Mazungumzo yasiyosikika

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,675
698,670
Mazungumzo yasiyosikika ni asilimia tisini ya mazungumzo yetu yote yanayosikika kila siku katika maisha yetu.

Mazungumzo yasiyosikika ni yale tunayoongea wenyewe kwenye bongo zetu, tunapanga tunapangua tunakumbuka hili tunawaza hili yote haya kimya kimya lakini wakati huo uko unafanya jambo lingine au unasikiliza mazungumzo mengine au unaongea Mko kwenye mkusanyiko wa watu, kanisani, msikitini, kwenye kutano au kwenye chombo cha usafiri kuna wazungumzaji wachache wanaongea mnawasilikiliza kwa makini mko kimya, lakini kiuhalisia kila mmoja yuko busy akilini mwake anaongea yake.

Mazungumzo yasiyosikika ni mengi mno na kama kila mmoja angetaka kuyaongea kwa sauti inayosikika basi dunia ingejaa mwangwi mkubwa mno yani ni kama vile walokole wanaposali kwa sauti.
 
Very truthful...si tu yangeleta mwangwi bali mengine yangezua ugomvi kati ya mtu na mtu.Waliosema"some things are rather left untold" vikiongewa vyote mwanadamu anavyovizungumza ndani..Balaa


Just imagine Boss akimgombeza mfanyakazi wake aliye kimywa, unajua anamjibu au kumtukana kiasi gano wakat huo??

Ama mzazi anapimgombeza mtoto laiti kama yale mazungumzo yangefunuliwa pasingekalika!
 
tena mazungumzo yasiyo sikika asilimia kubwa ni negative.... matusi, kejeli, dharau, laana, masengenyo, malalamiko

Hebu pata picha hii umemdate mtu mmeenda vizuri sana mpaka ikafika siku ya siku! Unakuwa na hamu naye kweli mnapanda kitandani unamaliza ufundi wako wote halafu mwenzako yuko kimya baridi kabisa unafikiri anawaza nini kwa wakati ule? Hawezi kuwa mkweli kukwambia aslani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom