Mazungumzo na Dr. Slaa: Maswali na Majibu

Mazungumzo na Dr. Slaa: Maswali na Majibu

Status
Not open for further replies.
- Inategemea sheria inasema nini wewe na mimi, yaani wananchi wa kawaida tunatakiwa kutibiwa wapi, lakini ninaamini kwamba sheria iko wazi kuhusu viongozi wa juu! sio kosa langu kuhusu hiyo sheria, hata mimi nikiumwa ninatibiwa Muhimbili kama wananchi wengine!

- Huo utetezi wako wa DR. Slaa kutokulipa kodi ni upuuzi sana!



Willie @ NYC, USA.

hakuna sheria inayozuia mwananchi (bila kijali cheo) kutibiwa nje ya nchi tena kwa ghalama ya serikali kama wataalamu wakisha sema hivyo kutoka na kukosa uwezo wa kumtibu hapa nchi ila tatizo ni kwamba serikali itasema haina pesa.
ila wao wakiumwa hata kichwa kwa sababu ya kutokunywa maji au jua kali wanakwenda kutibiwa nje.
tuweke siasa pembeni kidogo kuvuia matibabu ya mtu ni sawa na kuua, ndio maana kuna watoto na watu wenye magonjwa ya moyo wako kwenye waiting list ya kwenda india TATIZO ni pesa kutoka serikalini.
kwa viongozi wa serikali na walikuwa viongozi wa serikali kutibiwa nje sio matakwa ya wataalum mara nyingi ni mashinikizo ya kisiasa/ubinafsi.
ndio maana Kitine kwa kutumia udhaifu huo wa sheria aliweza kututoa milioni Hamsini kwa matibabu ya mke wake huko USA lakini baadaye kila kitu ilijulikana ni fake mpaka dr waliyesema amemtibu huyo mama alikuwa sio dr ila mwanafunzi katika hicho chuo.
sasa kama wataalamu wanatoa maamuzi hapo ilikuwaje.
mimi nadhani hawa viongozi wakijisikia tu wanakamata pipa na kwenda zao kutibiwa si bajeti hipo

Ndugu Willie nina swali kwako, mzee alilipiwa na nani tiketi ya kwenda kutibiwa?
ilikuwaje anakuja USA hali alikuwa na safari ya kutibiwa india ACCOUNT zinasemaje hapo
kama mzee afya yake ilikuwa mbaya kiasi cha kwanda kutibiwa india nguvu za kuja kula bata hapo USA kazipata wapi?
TUWE WAZALENDO KWA TAIFA
 
Duuuh, hivi wakubwa huyu WJ Malecela ni kijana wa Mh. Malecela yule aliyekuwa Waziri wetu mkuu mstaarabu, mwenye busara, hekima na kujua kujibu hoja!!!??? Mbona sasa huyu anaonekana hayuko makini/serious ktk kujibu au kuuliza swali, au nduio kusema ni hulka kuwa hata iweje nae atakuwa kiongozi wa taifa letu kama mzee wake? kwa majibu haya na maswali haya kweli? Mi mgeni, nauliza tu!
nani kakwambia Malecela alikuwa na busara ya kujibu hoja?
 
Napotosha kivipi mkuu?,Huyu Binti Jenifa alianzisha thread ikiwa na heading Dr. Slaa kapotelea wapi?



na kwa bahati nzuri Dr.Slaa alijitokeza na kuanza kumjibu kabla ya Malaria Sugu,Ritz,Mdondoaji na FaizaFoxy hawajaja na maswali yao yanayohusiana na mambo ya udini ikiwemo mahakama ya kadhi(sijaona Jenifa akipost ishu yoyote ya udini)......Baadaye mods walibadilisha title ya thread na kuwa 'Mazungumzo na Dr. Slaa: Maswali na majibu' ambapo post za udini ziliendelea kuingia mpaka tukafika page ya 9 kama sio ya 10 kabla Silencer hajaziondoa na kutoa onyo tukafika......Na baada ya post za udini kuongezeka niliweka post hii



Baada ya hapo nilimtaka Dr.Slaa ajibu maswali ya baadhi ya watu baada ya kuona heading imebadilishwa(nijuavyo mimi mods pekee ndio wanaweza kubadilisha heading na si member,) nikadhani labda wameibadilisha baada ya kuwasiliana na Dr. Slaa ili thread hii iwe maalum kwa yeye kuongea na wana JF kwa njia ya maswali na majibu.....




