Mazungumzo yasiyosikika

Mazungumzo yasiyosikika ni asilimia tisini ya mazungumzo yetu yote yanayosikika kila siku katika maisha yetu.

Mazungumzo yasiyosikika ni yale tunayoongea wenyewe kwenye bongo zetu, tunapanga tunapangua tunakumbuka hili tunawaza hili yote haya kimya kimya lakini wakati huo uko unafanya jambo lingine au unasikiliza mazungumzo mengine au unaongea Mko kwenye mkusanyiko wa watu, kanisani, msikitini, kwenye kutano au kwenye chombo cha usafiri kuna wazungumzaji wachache wanaongea mnawasilikiliza kwa makini mko kimya, lakini kiuhalisia kila mmoja yuko busy akilini mwake anaongea yake.

Mazungumzo yasiyosikika ni mengi mno na kama kila mmoja angetaka kuyaongea kwa sauti inayosikika basi dunia ingejaa mwangwi mkubwa mno yani ni kama vile walokole wanaposali kwa sauti.

Daaah!!!
Nimeipenda hii
 
Dah ila kweli kwa nfano ninavyomdanganya msichana laiti kama angesikia na ninachoongea ndani angenikimbiza na makuni esi suni esi posibo.
 
Mazungumzo yasiyosikika ni yale tunayoongea wenyewe kwenye bongo zetu, tunapanga tunapangua tunakumbuka hili tunawaza hili yote haya kimya kimya lakini wakati huo uko unafanya jambo lingine au unasikiliza mazungumzo mengine au unaongea Mko kwenye mkusanyiko wa watu, kanisani, msikitini, kwenye kutano au kwenye chombo cha usafiri kuna wazungumzaji wachache wanaongea mnawasilikiliza kwa makini mko kimya, lakini kiuhalisia kila mmoja yuko busy akilini mwake anaongea yake.

sehemu ya mazungumzo yasiyosikika hutafsiriwa kuwa matendo!

Yasiyosikika (tafakari) - "bungeni kunaendelea nini?".
Matendo - mhusika anawasha redio/tv kusikiliza/kuona komedi za Bunge.
 
Hiyo inaitwa intra-personal communication, speaking with your yourself.

Hapo lazima kuwa na sender, receiver na feedback!

Kikawaida mazungumzo ya hivi huwa yana nguvu sana kuliko yale ya kusikika...

Trust me, wazo la 'ningejua' huwa tayari limeshapatiwa majibu kwa asilimia kubwa sana na intrapersonal comm, basi tu ni kutotii mawazo ya ndai kwa ndani!

Sensorsecurityservices
 
Daaah! Itokee mtu amenikera anavyoendelea kuongea me kimya ila majibu nayompa ambayo hayasikii angesikia anaweza asiamini km ni mimi naemjibu akaishia kupata pressure na nilivyo naonekana mpole
 
Yani sijui ingekuwaje kama ingekuwa tunawaza kwa sauti
Pasingetosha mkuu, ingekuwa kitim tim halafu tusingesikilizana, sidhani kama kuna binadamu anaekosa kuwaza, ujue hapo ni lazima. Kuwaza sio mabaya au hali ngumu tu kuna kuwaza maendeleo, mipango ijayo, mafaniko n.k.

Kwa kweli pasingetosha mkuu
 
Hebu pata picha hii umemdate mtu mmeenda vizuri sana mpaka ikafika siku ya siku! Unakuwa na hamu naye kweli mnapanda kitandani unamaliza ufundi wako wote halafu mwenzako yuko kimya baridi kabisa unafikiri anawaza nini kwa wakati ule? Hawezi kuwa mkweli kukwambia aslani

Anakuwa anafikiria ni kwa jinsi gani usivyojua mapenz!!
 
