Nsekela aongoza harambee shule za Marian, Bagamoyo

Blasio Kachuchu

Senior Member
Sep 7, 2016
152
111

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) akilisalimiana na Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Kadinali Polycarp Pengo wakati alipowasili kwenye viwanja vya michezo vya Bongololo vya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Marian mjini Bagamoyo, alipokuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Marian inayojengwa pamoja na zahanati, katika eneo la Mlingotini, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani. Kushoto ni Mwanzilishi wa Shule za Marian, Father Valentino Bayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela ameongoza harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Marian inayojengwa pamoja na zahanati, katika eneo la Mlingotini, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.

Harambee hiyo iliyofanyika leo katika viwanja vya michezo vya Bongololo vya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Marian mjini Bagamoyo ilisindikizwa na shughuli tofauti ikiwamo riadha, ibada maalumu ya kumshukuru Mungu pamoja na maonyesho ya wanafunzi.

Katika mchango wake, Nsekela alisema kuwa Benki ya CRDB imetoa Sh20 milioni kama sehemu ya mchango wa kufanikisha ujenzi huo huku yeye mwenyewe akichangia Sh10 milioni na marafiki zake wakitoa zaidi ya Sh10 milioni zitakazotumika kumalizia ujenzi wa madarasa shuleni hapo na miundombinu ya zahanati.

“Elimu ni moja ya kipaumbele cha Benki ya CRDB. Kila mwaka, tunatenga asilimia moja ya faida yetu baada ya kodi kusaidia utekelezaji wa miradi ya kijamii ikiwamo ya elimu na afya. Mwaka jana, tulitumia zaidi ya Sh366 milioni kwenye elimu na zaidiya Sh403 milioni kwenye afya. Tunafanya hivi tukiamini Serikali pekee haiwezi kukidhi mahitaji makubwa yaliyopo nchini hivyo ushiriki wa taasisi za dini na sekta binafsi ni muhimu,” amesema Nsekela.

Nsekela aliyekuwa mgeni rasmi kwenye harambee hiyo, alitoa mchango huo baada ya Father Valentino Bayo, mwanzilishi wa shule za Marian kumweleza kuwa jitihada zao za kuielimisha jamii hasa watoto wa mwambao wa Pwani zinakwama kidogo kutokana na ukosefu wa fedha.

“Sekondari ya Wasichana Marian ilijengwa Februari 1997 ili kuwapa fursa wasichana wa Mkoa wa Pwani na maeneo jirani kupata elimu bora. Mpaka sasa tumetanua huduma na sasa tunajenga Sekondari ya Wavulana hapa Mlingotini. Pia, tunajenga zahanati kuwahudumia wananchi. Ili kukamilisha miundombinu muhimu kwa huduma hizi, tuna upungufu wa fedha ambazo tunawaomba wadau mtusaidie kwa michango ya hali na mali,” alisema Father Bayo.

Baada ya harambee hiyo iliyokamilika kwa mafanikio, Mwalimu Super Vedasto, mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Marian Mlingotini aliishukuru Benki ya CRDB na wazazi waliojitokeza.

“Tunamshukuru Nsekela na marafiki zake kwa kujitoa kwao kufanikisha harambee hii. Wazazi na wananchi waliokuja leo wametupa faraja na tunaamini tutafanikiwa kukamilisha ujenzi huu hivyokutoa elimu bora kwa vijana wetu,” amesema Mwalimu Vedasto.

Naye Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kadinali Polycarp Pengo aliyeshiriki harambee hiyo aliipongeza Benki ya CRDB kwa kujitoa kushirikiana na kanisa kuboresha huduma za jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) akizungumza jambo na Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Kadinali Polycarp Pengo, wakati wa harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Marian inayojengwa pamoja na zahanati, katika eneo la Mlingotini, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo.

Sehemu ya wanafunzi wa sasa wa Shule za Marian.
OTMI6034.jpeg

Burudani kutoka kwa Wanafunzi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akimkaidhi hundi kwa Mwanzilishi wa Shule za Marian, Father Valentino Bayo.

OTMI6456.jpeg

OTMI6433_1.jpeg
 
CRDB wamechukua maji kisimani, wakenda kumwaga baharini. Marian wanao uwezo wa kujenga shule vizuri kabisa bila shida. Hii michango ilitakiwa kwenda "Mwembe kiuno" sekondari, au shule ya msingi "sogea tukae".

By the way, sioni kama lengo la kuzianzisha hizi shule za Marian linatimizwa kwa sasa. Imekua kinyume chake!
 
Uko sahihi chief.
Malengo ya kuanzishwa kwake hayatimizwi
 
CRDB wamechukua maji kisimani, wakenda kumwaga baharini. Marian wanao uwezo wa kujenga shule vizuri kabisa bila shida. Hii michango ilitakiwa kwenda "Mwembe kiuno" sekondari, au shule ya msingi "sogea tukae".