Sasa upotoshaji sijui unatoka wapi hapa............Halafu kwa nini umsemee Dr.Slaa wakati yeye mwenyewe yuko online humu na alianza kuijibu hiyo thread unayoisema inamkejeli kabla hata haijabadilishwa heading.......
Bala nakuhakikishia kichwa changu mimi kina Hansard, hiyo thread ameifanyia editing Jenifer, kumbuka sio kila editing ni lazima ioneshe neno Last edited.
Hiyo thread ilikuwa inaanza kwa maneno ya kejeli kumuita Dr Slaa ni Dr wa wakatoliki. mimi nadhani nilikuwa mmoja wa watu wa mwanzoni kabisa kuingia ndani ya thread hii. huu ndio ukweli ninaokuhakikishia. hii thread ilikuja kwa njia za kejeli na muda huo huo, huyu huyu Jenifer akaazisha tena thread nyingine ya uchokozi hana lolote huyu Jenifer. (Jenifer? )

Niko makini sana mkuu kuliko unavyoweza kudhania, na always watu wakiwa serious kuzama kwenye topic bila kuleta mizaha na kejeri hapo utanipenda material nitakayoshusha, lakini mtu akianza matango pori atakimbia yeye.
Jiulize mbona tangu Silencer azifute zile post za kipuuzi kwa nini humuoni hapa Faiza Foxy, Ritz, Mdondoaji na wale wote ambao kazi yao ni kuharibu mijadala?
Hapa ndio ninapata ushahidi kwamba huu upumbavu unaoendelea hapaJF unashabikiwa na Mods, kama leo wameweza kufanya kazi nzuri namna hii kwa kufuata post nyingi zaidi ya page 5 kwa nini siku nyingine wanaacha wapuuzi ambao hawazidi 10 kupandikiza chuki? au kwa sababu Dr Slaa alikuwa online wakajifanya kumuonesha kwamba wapo makini? i don't understand this!
 
- Kabla ya kumuita fisadi tumpe nafasi ya kujieleza kwanza si yupo? Aje ajibu mwenyewe na ningependa kujua zile Shilingi Billioni 450 ambazo Chadema wamedai ziongezwe kwenye bajeti, walitegemea zitoke wapi? Mbona hawakusema?

- Na klwa nini ukusanyaji kodi sio agenda ya Chadema?


Willie @ NYC, USA.
Tafadhali uwe na heshima hata kidogo kwa Mh. Dr Slaa hata kama unamuuliza swali si kuanza hivyo--Kabla ya kumuita fisadi----aje ajibu,
huo si ustaarabu hata kidogo, Dr Slaa ni kiongozi wa Kitaifa halafu ni mtu mzima kwa umri kukuzidi wewe tumpe heshima yake.

Kuna post za kina MS zilikuwa hazina heshima kama hizi zote zimefutwa kwa hiyo usije sababisha tena thread hii kufutwa kwa sababu kuna wengine hawatakubali kiongozi wao kudhalilishwa kwa maswali ya kejeli nao watakujibu kwa kejeli.
 
ee Lwakatare nae yuko online ana2pia macho...
Au macho yangu! Slaa no longer on air,chaji itakua imekwisha kama alivyosema acha apumzike ajiandae na cku nyingine ya ukombozi wa taifa hili,wanaharakati bado 2po by the way...
 
bot_tabimg.gif


[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"] Dk Slaa amvaa IGP Mwema [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

eeslaa.jpg
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa

Geofrey Nyang'oro na Elizabeth Ernest, Kisarawe
KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa amelitaka Jeshi la polisi nchini kutoingilia masuala ya vyama vya siasa kwa kuwa kufanya hivyo ni kukiuka wajibu wake.