Na ndio maana watu wakimya wanaogopeka mno kwakuwa mazungumzo yao yasiyosikika ni mengi zaidi na ngumu kuweza kuhisi kuwa anawaza nini
 
Mfano halisi ni wa hivi karibuni kwenye medani za siasa mgombea mmojawapo EL baada ya kukatwa jina lake amekuwa kimya kabisa watu ndio wanamsemea na kumuwekea maneno lakini unafikiri kakaa kimya na haongei kimyakimya?
Anaongea sana tena mengi sana within himself lakini bahati mbaya hayasikiki, hayaongei kwa sauti ndio maaana tunasema yupo kimya
 
Mazungumzo ya kimyakimya ndo ya kweli kuliko yanayosikika, maana heart/soul hauna unafiki hata chembe! Pale binadamu anapoanza kutaka kutamka jambo basi na uwongo hujitengeneza hapohapo/ Mtu unaanza kupigwa sound!
 
Last edited by a moderator:
hivi hamna njia ya kufanya haya mazungumzo ya kimya kimya yakapungua wakati huyahitaji..mfano mwanafunz yupo class unakuta wakat wa somo haya mazungumzo ya kimya kimya yamemtawala..hii inapoteza umakin wa masomo

Kikwao inaitwa lack of concentration, wale wanaofanya meditation wanalijua vizuri hili yaani unapoanza tu kumakinika akilini inakuja live stream ya matukio, mipango na changamoto mbalimbali kichwani...unajikurupusha na kurudi kwenye umakini lakini mara yanakuja mengine.... Kuna watu hufikia kutoka jasho kwa ajili ya kupambana na hii hali
 
Mazungumzo ya kimyakimya ndo ya kweli kuliko yanayosikika, maana heart/soul hauna unafiki hata chembe! Pale binadamu anapoanza kutaka kutamka jambo basi na uwongo hujitengeneza hapohapo/ Mtu unaanza kupigwa sound!

Kilichomo mawazoni ndio halisi, kizungumzwacho kwa sauti kimechakachuliwa kukidhi mahitaji ya wakati na mazingira husika
 
Kikwao inaitwa lack of concentration, wale wanaofanya meditation wanalijua vizuri hili yaani unapoanza tu kumakinika akilini inakuja live stream ya matukio, mipango na changamoto mbalimbali kichwani...unajikurupusha na kurudi kwenye umakini lakini mara yanakuja mengine.... Kuna watu hufikia kutoka jasho kwa ajili ya kupambana na hii hali
ila mhh mi hii hali ianitokeaga sana nikiwa ibadani yaan unakuta mawazo yamehama..nikisikia amen duh nashtuka narud kwenye kusikiliza..!ila unakuta mambo mengi yameshanipita
 
Na pia kuna mawasiliano yasiyosikika kati ya mtu na mtu,mfano unamkumbuka mtu aliye mbali mkoa mwingine kuwa utampigia simu badae kidogo kabla ya we kupiga unashangaa anakupigia. Pia inatokea mtu unampenda(sio kimapenzi) tu bila kuwa na sababu maalum unashangaa na yeye anakupokea vizuri kama vile alijua nn unawaza,mwingine humpendi tu bila sababu na yeye akikuona tu anakunja sura na hujamwambia chochote kibaya
 
ila mhh mi hii hali ianitokeaga sana nikiwa ibadani yaan unakuta mawazo yamehama..nikisikia amen duh nashtuka narud kwenye kusikiliza..!ila unakuta mambo mengi yameshanipita

Sio wewe tu hata yule anayeongoza ibada kuna wakati unaona kabisa anafanya kwa mazoea lakini akili yake inawaza mengine kabisa
Kitu cha kushangaza kuhusu mind ni kwamba ina uwezo wa kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja,kwa mfano unaandika kitu hapa lakini wakati huohuo unafikiri mengine kabisa na vyote vinaenda kwa pamoja
Ndani ya meditation tunaita scattered/wondering mind....na lengo kuu la meditation ni kuirudisha hiyo mind na kuwa kitu kimoja, ikifanya jambo moja bila interference ya kingine chochote
Wanasema settled and focused mind is lethal because can see beyond this moment
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom