua watu walikuwa wanatembea kutoka Bandari mpaka mbagala. maandamano sio suruhisho la matatizo
 
Kwa aina ya mvua tunazopata nchini(torrential rains), kwa aina ya landscape ya jiji la Dar es salaam, kwa negligence iliyopo kwa watendaji wakuu, kwa uzembe uliopo na mwisho kwa uchumi wetu, sidhani kama tayari tumefikia huko.

Tuboreshe kwanza hizo mwendo kasi, tuwe na ufanisi nazo, tupate experience kupitia hizo, baada ya hapo labda tunaweza kufikiri kuhusu underground trains. Lakini hata kabla ya kufikiria underground trains, kuna trains za kawaida, Kibaha - City centre, Bagamoyo - City centre, Kisarawe-Mbagala-City centre inaweza kuwa starting point.
 
Serikali ilishindwa kuplan mipango miji mda mrefu. Kupanga barabara na huduma zingine za jamii nk nk.ni sawa na kuoa halafu unajenga nyumba ya vyumba viwili then unazaa watoto 10.

Tunafikiria leo pasipo kuangali kesho watu wanaongezeka na huduma zaidi zinahitajika.mfano tungekua na barabara 4 zinaenda na 4 zinarudi tusingekuwa na hii shida.

Mwisho wa siku tunajenga na kuvunja ambayo ni gharama sana kuhamisha vitu na watu kwa kuwafidia.kuleta mwendokasi mbagala wajipange
Umeliona hilo lipo linakuja, watakuja kuvunja na kubomoa hizi njia za mwendokasi waweke njia za chini hapo baadae. Inawezekana kwa utajili wa nchi yetu, sema nafikilia gharama za kubomoa!
 
Mwendokasi imeshathibitisha kushindwa katika awamu za mwanzo ukiangalia usafiri wa shida wanaopata Kimara. Japo hapa siasa zitaletwa kutetea hoja, lakini ukweli ndio huo. Nashangaa jitihada zinazoendelea kuleta huo mwendokasi kwa wakazi wa Mbagala. Tayari kituo cha gerezani kinaimalishwa na kule Mbagala rangi3 ili kuegesha mabasi hayo. Sasa hii sijui ni kuweka sawa ili 2020 itumike kuombea kura/la kwa wakazi wa Mbagala. Harafu wakazi wa huko nawashangaa! yaani kimya wakati wanasogezewa janga. Sasa hivi usafiri Mbagala kuja mjini ni mzuri mara 10 ya ule wa Kimara na Mbezi.

Ningekuwa mimi kwenye kiti cha maamuzi NINGESIMAMISHA KWANZA HUU MRADI NA KUTAFAKARI NJIA NZURI ZAIDI YA USAFIRI WA MWENDOKASI ambao sio mwingine zaidi ya underground train( treni ya chini kwa chini kwa route ya Mbagala). Hata kama itachukua miaka kumi kukamilisha ni kheri kuliko mkurupuko huu.
Network ya mwendokasi jijini haifai hususani Mbagala kwa sababu: inasababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara iliopo kwa kuchimba mashimo yalioinuka (matuta) kwenye barabara iliopo. hii inaongeza kwa uchakavu wa magari na ucheleweshaaji wa magari mengine yanayotumia njia hiyo mfano gari/roli litalazimika kusimama kila kituo watu wavuke. sasa kuna magari makubwa yanaitegemea Kilwa road kupeleka na kutoa bidhaa katika viwanda vilivyopo Mbagala na njia ya Kilwa road kwa ujumla.. Shughuli za viwandani zitacheleweshwa na mashimo haya mafundi watakubariana na mimi, kuwa gari lazima litaenda service mapema kulinganisha na yale yanayopita njia isiyokuwa na mashimo. Haya Ndio maandalizi ya kuelekea 2025 ya viwanda!
Ningekuwa mimi kwenye kiti cha maamuzi, fungu la kujenga mwendokasi Mbagala ningelitumia kutengeneza njia au barabara ingine kuu ya kuingia Mbagala kupitia Tandika Buzza. hii ingesaidia sana kupunguza msongamano wa magari na kuboresha usafiri wa mabasi uliopo sasa. Eneo lililopo kwa ajili ya kujenga mwendokasi njia ya Kilwa road ndio ningelitumia kujenga TRENI YA CHINI KWA CHINI. Na hii ndio ningeiita mwendokasi mana hakuna trafik light za kupunguza kasi kama ilivyo kwa huu mkurupuko wa sasa. Mtanisamehe natumia jina mkurupuko mana naona ni kama vile uchunguzi yakinifu haukufanyika na kuona TATIZO KAMA HILI LINALOJITOKEZA SASA.
Njia karibu zote zinazoingia mjini kwa sasa zimejengewa njia mbadala. mfano kwa mtu wa Kimara Mbezi ya kule badala ya kutegemea Morogoro road anaweza zunguka Madale au Segerea, Gongolamboto badala ya njia ya airport anaweza zungukia Tabata. Sasa ni muhimu njia ya Kilwa road ipatiwe mbadala wa kuzungukia Tandika Buza. Itasaidia sana sana kuliko huu mkurupuko wa mwendokasi mnaotaka kuuweka. Na nyie wakazi wa Mbagala mmezidi ukimya hamuoni mkurupuko huu unaenda kuwadodesha.
Kilwa road imetulia wahusika msiiharibu na mkurupuko wenu wa mwendokasi. Sawazisheni pale Bandarini kuingia mjini iwe njia nne. Baada ya hapo fuateni mawazo yangu msiitibue Kilwa road please!!!
Mkuu kinachokwamisha mwendokasi sasa sio miundombinu bali ni watendaji kazi.
Hata underground kama viongozi wabovu sio suluhisho.
 
Kwa aina ya mvua tunazopata nchini(torrential rains), kwa aina ya landscape ya jiji la Dar es salaam, kwa negligence iliyopo kwa watendaji wakuu, kwa uzembe uliopo na mwisho kwa uchumi wetu, sidhani kama tayari tumefikia huko.

Tuboreshe kwanza hizo mwendo kasi, tuwe na ufanisi nazo, tupate experience kupitia hizo, baada ya hapo labda tunaweza kufikiri kuhusu underground trains. Lakini hata kabla ya kufikiria underground trains, kuna trains za kawaida, Kibaha - City centre, Bagamoyo - City centre, Kisarawe-Mbagala-City centre inaweza kuwa starting point.
Tusijizarau. Mbagala imekaa vizuri hakuna mafuriko kule. Hata mifereji inakubari watu wakatumia njia ya maji kufika mjini. Kuanzia kijichi, pale chini ya daraja la TAZARA relini, muonekano wake ni rahisi kujenga usafiri wa boti endapo patachimbwa kuwezesha kupita boti. Ukisema haiwezekani haitawezekana. Try to think...........
 
Back
Top Bottom