Mazishi ya Kanumba, kamati yapiga hela ndefu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mazishi ya Kanumba, kamati yapiga hela ndefu

Discussion in 'Celebrities Forum' started by KIM KARDASH, Apr 16, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  KAMATI YA MAZISHI YA KANUMBA NA KASHFA YA KUCHAKACHUA MICHANGO

  [​IMG]
  Hawa wenye suti na miwani myeusi ndio baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wanaodaiwa kufanya upigaji huo wa fedha za michango ya msiba

  Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka ndani ya familia ya Kanumba, kamati hiyo imedaiwa kufanya uchakachuaji wa michango hiyo inayokadiriwa kuwa mamilioni ya fedha, achilia mbali

  vitu kadhaa, yakiwemo magunia 32 ya mchele.
  Chanzo hicho kimeidokeza Sayari kuwa, dalili za hali hiyo zilianza kujitokeza mapema kabisa pale mwanandugu mmoja alipoenguliwa kwenye kamati hiyo, kwa kile kinachoelezwa, kamati hiyo kufanya jukumu hilo kwa uhuru zaidi.
  Dalili nyingine, ni kitendo cha wajumbe wa Kamati hiyo kutoweka baada ya mazishi hadi walipofika nyumbani kwa marehemu Alhamisi usiku.
  Kwamba, pamoja na mambo mengine, kwenye kikao kilichofanyika siku hiyo kati
  ya wanandugu na kamati hiyo, Mama Kanumba amezuia kuzungumzia suala la michango.
  "Mama Kanumba ametakiwa asiseme lolote kwa Waandishi wa Habari kuhusu michango… kaelezwa kama atafanya hivyo, huenda asipate kitu kabisa," alisema ndugu huyo.
  Kwa mujibu wa chanzo hicho, Kamati hiyo imetoa onyo hilo kwa vile tangu kwisha kwa maziko ya Kanumba, wamekuwa wakipata usumbufu wa simu watu kuulizia kilichokusanywa na kilichobaki.
  Chanzo hicho kimedokeza kuwa, baada ya kamati hiyo kukutana na wanafamilia kwa mara ya kwanza baada ya ukimya mrefu, ilisema michango yote ni sh mil 51.
  Kati ya fedha hizo, gharama za mazishi ni shilingi mil 48 huku kukiwa na deni la sh
  mil 2 za ukarabati wa barabara Leaders kutokana na uharibifu uliofanywa na waombolezaji.
  Chanzo hicho kimedokeza kuwa, walipohoji fedha zilizochangwa kupitia M-pesa kupitia namba ambayo ilitangazwa, walielezwa ilipatikana sh 20,000 tu.
  Kilisema, kiasi hicho ni kiduchu mno kwa sababu mashabiki wa Kanumba wa Mwanza pekee, walichanga sh 300,000.
  Kilidokeza kuwa, pia kulikuwa na gunia 32 za mchele zilitotolewa na msamaria, hazijulikani zilipokwenda.
  "Licha ya kutolewa gunia 32 za mchele, hazijulikani zipo wapi…. fikiria hata mfiwa, anakosa hata gunia moja la kwenda kuanzia maisha mapya bila mwanaye," kilidokeza chanzo hicho.
  Kilipoulizwa kwanini hawakuweka ndugu kwenye kamati hiyo tangu mapema, kilisema alikuwemo, lakini akaenguliwakwa kwa zengwe.
  Uratibu wa msiba huo ulikuwa chini ya Kamati iliyokuwa chini ya Gabriel Mtitu na wajumbe kama Ray, Cloud, Steve Nyerere, Hapines Magese, Mtitu William, Jacob Steven na wengineo.
  Sayari ilipomtafuta Mtitu kwa njia ya simu jana, alisema kutokana na usumbufu ambao wanaupata kwa wengi kutaka kujua juu ya michango hiyo ya msiba, Kamati yake imeamua kukutana na waandishi wa Habari kesho Jumanne kuweka kila kitu bayana.
  "Kuna mengi yanasema hadharani na chini ya zuria kuhusu rambirambi, kwa lengo la kuweka bayana kila kitu, tumepanga kukutana na waandishi wa Habari Jumanne (kesho) kuanzia majira ya saa nne," alisema Mtitu.
  CHANZO:GAZETI LA SAYARI
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  honestly..yasingetokea haya ndio ningeshangaaa
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Si watoe receipt kuondoa mzozo
   
 4. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  jamaa wanaonekana wana nguvu sana kama waliweza kumuengua ndugu wa marehemu kwenye kamati ili tu wafanye kazi kwa uhuru zaidi na kama wamempiga stop mpaka mama kuongelea issue za michango unadhani ni watu wa kuwaambia waonyeshe risiti,pia ikibidi risiti si zinatengenezwa na makaratasi tu
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Iyo ya mpesa 20,000tshs nimechoka!
  Anyway wekeni mambo hadharani basi wapenzi wake waridhike
   
 6. ze encyclopedia

  ze encyclopedia JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 271
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  mmmmmh.....................hata JB? napita
   
 7. T

  The Priest JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 1,026
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nilijua tu lazima haya yangefuata,oppotunists wakubwa hao...laana kubwa inawanyemelea hao.
   