By the way, sioni kama lengo la kuzianzisha hizi shule za Marian linatimizwa kwa sasa. Imekua kinyume chake!
Marian ya Sasa wanaangalia pesà sio akili za mtoto

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hapa haijakaa sawa,
Labda huyu Majid hazijui vizuri hizi shule. Na ni Bora hizi 20mil wamechanga yeye na rafiki zake binafsi, na sio benki kama benki.

Hizi shule zinajiweza, hazihitaji michango. Ada zake ni kubwa tu, plus idadi ya wanafunzi wanaojiunga means collection yake ni kubwa.

Ni shule zenye mrengo wa kibiashara zaidi kuliko kusaidia jamii. Ni kama zilivyo tu Feza Schools na Zinginezo za aina yake.
 
Kwenye maelezo pale juu imeandikwa katika mchango wake, Nsekela alisema kuwa Benki ya CRDB imetoa Sh20 milioni kama sehemu ya mchango wa kufanikisha ujenzi huo huku yeye mwenyewe akichangia Sh10 milioni na marafiki zake wakitoa zaidi ya Sh10 milioni. Mimi nilivyoelewa hapa ni kwamba bank kama bank ya CRDB wametoa 20m, yeye mkurugenzi katoa 10m na marafiki zake wametoa zaidi ya 10m. Hivyo kwa ujumla bank, mkurugenzi na marafiki zake wamechangia zaidi ya 40m.
 
Crdb wachagie shule nyingine za jamii sio hizi za watu binafsi.

Marian hawajashindwa kujenga shule, ada kubwa wanayotoza wazazi faida wanapeleka wapi?

Cha ajabu shule inajengwa kwa michango ya waumini na misaada lakini ada yake kubwa sana. Huu ni wizi.

Mapato ya kanisa na ada vinafanya kazi gani kama bado hadi warudi tena kukamua watu kwa michango na harambee?

Taasisi za dini zimejaa utapeli, unyonyaji, kuongeza umasikini kwa waumini wake kwa kuwatoza michango na sadaka zisizo na kikomo na bado hawasaidii waumini kwa chochote.
 
Kwenye maelezo pale juu imeandikwa katika mchango wake, Nsekela alisema kuwa Benki ya CRDB imetoa Sh20 milioni kama sehemu ya mchango wa kufanikisha ujenzi huo huku yeye mwenyewe akichangia Sh10 milioni na marafiki zake wakitoa zaidi ya Sh10 milioni. Mimi nilivyoelewa hapa ni kwamba bank kama bank ya CRDB wametoa 20m, yeye mkurugenzi katoa 10m na marafiki zake wametoa zaidi ya 10m. Hivyo kwa ujumla bank, mkurugenzi na marafiki zake wamechangia zaidi ya 40m.
Duh,
Hizi ya Bank kama bank sio sawa. Kuna shule nyingi zenye uhitaji. Wale wenye hisa CRDB watajisikiaje? Yeye binafsi atajijua mwenyewe kwa mapenzi yake.
 
Hapa haijakaa sawa,
Labda huyu Majid hazijui vizuri hizi shule. Na ni Bora hizi 20mil wamechanga yeye na rafiki zake binafsi, na sio benki kama benki.

Hizi shule zinajiweza, hazihitaji michango. Ada zake ni kubwa tu, plus idadi ya wanafunzi wanaojiunga means collection yake ni kubwa.

Ni shule zenye mrengo wa kibiashara zaidi kuliko kusaidia jamii. Ni kama zilivyo tu Feza Schools na Zinginezo za aina yake.
Kwa akili ndogo tu ya kufikiri, Nsekela ni mnufaika na hiyo biashara, ama yeye moja kwa moja ama anamsaidia mtu katika hiyo biashara.

Tunatoaje hela benki?

Basi awe mgeni rasmi ili tupige mpunga.

Kiukweli kuichangia Marian haiwezekani. Marian ina utajiri mkubwa kuliko CRDB.
 
Marian ina utajiri kuliko CRDB?
Unaijua CRDB au unaongea tu, benki kubwa vile yenye mamilioni ya wateja na trillions of assets izidiwe na kishule kimoja kinachoitisha harambee. Ushawahi soma hata financial report ya hiyo bank mwaka wowote?
Marian hawana utajiri hata 5% ya CRDB
 
"Sekondari ya Wasichana Marian ilijengwa Februari 1997 ili kuwapa fursa wasichana wa Mkoa wa Pwani na maeneo jirani kupata elimu bora"
Hivi hata viongozi wa dini siku hizi ni matapeli,hii shule lini ililenga kusaidia wasichana wa mkoa wa pwani?? Hata tukifanya sensa ndogo hapo sidhani kama wasichan wa pwani watafika hata 1%,
 
Yaani wewe! Ushafikiri siku wenye amana zao wazichomoe, CRDB itasimama?

CRDB ni taasisi inayojijenga kupitia amana za watu na mipaka yake inafahamika.

