KERO TANROAD,Hizi Taa Zitasababisha Ajali.

KERO TANROAD,Hizi Taa Zitasababisha Ajali.

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

RRONDO

Platinum Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
59,623
Reaction score
136,104
Kwenu Tanroads na wahusika wengine wa usalama barabarani. Taa za kuongoza magari katika makutano ya Barabara ya Kilwa na Barabara ya Kawawa zimesetiwa kimakosa. Taa hizi zinaruhusu magari yaa kawaida kunyoosha moja kwa moja na mabasi ya mwendokasi kukata kulshoto na kunyoosha kwa wakati mmoja. Ilivyotakiwa iwapo taa zitaruhisu magari kwenye njia ya kawaida kunyoosha na mabasi nayo yanyooshe. Na iwapo taa za mwendokasi zitaruhusu mabasi kukata kushoto ilibidi magari madogo yasimamishwe na taa hizo.
Kwa wasiojua nazungumzia eneo gani ni pale Chuo cha Diplomasia au Malao Maluu ya Uhamiaji.
20260904_095022.jpg

20260904_095021.jpg
 
Tuna changamoto pia maeneo ya Mombasa. Kama umetokea Moshi Bar kwa wale wanao jua sehemu hiyo, hakuna taa zinazokuruhusu wakati inaingia main road ili upite upande wa pili kwenda mjini. Unasubiri fadhili ya Red signal ya kuzuia magari yaliyotoka mjini au Gongo la mboto update nafasi ya kupita. Na wakati huo huo ndio Green signal ya mwendo kasi kupita.....
 
Kuna watu wanakula mishahara ya bure hii nchi
Hapa kinachosaidia hii junction iko busy hivyo magari yakifika hapo yanakuwa slow na jamaa wa mwendokasi ni wapole huwa wanasubiri. Ila kukiwa hamna gari mtu kajiachia akijua taa ni kijana lazima kiwake.
 
Tuna changamoto pia maeneo ya Mombasa. Kama umetokea Moshi Bar kwa wale wanao jua sehemu hiyo, hakuna taa zinazokuruhusu wakati inaingia main road ili upite upande wa pili kwenda mjini. Unasubiri fadhili ya Red signal ya kuzuia magari yaliyotoka mjini au Gongo la mboto update nafasi ya kupita. Na wakati huo huo ndio Green signal ya mwendo kasi kupita.....
Hapo unatakiwa utoke hadi service road halafu utumie service road kuingia main road huko mbele. Hii nimeona hapa kati ya mataa ya chang'ombe na Tamara. Huwezi kuingia main road direct ukitoka upa de wa Quality Plaza.
 
Back
Top Bottom