GREAT NAME
JF-Expert Member
- Aug 31, 2016
- 1,078
- 1,722
Nimesoma coment zote ila bado sijajua MB zinatengenezwaje na wapi labda nina kichwa maji
Hujajibu swali bado. Ameuliza hizo Mb zinatengenezwa wapi? Je mtu anaweza kijitengenezea za kwake binafsi?Nadhani, MB ni kikomo cha ww kutumia intanet.
Mfano unaambiwa ufike ofisini saa 3 asubuhi hiyo ni kikomo cha saa kufika kazini ila haina maana kuwa mwisho wa saa ya kufika kazini ni saa 3 mana muda bado unaendelea.
Intanet ni ujumla wa hizo KB, MB, GB, TB kwahy unapewa au unamegewa kipande/kifurushi cha intanet kulingana na pesa yako.
Sasa kwa kulingana na pesa yako ndio kuna vipande/kifurushi vya intanet ndio vikapewa majina kama KB, MB, GB TB
Pia kuna vifurushi vingine havina ukomo wa utumiaji wa intanet hiyo ni kwamba umeachwa utumie intanet bila kupewa kifurushi/kipande chenye ukomo.
Ni sawa na kwenye vifurushi vya ving'amuzi ni kwamba channel zipo nyingi ila unapewa channel kulingana na pesa yako, ndivyo hvy hvy intanet ipo ya kumwaga ila unapewa ukomo kulingana na pesa yako.
Umesoma uzi wote kuona comments za watu wengine au umekuja kwangu moja kwa moja?Hujajibu swali bado. Ameuliza hizo Mb zinatengenezwa wapi? Je mtu anaweza kijitengenezea za kwake binafsi?
hurudi kwa Bwana.Je zile Mb au dakika zinazobakia baada ya muda wa bundle kuisha huenda wapi?
Yaani unatakiwa uwe na nini na nini uwe na uwezo wa kutengeneza Mb zako? Hao wenye miundombinu mikubwa wanafanyaje ili wauze mb? Nadhani mtoa mada anataka aweze kuzitengeneza bila kupitia kwa mtu,au miundombinu ya mtu.Internet ni miundombinu, ukiwa na miundombinu na wewe unaweza uka charge na kuuza hizo mb.
Kuna miundombinu ya ndani nchini na miundombinu mikubwa ya Baharini/Nchi kavu.
So ili na wewe ucharge mb Inatakiwa
1. Utengeneze miundombinu yako
2. Ununue/ukodishe miundombinu ya wenzako.
Mfano kijijini kwenu km kama 10 umepita Mkonga wa Taifa, unaweza ukaenda TTCL ukanunua bandwidth, let's say 10GBps, hio ni capacity yako, halafu wewe mwenyewe ukatengeneza miundombinu yako ukatoa waya kwenye Mkonga mpaka kijijini, pale kijijini ukajenga minara na ili kila mtu apate halafu uka charge kutokana na matumizi.
Nakazia 👍👍majibu wanayotoa wadau yamekaa kI HKL
Shukran kiongoz nyiny ndio munatakiwa hapa jfVPN maana yake ni kwamba wewe unakuwa physiclly uko hapa lakini kifaa chako kime-connect tuseme na LAN ya watu walioko kwenye ofisi moja mahali fulani KOREA YA KUSINI au uingereza. Kwa hiyo ulionao phsically hapo ofisini kwako, COMPUTER yako haiwezi kuonana na computer zao pamoja na kwamba mpo wote kwenye chumba kimoja, isipokuwa inaweza kuonana na watu waliopo kwenye ofisi moja mahali fulani huko Korea ya Kusini au Uingereza, as if uko nao phsically mahali pale ulipo wewe
Nadhani nimejibu baada ya kusoma yako,anyway kuna wengine wamejazia nimepata mwanga,ni mada nzuri ya kujifunza/ kufikirisha. Tuendelee kuelimishana.Umesoma uzi wote kuona comments za watu wengine au umekuja kwangu moja kwa moja?
Ili usitumie miundombinu ya mtu inabidi usambaze waya mwenyewe dunia nzima. Kama unataka kumtext mtu China uhakikishe waya zako zinatoka Tanzania hadi China, kifupi sio realistic kutotumia miundo mbinu ya Mtu, Hata Hao Mapapa kina Voda na Tigo waya za watu zilivyo katika na wao Waliathirika, Internet ni muunganiko wa miundombinu ya watu wengi mno.Yaani unatakiwa uwe na nini na nini uwe na uwezo wa kutengeneza Mb zako? Hao wenye miundombinu mikubwa wanafanyaje ili wauze mb? Nadhani mtoa mada anataka aweze kuzitengeneza bila kupitia kwa mtu,au miundombinu ya mtu.
Kwahiyo ukiwa na miundombinu mfano ka mnara na vifaa vingine(intaneti). Je unaweza kutengeneza Mb? Kuwa na ule uwezo wa kampuni kama airtel na Tigo?Naelezea kwa namna nyengine
Internet inafanya kazi kwa mechanism mbili downloading na uploading.
Kuna policies wameziconfigure kwenye vifaa vya mtandao mfano IN (intelligent node) labda mtu akilipa 2000 apewe ruhusa ya kutumia infrastructure kwa siku 7 kwa MB 1000, hii inamaana utaruhusiwa kudownload na kuupload MB1000 ndani ya siku 7
Hivyo MB za kwenye internet ni ruhusa tu ya wewe kutumia infrastructure au miundombinu ya mtandao muda wako ukiisha wanakudisconect.
Au mfano mwengine
Barabarani nimeweka barrier
Nakuruhusu kupitisha magari matano badala ya hapo nafunga barrier
Barabara ni miundombinu ya internet
MB ni magari matano uliyoyavusha kwenye barrier
Internet ni ile ruhusa ya kupita akifunga barrier hakuna internet
Ewaaaa... hapo sasa nimekulewa vyema. Kwahiyo kuna namna nao akina tigo wanalipia waya za watu na wao wakipata huduma zinazotokana na waya hizo wanatuizia sisi,ndio maana bei hazitofautiani sana za vifurushi. Asante sana !Ili usitumie miundombinu ya mtu inabidi usambaze waya mwenyewe dunia nzima. Kama unataka kumtext mtu China uhakikishe waya zako zinatoka Tanzania hadi China, kifupi sio realistic kutotumia miundo mbinu ya Mtu, Hata Hao Mapapa kina Voda na Tigo waya za watu zilivyo katika na wao Waliathirika, Internet ni muunganiko wa miundombinu ya watu wengi mno.
MB ni Si unit ya Data tu, popote pale kwenye kifaa kinachopitisha data kuna MB.Kwahiyo ukiwa na miundombinu mfano ka mnara na vifaa vingine(intaneti). Je unaweza kutengeneza Mb? Kuwa na ule uwezo wa kampuni kama airtel na Tigo?
Je wao kampuni za simu wana miundombinu tu au wanalangua uwezo wa kuchakata mb kupitia hiyo mikongo ya baharini inayozunguka dunia nzima?