Lakini huwezi kulifilisi kirahisi kanisa katoliki ambalo ni wamiliki wa Marian schools.

Kanisa siyo jimbo tu la Morogoro. Wamefungamana worlwide. Ni system. Wanaweza kufanya jambo lolote watakalo kama kanisa. Usiitazame Marian kama shule, tazama mmiliki ni nani halafu linganisha na CRDB.
 
Kampuni mara nyingi hazitoi misaada kwenye hamna, vigumu kuwaona shule yenye majengo mabovu na sare zimechafuka na kuchanika, vyoo havitoshi. Positive effect itakayotokea hapo ni ndogo kibiashara kuliko wakienda shule inayojulikana. Kwanza mazingira mazuri yanaendana na hadhi ya kampuni, taarifa itafikika zaidi kama hapa kila mmoja anaijua Marian, pia matokeo chanya yataonekana kwa wazazi, watoto na watumishi. Mjue kuna shule hakuna mwanafunzi hata mmoja mwenye kadi ya benki yoyote.

Kingine ni dini, waumini wa dini zote hupenda kwenda kwa mkumbo na upendeleo kwa taasisi zinazowaunga mkono ndio maana Abdulmajid kahudhuria kwa Wakristo na kuchangia. Image inayotokea hapo ni kubwa kwa benki, mwaka mwingine wataenda shule ya Kiislamu au walishaenda, mwingine ya Lutheran.

Makampuni hayatoi misaada kwamba yanawapenda sana Watanzania. Corporate Social Responsibility ni strategic hutoi hela bila calculations. Hata wanasiasa hutomuona mbunge anahudhuria mahafali shule ya kata madirisha hayana vioo, mpaka iwe shule nzuri nzuri. Last year NMB walitoa msaada CCBRT wakati wangeenda hospitali za ndani ndani uko ambako madawa tu ni tatizo
 
"Sekondari ya Wasichana Marian ilijengwa Februari 1997 ili kuwapa fursa wasichana wa Mkoa wa Pwani na maeneo jirani kupata elimu bora"
Hivi hata viongozi wa dini siku hizi ni matapeli,hii shule lini ililenga kusaidia wasichana wa mkoa wa pwani?? Hata tukifanya sensa ndogo hapo sidhani kama wasichan wa pwani watafika hata 1%,
Kweli, kuna wanafunzi wanatoka nje ya nchi. Wenyeji tunashangaa shangaa tu.
 
Shule za makanisa zinajengwa Kwa michango ya waumini lakini nashangaa zinakua na ada kubwa kiasi hata wengi wa waliochangia ujenzi hawawezi kupelekea watoto wao.
Kumbuka ni mfumo wa unyonyaji uliojengwa toka dola ya Rumi. Hiyo ni mifumo, haiwezi kubadilika.

Makanisa yote mfumo wake wa uchumi ni wa kinyonyaji.

Mfano tu mdogo, muumini mashuhuri na mtoa sadaka mzuri, akiumwa, kanisa haliwezi kutoa sehemu ya mapato yake kumsaifia matibabu. Badala yake akihitaji huduma ya kanisa kama ubatizo wa watoto au komunyo na kipaimara lazima alipie.

Ninawashangaa sana walio busy kumtolea Mungu.
 
Yaani wewe! Ushafikiri siku wenye amana zao wazichomoe, CRDB itasimama?

CRDB ni taasisi inayojijenga kupitia amana za watu na mipaka yake inafahamika.

Lakini huwezi kulifilisi kirahisi kanisa katoliki ambalo ni wamiliki wa Marian schools.

Kanisa siyo jimbo tu la Morogoro. Wamefungamana worlwide. Ni system. Wanaweza kufanya jambo lolote watakalo kama kanisa. Usiitazame Marian kama shule, tazama mmiliki ni nani halafu linganisha na CRDB.
Marian ni shule, mali za kanisa haziendeshwi hivyo. Yaani tuzungumzie Azam media utoke uko uzungumie Azam ngano na maandazi? Kwani nini maana ya asset management kwenye portfolio.

Kwani amana zimechomolewa? Kwanini uzungumie kitu ambacho hakijafanyika.
Unajua utajiri unapimwaje? Nikiwa na nyumba ya milioni 400 na wewe una ya milioni 20 utasema nyumba yako ndio yenye thamani zaidi kwa sababu ya kwangu inaweza kuungua. Kwani hapa kwa sasa tulipo shareholders wametoa assets CRDB, kwanini ifirisike na sio Marian. Any business is termed as a going concern.

Assets tu za CRDB ni zaidi ya trilioni 6, savings na fedha nyingine zinazozunguka humo ni zaidi ya trilioni 4. Anatokea mtu anailinganisha na kishule kilichokinga bakuri. Yale makao makuu ya CRDB pekee na lile eneo lake, plus makao makuu ya zamani pale viwandani ukiyauza hayo tu yanatosha kuizidi thamani Marian.
 
Back
Top Bottom