Mazungumzo na Dr. Slaa: Maswali na Majibu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mazungumzo na Dr. Slaa: Maswali na Majibu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jenifa, Jul 3, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  Nina maswali magumu ya kumuuliza.

  tafadhali baba rudi jf tujadili ile posho kubwa ya milioni 7.5

  ninayo maswali mengine kuhusu mchumba wako wa kudumu kuwatumia waheshimiwa sms za mipasho.

  maswali mengine yanahusu demokrasia finyu ndani ya chama chako. eti diwani wa arusha hawezi kuamua kitu mpaka lichama kule nyumbani kwa mtei liseme yeah!
   
 2. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kazi kweli...
   
 4. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #4
  Jul 3, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  WanaJF,

  Naamini hamjambo. Msiwe na wasiwasi, nimejaa tele vijijini. Kazi kawaida ya Chadema mapambano yanaendelea Bungeni, na Slaa anaendelea kujenga Chama. Wiki hii nilikuwa Wilaya ya Kisarawe, na tumefanya mikutano mikubwa Chole, Maneromango na jana tumehitimisha Kisarawe mjini.

  Kazi yetu kubwa ni kuwaelimisha watanzania, kuwaamsha wajue majukumu yao katika kulinda rasilimali zao, kuwasaidia kwanini tuko kwenye harakati za ukombozi wa mara ya pili, ambao kimsingi ni mgumu kuliko kazi ya kumwondoa mkoloni. Hii ndiyo kazi ya Dr Slaa na Sekretariat yake. Time is money hatuna muda wa kupuuza kujibu maswali yasiyo na tija kwa Mtanzania.

  Kama ni posho na mishahara ya Dr Slaa hata Kisarawe wametuelewa. Wamejua jinsi TRA ilivyo wazembe wameikimbia Chadema baada ya kuja kwa mbwembwe, na leo washindwa kwa aibu kwa kuwa tumewaonyesha ukwepaji mkubwa ulioko serikalini ni aibu tupu. Kama rafiki yangu anahitaji kufahamu naomba afuatane nasi ziara ijayo vijijini.

  Kama yuko mwenye maswali yenye tija kwa Taifa hili, pamoja na shughuli nyinmgi, pamoja na ukosefu wa umeme niko tayari kuyajibu. Lakini yenye tija kwa Mtanzania siyo ya kujifurahisha.   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Dr Slaa una majukumu mazito kwa Taifa, sitegemei kama utajibu hawa waandishi wa magazeti ya udaku, hapa nategemea utueleze ni lini huyu Mamluki Shibuda mtamuondoa ndani ya chama, hafai hata kidogo.
  Kumbuka ukiona mtu hata ccm hawamtaki basi juwa huo ni mzigo usiobebeka.
   
 6. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  daktari shikamoo.

  asante kwa kuja kuchangia maswali yangu.

  muuza mitumba analipa kodi iweje kiongozi mkuu wa chama upate posho milioni 7.5 bila kodi.

  kulipa kodi ni wajibu wa sisi raia wote. uzembe wa TRA si sababu ya kushindwa kulipa kodi. ukishindwa kulipa kodi unakuwa na kosa. tuambie kwanini ni sawa kwa wewe kuwa na pato la milioni 7.5 na kushindwa kulipa kodi.
   
 7. M

  MPG JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr Slaa kipenzi cha watanzania yupo vijijini anawaelimisha watanzania ili wajue dhuruma ya chama cha MGAMBA CCM dhidi ya watanzania.
   
 8. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Hivi wewe huwa unasomaga hili jamvi vizuri na thread by thread, topic by topic??maana unarudia vitu vile vile ambavyo vilisha jadiliwa, find something else cha kuongelea kama umeme na kwa nini unalala na giza na sio maswali ya kipuuzi na too personal na yasikuhusu na umbeya.
   
 9. I

  Ismaily JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maoni yangu waislam tuache kudanganywa na wajinga wachache kama BAKWATA ambao ni adui namba moja wa waislam tangia enzi za uhuru,BAKWATA ipo kwaajiri ya kulinda maslahi ya serikali ya CCM Badala ya waislam ambao tuna matatizo mengi.
   
 10. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Acheni maswali ya kijinga haya,hivi unavyoona CHADEMA inaongozwa kidini au wakitaka kufanya kitu lazima waingize dini??au CCM yenu pia inaongozwa kidini??acheni mambo ya udini na tuangalie why tunalala na giza bila sababu za msingi na sio kutoa upupu usiokuwa na mpango.......
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Wasalaam Dr Slaa, na nakushukuru sana kuwepo kwako hapa jamvini.