Kadhalika Dk alisitiza kuwa Chadema wataendeleza maandamano kudai haki za raia na kwamba kamwe hawatalala na kwamba kinachoweza kuwanyamazisha ni iwapo serikali ya CCM na Polisi watatekeleza wajibu wao kwa kuondoa kero za wananchi na ikiwa ni pamoja na kuwafikisha watuhumiwa wote wa ufisadi mahakamani.

"Sisi Chadema tunalitimiza hilo kwa vitendo na kamwe hatutalala na wala hatuogopi polisi, tutaendelea kutimiza wajibu wetu, kama serikali ya CCM na Jeshi la Polisi wanataka Slaa anyamaze, watekeleze wajibu wao kwa kuondoa kero za wananchi na kuwafikisha watuhumiwa wote wa ufisadi mahakamani,"alisema.

Dk Slaa ambaye alikuwa akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kisarawe Mkoani Pwani, alisema kazi ya polisi si kutisha na kuzuia kazi ya vyama vya siasa bali ni kulinda raia na mali zake.

"Polisi na usalama wa Taifa mpo nataka mumpelekee taarifa IGP Mwema kuwa kazi ya polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao, hawa ni watumishi wa wananchi na si mabosi wao, siyo hizi za kujiingiza kwenye masuala ya kisiasa na kusahau majukumu yenu,"alisema Slaa na kuongeza

"Mwambieni Mwema kama hawezi avue magwanda apande majukwaani ili tupambane kwa hoja, vitisho mnavyovifanya mtawafanyia hao wasiojua haki zao lakini sio mimi Dk Slaa ambaye nazijua sheria na haki zangu za msingi,"alisema.

Alisema kuzuia shughuli za vyama vya siasa kwa kisingizio cha kuhatarisha amani na utulivu si kwamba ni kinyume na katiba tu bali pia ni ukandamizaji wa maksudi wa demokrasia.

Maandamano na mikutano
Slaa katika mkutano huo alitetea maandamano na mikutano inayofanywa na chama chake kuwa siyo chanzo cha kutoweka kwa amani hapa nchini, bali Chadema wanatimiza wajibu wao wa kikatiba na kwamba "amani inalindwa na haki dhidi ya wananchi wote".

"Polisi mpo,….. naomba mpige picha na mnakili hili vizuri na kumfikishia IGP Mwema; ghasia katika nchi yoyote haitokani na maandamano bali inatokana na kukiukwa kwa haki, kama wananchi hawapati haki zao za msingi hiyo siyo amani na utulivu tunayoihubiri,"alisema Slaa.

Slaa alitetea maandamano na mikutano inayofanywa na chama chake inalenga kuamsha uelewa wa wananchi na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo, Chadema wanatimiza wajibu wa msingi kama chama cha siasa kwa mjibu wa katiba.

"Naomba niwaambie Polisi, kazi ya chama cha upinzani si kupigia makofi serikali iliyoko madarakani, bali ni kuikosoa na kuwaleleza wananchi juu ya kushindwa kwake kutatua kero za wananchi ili unapofika uchaguzi wananchi kwa pamoja wachukue hatua kwa kukiondosha madarakani kwa njia ya kura,"alisema Slaa.
Upotevu wa fedha
Katika mkutano huo Slaa alidai kuwa tangu Tanzania ipate uhuru 1961 hadi June 30 mwaka jana, ilikuwa imepoteza Sh 1.3 trilioni sawa na asilimi 10 ya pato la Taifa kwa matumizi yasiyofahamika.

Alisema fedha hizo ambazo zimeishia mikononi mwa watu wachache zingeweza kujenga barabara za lami kilomita 500.

"Tulipoanza kuzungumza kuhusu EPA (Fedha za kulipa madeni ya nje), Kikwete (Rais Jakaya) alisema kelele za akina Slaa hazininyimi usingizi lakini leo hii halali usingizi kwasababu ya EPA,"alisema Slaa.

Alisema Chadema kitaendelea kupiga kelele hadi watuhumiwa wote wa mali za umma watakapokamatwa na kufilisiwa kwa fedha zao kurejeshwa ili zitumike kujenga shule na Zahanati kwa ajili ya Watanzania.

Kauli ya Mpendazoe
Naye kada maarufu wa Chadema, Fred Mpendazoe aliwataka wakazi wa Kisarawe kubadilika na kukihama CCM kwa maelezo kwamba chama hicho kimetengeneza matabaka ya masikini na majiri.