 8. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Aliishi kisanii akazikwa kisanii
   
 9. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Na ikiwa waliweza kuamua the great azikwe bongo wakati baba alitaka SHY kweli wananguvu!
   
 10. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  lakini ndio hivyo kufa kufaana,kama shughuli ilienda vizuri naona walizitumia kuvunja kamati kwa kujipongeza kwa kazi nzuri!
   
 11. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kule dizaini upigaji ungekua mgumu si unajua wasukuma tena,wangewashukuru kwanza kwa kuufikisha mwili pale then wangewataka wakae pembeni ili mambo ya "kimila" yachukue nafasi kubwa,hata haya masuti na miwani myeusi yasingekua na chance
   
 12. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Imethibitiswa Tshs........ imetumwa kwenda kwa ASHA BARAKA Tarehe 8/4/2012 saa 8:20 AM Salio lako la M-Pesa ni Tsh...... Umeingia kwenye droo!

  Kwa ujumbe huu tu uliokuwa unarudi hapo ujue tayari usanii Jazz Band. Itathibitishwa vipi ikiwa mkwanja alioripoti huyu mdau ndio aliopata na utaendaje voda kuulizia akaunti ya mtu binafsi??? Hivi unajua kuwa ushindani ni mkali sana kwenye bendi hivyo unabidi kutafuta vyanzo vya ziada vya mapato? Mshike mshike ndege tunduni....
   
 13. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,542
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Kula ni kula mbaya ni kukomba mboga.
   
 14. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,027
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kweli, kufaa kafaana!.
   
 15. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #15
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Kama TFF vile.......
   
 16. m

  makumvi Member

  #16
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 26, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kama ni kweli basi kamati ya mazishi imefanya makosa pasipokuwa involve wanandugu wa marehemu, hata kama hawakuchakachua michango ya Rambi rambi bado wamejijengea taswira mbaya kwa familia ya marehemu na wanajamii kwa ujumla.
   
 17. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  mimi ningeshangaaa sana haya yasingetokea jamani lol
   
 18. m

  mtx2006 JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2012
  Joined: Feb 1, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Wengi mtakuwa mmefatilia kwa karibu yote yaliyotokea katika kifo cha Msanii Steven Kanumba. Baada ya kifo hiki watu mbalimbali wakiwemo wabunge wamezidi kupaza sauti zao kutaka kifanyike kitu ili kazi za wasanii zisiimbiwe. Hii ndio iliyonipelekea kuandika hili ili kuona changamoto hii tutaikabili namna gani.

  Wote tulishuhudia Clouds FM radio na TV zikirusha na kutangaza live matukio yote ya kifo cha Kanumba. Ila sina uhakika kama Familia ya Marehemu Kanumba ilitoa idhini ya chombo hicho cha habari kufanya hivyo walivyofanya. Na kama walipata ni kiasi gani familia imelipwa kwa ajili hiyo. Na kama hawajafanya yote hayo (Kupata ruhusa na kuliilipa familia) basi wamefanya WIZI mkubwa.

  Hakuna atakayebisha kwamba Chombo hicho cha habari kimejinufaisha sana na msiba ule kwa njia mbali mbali. Kwanza watu wengi kukijua kuwa kipo, watu wengi kununua starTY ili tu wanase Clouds TV na kushuhudia matukio ya msiba wa Kanumba na pili kuwanyima haki wanafamilia kuja kutoa DVD za coverage yote ya musiba wa Kanumba na kupiga pesa kidogo kwa ajili ya maisha.

  Wote wanajua wenzetu walivyofaidika kwa kuuza rights za matangazo. Mfano kifo cha Michael Jackson, Whitney Huston na hata mjuu kuu wa mandela aliyetaka kuuza rights za kurusha kifo cha Mandela kabla hata hajafa.

  TUTAMALIZAJE WIZI HUU WA VYOMBO VYA HABARI KAMA CLOUDS RADIO AND TV. Nipo tayari kufungua kesi ya madai kwa niaba ya familia ya Kanumba ili Clouds Walipe maana wamefaidika.
   
 19. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #19
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,072
  Trophy Points: 280
  mkuu, wabongo akili yetu tunalazimisha iwe fupi na 'ndio maana wakenya wanatudharau'.
  Hawa jamaa upeo wao hawawezi kuona huko unapopasema!

   
 20. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #20
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Always GIFT goes to the GIVER
   
Loading...