Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
Naomba kuchukua nafasi hii kutoa ufafanuzi wangu binafsi kuhusu utata uliojitokeza kuhusu mazishi ya Malkia wa Uingereza Queen Elizabeth 11 siku ya leo!
Wapo viongozi walioalikwa rasmi kuhudhuria mazishi hayo na wapo walioalikwa jumla jumla kwa kuhudhuria kama viongozi wa nchi za Jumuiya ya Madola.
Hii ni sawa na kuwaalika rasmi watu kuhudhuria harusi yako na hapo hapo kuwakaribisha ndugu zako wa karibu jumla jumla kuwa nao wanaweza ku jumuika nanyi
Kwa uelewa wangu waliopewa rasmi barua za mwaliko ni hawa...
Katika hii orodha aliyealikwa rasmi kuhudhuria hayo mazishi kutoka Afrika ni Kiongozi wa Jamhuri ya Afrika Kusini Rais Cyril Ramaphosa.
Viongozi wengine waliotoka sehemu mbali mbali duniani wapo walioalikwa jumla jumla kama viongozi wa nchi wanachama wa Commonwealth.
Hivyo haishangazi kuona wakipewa huduma za jumla jumla kama ilivyotokea kwa baadhi yao kupewa huduma ya usafiri wa pamoja wa mabasi.
Kama nitakuwa nimepotosha kwa namna yoyote nia na madhumuni ya mialiko hiyo natanguliza samahani kwa viongozi na wananchi wa nchi husika.