Alisema wakati wa utawala wa Rais wa kwanza, Hayati Julius Nyerere, CCM ilisimamia haki kwa wote, matajiri na maskini hivyo kujenga heshima ya Watanzania ndani na nje ya nchi.

"Wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere maadili ya uongozi yalizingatiwa, mtu aliyetaka kugombea aliulizwa fedha amezipata wapi, lakini leo uongozi ndani ya CCM ni biashara na mtu akitaka kugombea nafasi yoyote anaulizwa una shilingi ngapi?"alisema Mpendazoe.

Alisema viongozi wa aina hiyo hawawezi kuhoji sababu za umasikini wa wananchi na badala yake wanawaza jinsi ya kurejesha fedha walizotumia kwenye kampeni.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
- Ndio maana nimesema wote huenda hawatufai, maana wote hawathamini ukusanyaji kodi, Wewe unasema nini kuhusu kodi kutokusanywa? Halafu vipi wewe ni msemaji wa Slaa?

Willie @ NYC, USA.
Shida ya kukusanya kodi ni ya kimfumo tu. Imeshapigiwa kelele sana na inaelekea viongozi wetu hawaoni haja ya mabadiliko.
William, hata enzi za baba yako akiwa waziri mkubwa shida hii ilikuwepo. Nakumbuka ilibidi hata Nyerere aipigie kelele maana serikali ilifikia mahali pa kutangaza kuwa imefirlsika, na hapo ndio wazo la kuzaliwa tra lilipoasisiwa.
 
Duuuh, hivi wakubwa huyu WJ Malecela ni kijana wa Mh. Malecela yule aliyekuwa Waziri wetu mkuu mstaarabu, mwenye busara, hekima na kujua kujibu hoja!!!??? Mbona sasa huyu anaonekana hayuko makini/serious ktk kujibu au kuuliza swali, au nduio kusema ni hulka kuwa hata iweje nae atakuwa kiongozi wa taifa letu kama mzee wake? kwa majibu haya na maswali haya kweli? Mi mgeni, nauliza tu!
Angalia majibu yake akizidiwa hoja utasikia anasema watu wameanza matusi.
- Lakini mbona kichwa chako ni pumba tupu halafu unajivua nguo mwenyewe, swali anaulizwa Slaa wewe vipi mkuu huoni ndio kichwa mbuzi sana hicho? ha! ha! vipi Slaa amekuomba umjibie? ha! ha! ha!

Willie @ NYC, USA.

- Unajua ni mtu mpumbavu ndio hujfanya anajua sana kama wewe na uchungaji wako mbuzi sana,Willie @ NYC, USA.
 
........................................
BTW huna hekima kama babako Mzee Malecela miaka yoote aliyokuwa madarakani hasa alipokuwa Waziri Mkuu ameshindwa hata kujenga hospitali ya maana Dodoma mji Mkuu wa Tanzania!

Mbona nyerere kawa rais miaka kibao huzi tu tunasikia mbunge analilia hospitali.

jamani tafuteni hoja zenye kueleweka Kiongozi wa kitaifa hapimwi au hachekwi kwa kupeleka au kutopeleka maedeleo fulani wilayani au mkoani kwake.

Ukianza kumlaumu Waziri mkuu wa dodoma kushindwa kujenga hosptali dodoma sasa kwa nini vingzoi wenginewalaumiwe ni wadini au wakabila ??????? Kama unamlaumu Malechela waushindwa kujenga hospitali dodoma je unawea kumsifia kikwete kwa kuwezesha uwekezaji Pwani?

Malechela ni PM mstaafu sio yeye wapo wengi kina msuya warioba na hata Lowasa( naye ni mstaafu) Stahiki zaonyingi hata akiugua mafua anawezo wa kwenda nje Dakatari binafsi. Atleast safari mbili nje ya nchi kila mwaka. Hizi na nyingine nyingi ni stahiki zao na wanazidi kuziboresha. teh teh teh teh

Laikini katika kukosoea tukosoe sera sio attack ya mtu


BTN

Na wewe William@ newyork usifanye maigizo ya ujidai huelewi kero na hasira za watanzania. kama unavyosema na wew tofauti na mzazi wako e ulikuwa unaiabiwa muhimbili kama watanzani wengine basi unatakiwa kuelewa malamiko ya wengi sabbau muhimbili unapajua.Otheiwise hata huko muhimbili card yako ya wagonjwa ilikuwa ni VIP.

