Mazingira machafu Marian Girls/Boys Sec, Bagamoyo

Mazingira machafu Marian Girls/Boys Sec, Bagamoyo

kachumbari

Senior Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
126
Reaction score
9
Nasikitishwa na kushangazwa kuona tunaletewa kadi za michango ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Marian pale Bagamoyo, wakati hali ya mazingira ya shule zake ni mbaya mno, hata ofisi za waalim na mabweni ya watoto ni hovyo.

Hivi wizara husika haioni hili?

Hata Kama vijana wanafanya vizuri inabidi Hali ile irekebishwe. Tunaamini Kama anaijali hostel pale Msalabani ikawa na mazingira mazuri kwa nini asiboreshe na ya shule zake pia?
 
sasa wizara inahusika vipi hapo?au hujui kua marian ni shule binafsi?
 
Sawa tu.Cha msingi wanafunzi wanafanya vizuri katika mitihani yao.Elimu kwanza mengine mbwembwe tu.
 
Kuna shule hapa inaongoza kwa usafi,lakini wakati mwingine hiyo division four wanaisikia redioni ni mwendo wa sifuri tu.
 
Hapa ndo umeona pakushtaki....Wana web site yao..peleka malalamiko yako kule..

Hamisha mtoto wako...Peleka unakoona ni kusafi ala!!
 
Mkuu, nina wasiwasi utakuwa umetumwa. Katika Shule zote hapa Tanganyika, Marian Girls/Boys ndio chafu zaidi? Poa, tumekusikia. Sasa tuongelee kiwango cha ufaulu cha hiyo Shule. Unasemaje?
 
kwani kuchanga ni lazima?

Kuchangia chuo kikuu ni lazima kwa kila mwanafunzi hapo bado nichango ya ujenzi wa madarasa na hiyo ni lazima usipo changia wanasubiri siku ukienda kuchukuwa result au cheti utaipata fresh lazima ulipe
 
Mhhhhhh elimu first majengo baadae mfano Marian ( pwani) na Alliance ( mwanza) schools zina majengo ovyoo lakini zna kimbza kitaifa.
 
Nililalamika katika jukwa hili January mwaka huu kuhusu hali mbaya pale Marian Girls ndugu zangu wengi waliniponda je mmeona mayokeo ya form six walivyo fanya vibaya hizi shule Marian Boys and Girls.ni kwamba mwenye shule amezipuuza kabisa na kuto jali kuwa na waalim bora shule inakwenda mrama.
 
endelea kufatilia matokeo ya shule izo.. usiache kabisa... fuatilia idadi ya wanafunzi wanao graduate ndani ya mwaka, divisions wanazo pata..
mwaka huu 2016 hizo shule zipo top ten... girls ya nne na boys na tano.. lkn ni shule pekee zenye idadi kubwa ya watahiniwa ndani ya top ten.
 
Nililalamika katika jukwa hili January mwaka huu kuhusu hali mbaya pale Marian Girls ndugu zangu wengi waliniponda je mmeona mayokeo ya form six walivyo fanya vibaya hizi shule Marian Boys and Girls.ni kwamba mwenye shule amezipuuza kabisa na kuto jali kuwa na waalim bora shule inakwenda mrama.
Imekula kwako...Inpoongelea kufanya vibaya unaongelea ktk mrengo gani. ?
 
Back
Top Bottom