Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,889
Minong'ono ya chini kwa chini inasema katika wosia wake Mzee Mwinyi alitaka akazikwe Mkuranga nchini Tanganyika wazazi wake walipolala na si nchini Zanzibar alikoenda kama mhamiaji kwa mahitaji ya kisasa miaka hiyo
Wiki chache zilizopita kulikuwa na harakati nyingi huko wilayani Mkuranga hasa harakati za matengenezo ya barabara na redio mbao zikabashiri kama maandalizi ya tukio kubwa siku za usoni huku wengine wakisema kwa sauti za chini kwamba ni maandalizi ya mazishi ya Mzee Mwinyi
Baada ya hapo inasemekana ukatokea mkanganyiko mkubwa ama mgogoro kati ya ndugu na wanasiasa wa upande zote mbili za muunganiko wa Tanganyika na Zanzibar
Kuna kundi lilisisitiza ufuatwe wasia wa marehemu kutoka kulazwa pembeni ya wazazi wake huko wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani nchini Tanganyika na kuna kundi lingine kwa sababu za kisasa likitaka marehemu akazikwe nchini Zanzibar Unguja
Inasemekana mgogoro huo uliendelea hadi kundi la pili liliposhinda ndio uamuzi wa kutangaza tanzia ulipotolewa
Haya ni maneno yasiyothibitishwa popote na yeyote lakini kama ni kweli.
Nasisitiza kama ni kweli marehemu ataenda kuzikwa mahali kinyume na wosia wake.. Matatizo makubwa yanaweza kujitokeza
Tamshi la mwanadamu kiroho halina nguvu sana mpaka mhusika anapogeuka mfu baada ya roho kuuacha mwili.. Roho iachapo mwili huwa huru isiyo na mapaka ya kibinadamu na utashi wake! Na hii ndio hubeba matamshi ya wosia laana ama baraka za marehemu na kuzitekeleza katika ukamilifu wake!
Watani zangu Wachaga ni mashuhuda wazuri kwenye hili! Hivyo wanasiasa wamakinike mno na hili lisije kuleta mengine yasiyotarajiwa
Pumzika kwa amani mzee Ruksa