Ni hivi huwezi ok Tuseme basi kwa raisi na waiziri mkuu ni sawa. Hivi utakuwaje na wabunge wanaotetea sera ya afya bora kama wao wanajua wkaiugua ugonjwa wa moyo stahiki yao ni india lakini mpiga kura wake akigua moyo 1 kati ya kumi ataiona muhimili kwa shida.

kuonyesha responsibility tunataka tupange na wabunge foleni muhimbili bugando na KCMC ili watuwakilishe vizuri.

Watu sio wajinga kuhoji au kuchukia mawaziri utumia VX from masaki to posta. Yyete mwenye kudadisi anaweza kuelewa kwa nini watu wana hasira na na huo wivu. Sasa ni juu ya vingozi wanaosoma nyaati kuyafnyia kazi na wale wegine kuendela na kasumba ya ni mambo ya kisheria.

Pinda mwenyewe juzi kawa mpole kuhusu posho japo ameongea lugha watu waliyotaka kusikia badala ya kuendelea kubisha. Japo naona lugha za watu wengine sio nzuri niadhani ni sababu na wewe unajifanya huelewi ........


Nawasilisha
 
Mods naomba ili hii Topic isiwe closed anzeni kumark ni nani huwa wanaaza chokochoko hivi nilipomuwekea RED huyu ndugu kuna Dr WA uaskofudunia hii? kama kawaida hapa ni za uso tu ukija na kejeri utakimbiwa mwenyewe, nyumbani kwangu nina libraly ya kejeli zote.
Sijavunja sheria yeyote ana PhD ya Divinity (Theology) ni kitu gani??? Endelea kumark vizuri
 
Nina maswali magumu ya kumuuliza.

tafadhali baba rudi jf tujadili ile posho kubwa ya milioni 7.5

ninayo maswali mengine kuhusu mchumba wako wa kudumu kuwatumia waheshimiwa sms za mipasho.

maswali mengine yanahusu demokrasia finyu ndani ya chama chako. eti diwani wa arusha hawezi kuamua kitu mpaka lichama kule nyumbani kwa mtei liseme yeah!
Hovyo! Au ndiyo kufilisika huko. Hivi hakuna masuala "serious" kwa taifa yanayofaa kujadiliwa hadi kubangaiza na kujadili personalities? Ama kweli shida haina adabu, naona mmeshikwa pabaya sasa mnahunyahunya.
Posho anayoipata Dr. Slaa ina maslahi gani kwa taifa au hata sms za mipasho! Leteni national issues na si personal. Kwa nini tumjadili Slaa na kumwacha JK anayefuja mamia ya mamilioni kwa kwenda kuzurura na kupeleka watoto, wakwe na wajukuu zake majuu kutalii kwa gharama za sisi walalahoi? halafu ni aibu kwa mbunge msomi kupeleka umbeya mpaka kwenye bunge! baada ya kulihujumu taifa kwa kushiriki katika mkataba unaoifilisi nchi wa IPPTL mbunge huyu aliyetumia kikamilifu ngawira za rushwa kuikwaa nafasi hiyo sasa anaonyesha dalili za kuvimbiwa sumu ya ufisadi na kusahau kujadili masuala ya kitaifa bungeni, badala yake anapeleka mpaka bungeni ushambenga wa mitaani!
Ni demokrasia gani mnayotaka CHADEMA waifuate? hiyo ya kwenu ya kututengenezea maspika vibaraka kwa kumwondoa mwenye msimamo wa kulinda maslahi ya nchi? Au hiyo ya kwenu ya kutangaza kuwavua magamba ya chokaa wenzenu, tmkiyaacha ya kwenu ya chuma? Au ile ya kuwabagua watanzania wenzenu kwa misingi ya ukabila, imani na hata rangi kama mlivyofanya kwa Salim Ahmed Salim, Bashe na wengine kibao ili mtawale?
Kwetu sisi Dr. Slaa ni mtetezi wa wanyonge, mwenye uchungu na nchi hii ambaye hata mkifanya kampeni uchi kwenye masunagogi yenu ya kishetani kamwe hamtafaulu kutudanganya.
Historia itawahukumu. Laana ya mwasisi wenu iwatafune, iwaangamize na kuwasukuma Jehenam.
 