  Natambua kuwa CHADEMA hawajakamata dola na hivyo wana-limitation katika kutatua matatizo ya watanzania wengi maskini. Hata hivyo tumeshughudia mchango mkubwa wa CHADEMA katika kutatua tatizo la sukari (yaani kushusha bei) na kubwa zaidi, kuilazamisha serikali ya ccm kuanza mchakato wa katiba mpya.

  Sasa hivi tuna tatizo sugu la umeme na kila kukicha inaonekana kama mambo yanazidi kuwa mabaya zaidi kuliko hata jana yake! Kama taifa tunaanza kupoteza imani na walio madarakani juu ya uwezo, na nia ya kutatua tatizo hili. Ningeomba kujua CHADEMA wana-mpango kuishinikiza serikali hii ya ccm @kutambua kuwa umeme kwa sasa hivi ni janga la kitaifa? (b)kuweka msimamizi mwenye uelewa mpana na uwezo/uthubutu katika wizara ya nishati na madini, na (c)kuunganisha nguvu ya watanzania katika kudai marekebisho ya haraka kwenye hili tatizo la umeme?

  Nasema haya kwa sababu binafsi siamini kama Mh Ngeleja ana uwezo wa kutatua 'complexities' kwenye sekta ya nishati ya umeme. Na pia siamini hata kidogo kuwa tatizo ni bwala la Mtera 'kukataa' kujaa maji. Taarifa nilizonazo ni kuwa kuna wakulima wa mpunga wanashirikiana na bwawa la Mtera, je ushirikiano wao unaathiri (kwa kiasi chochote hata kama ni 1%) ujao wa maji wa bwawa la Mtera? na pia nijuavyo mimi, initial agreement ya IPTL ilikuwa kuleta mitambo ambayo ingeweza kutumia both oil na gas (baada ya technicak adjustment) lakini mitambo iliyoletwa nchini ni ya kutumia oil peke!

  Then Symbion, sasa hivi wanazalisha chini ya capacity kwa sababu hawapati gas ya kutosha toka Songosongo, na kuna mchezo wa kuku na yai unaendelea maana Songosong wanawaambia Symbion kuwa wakitaka gas waongee na Tanesco na Tanesco wanawaambia Symbion wakitaka gas waende Songosongo!

  Najua una sources nyingi na unaweza ku-double check haya matatizi niliyoandika lakini nadhani ingesaidia sana kama wananchi wote wangejua maana haiingii akilini kwa nini Mtera haijai!

  Shukrani
   
 12. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Waislam wengi sasa hivi wanashabikia CCM kwa vile inaongozwa na muislam na sio chama chenye dini tofauti ambacho kinataka kuleta maslahi kwa taifa na kwa ajili ya vijana wetu wanaochipukia,this is nonsense kabisa na siwezi kufanya huo ujinga,mtu kabisa anakaa na kuuliza nonsense kwa ajili ya ku support chama ambacho hakina maslahi kwa taifa....tuangalie tulikotoka na tunakoenda,sasa hivi imefikia kwa day unapata umeme 4 hours je bado mnalizika na hili swala???na tukiwaachia hawa watu madaraka mnaona tunaenda wapi?na tutaishi vipi??si tutakuwa hatuna umeme kabisa??tufikirie zaidi na udini tuweke pembeni ili tuweke mabadiliko mapema kwenye hii nchi kabla haijawa too late.........
   
 13. Loyal_Merchant

  Loyal_Merchant JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 589
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  nadhan utakuwa na upungufu wa mawazo kama sio akili, posho ya sh milion 7 bila kulipa kodi ni uzembe wa serikali yako kutoweka na kutokuwa tayar kuweka mikakat ya kudhibit mambo kama haya. Kama serikali inataka kata kodi katika hela hii n lazma strategies za kukusanya mapato wazbadilishe. Hiyo n changamoto kwa serkal ya ******. If you cant beat me then join me. Hamwez pambana na cdm, bas unganen nasi.
   
 14. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #14
  Jul 3, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Malaria Sugu,
  Wiki hii nimekuwa maeneo mbalimbali ya Kisarawe. Wengi wao waislamu. Unawazungumzia Waislamu gani? Waislamu ninaokutana nao wanazungumzia tatizo la kuwa na mlo usio na uhakika wa siku, kutokuwa na maji safi na salama, hakuna zahanati na dawa, hakuna barabara, wanaishi nyumba za makuti. Unawazungumzia wepi na ulikutana nao wapi?
   
