MB au data zinatengenezwa wapi?

MB au data zinatengenezwa wapi?

20240607_215631.jpg
 
Habari wanaforums, naomba kujuzwa Data au MB zinatengenezwa wapi, haiwezekani mtu yeyote kitaa akazitengeneza kimagendo?
Bytes (B) au Kilobytes (KB) au Megabytes (MB), au Gigabytes (GB) au Terabytes (TB), n.k ,....... ni memory capacity ya computer au storage device unayotumia kuhifadhi digital data zako, ambazo kawaida huwa zinahifadhiwa zikiwa kwenye form ya zeros na ones

Data hizi zinaweza kuhifadhiwa hata kwenye computer ambayo haiko kwenye intenet, yaani unaweza kuzihifadhi hata kwenye computer yako mwenyewe ambayo haijaunganishwa kwenye internet

Kwa hiyo ieleweke kuwa MB na internet ni vitu viwili tofauti, isispokuwa ukihitaji kutumia internet ndiyo unapimiwa NAFASI YA KUHIFADHIA DATA ZAKO kwa kutumia MB

Nafasi hiyo unayopimiwa ikishajaa, maana yake ni kwamba MB zako zinakuwa zimekwisha

Kwa hiyo inapotokea kuwa umeunganishwa kwenye internet, ina maana kuwa aliyekuunganisha kwenye internet amekupa storage space au memory space kulingana na mahitaji yako

Kwa hiyo kwa maana nyingine ni kwamba MB zinaweza kupatikana kwenye storage devices yoyote hata kama haina internet, na hivyo MB zimekuwepo hata kabla ya internet kuanza

Rasmi intenet ilianza mwaka 1992 lakini MB zilikuwepo hata kabla ya hapo

Wewe unayeandika kitu ndiye unayezitengeneza MB, ihuku computer yenyewe nayo ikiwa imtengenezwa kuzihesabu kwa kutumia utaratbu maalum

Hii text niliyoandika hapa kukujibu swali lako, tayari mimi mwenyewe nimeshatengeneza MB moja au mbili hivi
 
Ni logic questions mb nani anazitengeneza na hii mtandao inanunua mb toka kampuni Fulani au inatengeneza zenyewe kama inatengeneza zenyewe mbona bei zinawiana? Na pia kama wanaweza kutengeneza wenyewe kwanini wasisushe bei za hizo mb kama ushindani wa soko
 
Ni logic questions mb nani anazitengeneza na hii mtandao inanunua mb toka kampuni Fulani au inatengeneza zenyewe kama inatengeneza zenyewe mbona bei zinawiana? Na pia kama wanaweza kutengeneza wenyewe kwanini wasisushe bei za hizo mb kama ushindani wa soko
Mb hazitengenezwi..
 
MB hazitengenezwi

Unapewa access ya kutumia infrastructure za internet katika speed flani

Katika network kuna node au kifaa kina control matumizi ya mtandao wao wanaconfigure labda huyu akilipia 2000/= atumie mtandao kwa siku 7 kwa speed fulani

Inshort ni kitu cha kufikirika sana sana unalipia miundombinu unayoitumia the same applies to vocher za simu
 
Habari wanaforums, naomba kujuzwa Data au MB zinatengenezwa wapi, haiwezekani mtu yeyote kitaa akazitengeneza kimagendo?
Internet ni miundombinu, ukiwa na miundombinu na wewe unaweza uka charge na kuuza hizo mb.

Kuna miundombinu ya ndani nchini na miundombinu mikubwa ya Baharini/Nchi kavu.

So ili na wewe ucharge mb Inatakiwa
1. Utengeneze miundombinu yako
2. Ununue/ukodishe miundombinu ya wenzako.

Mfano kijijini kwenu km kama 10 umepita Mkonga wa Taifa, unaweza ukaenda TTCL ukanunua bandwidth, let's say 10GBps, hio ni capacity yako, halafu wewe mwenyewe ukatengeneza miundombinu yako ukatoa waya kwenye Mkonga mpaka kijijini, pale kijijini ukajenga minara na ili kila mtu apate halafu uka charge kutokana na matumizi.
 
Kwanza la msingi tujue internet ni Nini??

Internet ni mfumo wa Computer, simu au devices nyingineee za umeme zilizounganishwa pamoja..

So kwa tafsiri hiyo,Simu Yangu na computer yako vimeunganishwa kupitia INTERNET,Mimi nahitaji Kutoka kwako File lenye ukubwa wa 1GB,nalipataje??

Wewe unaweza nitumia kupitia Email(mfano),,so unatuma kwenye servers za Gmail file Hilo,Mimi naingia Gmail,napakua Kwenye server Yao..

Internet Service Provider,hawa Tigo,Vodacom,haha ndio wanakuwezesha kufikia HUDUMA hiyo,na sio kwamba wanatengeneza MB,na wanachaji kutokana na ukubwa wa Taarifa utakazo access,wanakupimia kwa kadiri utakavyo lipia..
main-qimg-fc7d3f9e5bf9ef8a308a8a49115298bf-lq.jpeg
 
Zinarudi kwenye saver ndo faida yao
Haziendi sehemu

Mfano wewe umelipia kuangalia mpira mechi dakika 90 ukiondoka dakika ya 60 hizo 30 wanazipeleka wapi? Jibu hawazipeleki sehemu hizo MB ni kitu cha kufikirika zaidi ni ruhusa ya wewe kitumia miundombinu ya mtandao sana sana hicho kiti ulichokaa wewe uwanjani atakuja kukaa mtu mwengine uwanjani wewe unalipia ile siti na kwenye mtandao wewe unalipia ile miundombinu ya mtandao
 
Ni kitu ambacho hakiwezekan!
Ila umeuliza swali la kiufundi kwel 👏👏👏
 
Back
Top Bottom