Mods naomba ili hii Topic isiwe closed anzeni kumark ni nani huwa wanaaza chokochoko hivi hapo nilipomuwekea RED huyu ndugu kuna Dr wa uaskofu dunia hii? kama kawaida hapa ni za uso tu ukija na kejeri utakimbia mwenyewe, nyumbani kwangu nina libraly ya kejeli zote.

Islam ubwabwa hao wala usiwaogope!
 
Mods naomba ili hii Topic isiwe closed anzeni kumark ni nani huwa wanaaza chokochoko hivi hapo nilipomuwekea RED huyu ndugu kuna Dr wa uaskofu dunia hii? kama kawaida hapa ni za uso tu ukija na kejeri utakimbia mwenyewe, nyumbani kwangu nina libraly ya kejeli zote.
anataka fananisha na yule Dokta wa kupewa yule,sasa hivi hana hata mda wa kuckiliza shida zao yuko nje cjui hata anafanya nini! Au kafata net zingine?
 
Islam ubwabwa hao wala usiwaogope?
Hivi ndio maana nilimsindikiza rafiki yangu kwenye ile minuso ya kwenye mkeka nikasikia kule kanzu wanataka wali mweupe, baada ya kudadisi kwa nini hawapendi pilau jibu lake liliniacha sina mbavu, eti pilau unashiba haraka! kwahiyo wao wanataka wale sinia 1 watu wawili, ulafi mwingine huu!......
 
Nimekuwa nikifuatilia thread hii toka jana bila kumng'unya maneno thread hii itaharibiwa na watu hawa

1. W.J.Malecela- atasababisha topic ibadilike watu wataanza ku discuss Malecela matters.
2. Mdondoaji- atasababisha watu wahame kwenye mada iliyopo waanze ku discuss udini na dini za watu.

Kwa hiyo nawashauri Mods kuwa waangalifu ili topic isitoke nje ya mada.
 