 15. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Mkuu ndio ambacho nashangaa,ni upuuzi tu na hamna jipya,wanaona kabisa magamba wanafanya ujinga eti kwa vile ni waislam basi lazima kuwatetea....ni upuuzi uliokithiri kabisa na kukosa kazi ya kufanya,tuangalie chama chenye maslah kwa taifa na chenye kuweza kufanya mabadiliko.....toka lini CCM ikawa marafiki wa waislam??shtuka.
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  Jul 3, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,470
  Likes Received: 19,854
  Trophy Points: 280
  we dogo sikiliza usione watu wanakukaushia tu hapa sio kwamba hatukuoni ...nnyie mumeuliza dokta yuko wapi na amekuja hapa kujibu hoja zenu sasa inabidi muulize maswali ya msingi yenye tija kwenye jamii kuna vitu vingine sio nvya kuuliza wewe ushawahi hata kupiga stori na kikwete au Nape??? huwezi hata siku moja sasa umepata fursa ya kujibiwa hoja zako na viongozi wa wakubwa kama hawa moja kwa moja inabidi uweke jazba zako na maswali ya kipuuzi pembeni ..
   
 17. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #17
  Jul 3, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  FJM,
  Thanks. Very serious concern. Ni dhahiri kwa hali tuliyonayo uchumi utadidimia zaidi.
  i) Sina hakika kama nitamaliza sentensi kwa kuwa niko kwenye reserve charge na sina umeme nilipo, kiashiria cha dhahiri. Mgawo umekuwa mkali kuliko wakati wowote katika historia ya Tanzania.
  ii) Serikali imeonyesha udhaifu, kushughulikia kuliko wakati wowote ule
  iii) Serikali imekuwa ikitoa kauli tata, za udanganyifu na upotoshaji
  iv) Serikali/Tanesco imeingia kwenye mkataba kinyume na amri ya mahakama na hivyo kuzua utata zaidi kuhusu nia na malengo ya mkataba na Symbion na hakuna uwazi katika mchakato wa kuingia mkataba huo.

  Chadema, tutakuwa na Kamati Kuu hivi karibuni, itakayofuatiliwa na Operation Sangara Dodoma, Singida, na Morogoro. Tutatoa kauli ya Chama kufuatia Kikao cha Kamati Kuu, ikiwa ni pamoja hatua mahususi za kuishinikiza Serikali.

   
 18. M

  MAURIN Senior Member

  #18
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr Slaa ni mtu smart siyo kama KIKWETE ambaye kila siku yupo nje ya nchi wakati watanzania wanaishi katika maisha magumu,kuna janga la umeme ambalo linarudisha maisha ya mtanzania nyuma,kazi ya KIKWETE anayofanya sasa hivi ni kuitumia BAKWATA KUENEZA PROGANDA AMBAYO KIMSINGI IPO KWA AJIRI YA KUWAGANDAMIZA WAISLAM KWA KWA KUFICHA UOVU WA SERIKALI YA CCM,ILA UZURU JAMII IMESHAELEWA MBINU HIZO ZINAZOTUMIWA NA SERIKALI YA KIKWETE KWA KUWEKA MAKONGAMANO YA BAKWATA AMBAYO YAPO KWA AJIRI YA KUILINDA SERIKALI YAKE KWA MAOVU YAKE
   
 19. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #19
  Jul 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Dr. Unapozungumzia nyumba bora sikuelewi!nakumbuka coverage moja channel ten ilimuonyesha mzee wako yaani Slaa akiwa katika makazi duni sana tena yenye kukatisha tamaa hivi usemi wa ''charity begins at home'' hauna maana?

  Leo unaubiri makazi bora huku ukijua for the past fifteen years as an MP bila ufisadi usingeshindwa kumjengea baba yako nyumba ya kisasa.Hapa kuna tatizo la aidha ubinafsi au hujui unachokiubiri.Mzee hawezi kuishi na Mbuzi ndani hata kidogo.

  Sitaki upambe,nahitaji Dr. anijibu hili kwani linamuhusu moja kwa moja katika jitihada zake za kutukomboa katika umasikini kama anavyodai.
   
 20. F

  FJM JF-Expert Member

  #20
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  @Malaria Sugu, ili kuwa na a very cilivilised debate ni vizuri tukangea issue based on facts kuliko hisia. Dr. Slaa amekubalika kwa wananchi wengi Tanzania kupitia 'bunge'. Ni kutokana na umahiri wake wa kuibua uzembe, ubadhirifu na kutozingatia sheria katika governance system yetu ndiko kumemfanya akajulikana kwa watanzania. Na amekaa bungeni miaka 15, kama utakuwa umesahau mapambano yake ndani ya bunge kaombe 'hansard' za bunge ili uweze kuandaa essay yenye mashiko.

  Hii tabia ya character assissination ili mtu aogope/ashindwe kuibua mapungufu kwenye utawala wa umma is extremely low and un-guided way of dealing with the malfunctions on your part.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...