Bala nakuhakikishia kichwa changu mimi kina Hansard, hiyo thread ameifanyia editing Jenifer, kumbuka sio kila editing ni lazima ioneshe neno Last edited.Hiyo thread ilikuwa inaanza kwa maneno ya kejeli kumuita Dr Slaa ni Dr wa wakatoliki. mimi nadhani nilikuwa mmoja wa watu wa mwanzoni kabisa kuingia ndani ya thread hii. huu ndio ukweli ninaokuhakikishia. hii thread ilikuja kwa njia za kejeli na muda huo huo, huyu huyu Jenifer akaazisha tena thread nyingine ya uchokozi hana lolote huyu Jenifer. (Jenifer? )Niko makini sana mkuu kuliko unavyoweza kudhania, na always watu wakiwa serious kuzama kwenye topic bila kuleta mizaha na kejeri hapo utanipenda material nitakayoshusha, lakini mtu akianza matango pori atakimbia yeye.Jiulize mbona tangu Silencer azifute zile post za kipuuzi kwa nini humuoni hapa Faiza Foxy, Ritz, Mdondoaji na wale wote ambao kazi yao ni kuharibu mijadala?Hapa ndio ninapata ushahidi kwamba huu upumbavu unaoendelea hapaJF unashabikiwa na Mods, kama leo wameweza kufanya kazi nzuri namna hii kwa kufuata post nyingi zaidi ya page 5 kwa nini siku nyingine wanaacha wapuuzi ambao hawazidi 10 kupandikiza chuki? au kwa sababu Dr Slaa alikuwa online wakajifanya kumuonesha kwamba wapo makini? i don't understand this!
Naona hatuelewani mkuu wangu.....Najua uko makini sana hilo sipingani nawe....Tatizo ni kwamba haujataka kunielewa.....Nilichosema mimi ni kwamba tumuache Dr. Slaa ajibu maswali anayoulizwa humu likiwemo hilo swali alilouliza Jenifer la kuhusiana na kodi,mwanzo kabisa Dr.Slaa alimjibu Jenifer lakini Jenifer akamuuliza tena na tangu wakati huo Dr.Slaa hakujibu kitu japo alikuwa akionekana online...Kuhusu kuhariri thread(editing) napo nadhani hatujaelewana,ni kweli unaweza kuedit yaliyomo ndani ya thread lakini hauwezi kuedit heading ya thread(sijui kwa premium members) ndio maana nikasema itakuwa ni mods(Silencer?) ndio wamebadilisha heading ya thread......Hebu jaribu kutafuta thread yoyote uliyoianzisha wewe kisha ujaribu kuedit heading ya hiyo thread kama utaweza....... Btw....Jenifer aliuliza hivi....
Dr. Slaa kapotelea wapi? Nina maswali magumu ya kumuuliza.tafadhali baba rudi jf tujadili ile posho kubwa ya milioni 7.5ninayo maswali mengine kuhusu mchumba wako wa kudumu kuwatumia waheshimiwa sms za mipasho.maswali mengine yanahusu demokrasia finyu ndani ya chama chako. eti diwani wa arusha hawezi kuamua kitu mpaka lichama kule nyumbani kwa mtei liseme yeah!
Na Dr.Slaa akamjibu hivi......
WanaJF,Naamini hamjambo. Msiwe na wasiwasi, nimejaa tele vijijini. Kazi kawaida ya Chadema mapambano yanaendelea Bungeni, na Slaa anaendelea kujenga Chama. Wiki hii nilikuwa Wilaya ya Kisarawe, na tumefanya mikutano mikubwa Chole, Maneromango na jana tumehitimisha Kisarawe mjini. Kazi yetu kubwa ni kuwaelimisha watanzania, kuwaamsha wajue majukumu yao katika kulinda rasilimali zao, kuwasaidia kwanini tuko kwenye harakati za ukombozi wa mara ya pili, ambao kimsingi ni mgumu kuliko kazi ya kumwondoa mkoloni. Hii ndiyo kazi ya Dr Slaa na Sekretariat yake. Time is money hatuna muda wa kupuuza kujibu maswali yasiyo na tija kwa Mtanzania. Kama ni posho na mishahara ya Dr Slaa hata Kisarawe wametuelewa. Wamejua jinsi TRA ilivyo wazembe wameikimbia Chadema baada ya kuja kwa mbwembwe, na leo washindwa kwa aibu kwa kuwa tumewaonyesha ukwepaji mkubwa ulioko serikalini ni aibu tupu. Kama rafiki yangu anahitaji kufahamu naomba afuatane nasi ziara ijayo vijijini.Kama yuko mwenye maswali yenye tija kwa Taifa hili, pamoja na shughuli nyinmgi, pamoja na ukosefu wa umeme niko tayari kuyajibu. Lakini yenye tija kwa Mtanzania siyo ya kujifurahisha.
Na kabla Dr. Slaa hajamjibu Jenifer,Jenifer aliweka post hii(ambayo nadhani ndiyo unadai alikejeli Dr.Slaa),
There are currently 9 users browsing this thread. (6 members and 3 guests)Jenifa,mshikachuma,Rigo.Dr.W.Slaa,Mzito Kabwela,Mwera
naona daktari wa wakatoliki slaa anachungulia. shikamoo baba.nitashukuru ukijibu maswali yangu.
ila post ya kwanza ilikuwa kama ilivyo,haikubadiliaka.....Kilichobadilika ni heading tu............
 
hahahaaa..dk hakuna hajaya kuja.SAIGONI keshawakamata wote humu..ulizeni maswali pls
 
Kwanza wewe sio Dr Slaa usimjibie on his behalf.

Pili nina haki kama mpiga kura kumuuliza hayo masuala kwasababu mimi ndiye nayemwajiri rais wa Tanzania umenifahamu hilo. Usimjibie Dr Slaa tafadhali tusitoke nje ya mada.
kamlete kikwete
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom