Maziko ya Ndugu Minyembe: Polisi Kawe tunaomba ulinzi msibani, vijana wamepanga kufanya fujo

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,151
Ni vyema tusisubiri maafa, tutoe angalizo mapema.

Maziko ni kesho

Ndugu zetu marafiki zetu wa Kawe Polisi, tunatoka msibani kunasikitisha ukiacha majonzi yanayoendelea.

Naamini mmeshapajua hapo msibani karibu na geti dogo la Lugalo. Bajaji kumi kidogo zimeshusha wahuni wanavuta bangi msibani hakufai. Ndugu zetu wa Kawe naamini mmefikishiwa taarifa na plan za msiba kesho.

1. Mpaka sasa wanahangaika wazike pale makaburi ya luventry

2. Wakitoka hapo wamepanga kusachi na kuingia maduka yote yaliyo karibu na makaburi na wamepanga kurudi Kawe kwa mguu wakifanya fujo na wizi

3. Wamepanga kufanya uhalifu mkubwa upande wa pili baada ya maziko

5. Tunaomba akazikwe makaburi ya E Fm

6. Tunaomba maduka na wafanyabiashara wote wa karibu na makaburi wapewe ulinzi mkubwa wamepanga kufanya fujo kubwa sana siku ya kesho

7. Nilichokiona pale kuna magrupu yametoka Mbagala/Vituka/Tegeta/na wanavuta bangi mpaka sasa

Kama hamuamini, wapo jirani na nyie. Ulizeni msibani kwa Rama, ni bangi kila kona

Tunaomba Jeshi la Polisi tushirikiane kwa pamoja kuondoa hizi fujo na kuwakanya kabisa hao wezi wenzie wasithubutu kugusa vijana wa pale M. Mapya

Tunaamini kabisa kwa ushirikiano tunaosaidiwa na kituo chetu pendwa Kawe basi pia tutasaidiana kuweka ulinzi msibani watu wasidhiruike, wanaotembea karibu ama wenye biashara maeneo anapozikwa.
 
Why? Whyyyy? Whyyyy? Why entertaining mob justice in a country where its citizens boast to be law abiders?

Minyembe is a human being too. He had blood running in his veins just like anyone of us.

Thieves, Robbers, bandits whatever have right to live. No one is guilty until proven in the court of law. Thats why even the president is afraid and hesitant to sign the death sentence to be implemented and enforce due to the weight concerning humans lives valueness.

Those people who killed this robber should be held accountable so that it will be a lesson to others who have this bad ideas and intentions of killing criminals at will without following proper law procedures.

Once again am heartbroken and saddened by the loss of this robber. In such a situation we should practice restraint and let full force of law to take course.

We are all sinners. What happened to this robber is unjustifiable. Its fundamental wrong and totally unacceptable for those mobs to kill this thief because he has a family too now they pass a very difficult time coming to terms to lose their beloved one.

I call to all citizens to be tolerant and restrain when encounteeing such situation dealing with Thieves. They are our brothers too.

Hata hivyo Alipangiwa atakufa hivyo pindi tu alipozaliwa.

Mzingo stroke Magonjwa Mtambuka
 
Hawa wahuni mbona wanabembelezwa Sana wanafanya watu wasiishi kwa amani.
Kaulize wanapovutia BANGI n umbali gan na .....ACHA mkuu wananguvu za ziadaa tutapambana naoo keshoo akiruka mmoja wanazika tenaaa wasijaribu tu......
 
We bwege unapiga sana mayowe bondeni ,enzi zetu mnyamala huko kwa mama zakharia na kopa walikoma, acha moscow chini huku mkwajuni kwenda bondeni.

Tulikomesha ukibaka wote.

Nilikua kamanda kimtaa ila jioni kwenye hiyo sungusungu utaomba poo.

Sasa nashindwa kuelewa hako kakibaka mmeshindwa vp kukaweka kati long time.

Vyuma nilivyokamatana navyo mimi vyote havipo, tulikua tukisema ondoka we nenda, tukikurudia ni safari
Jose kaondoka juzi tu na wasiojulikana, mi mzima na wengine tulihama long time, la inapokua vi issue kidogo km hivi hamuwezi kudeal navyo? Ndo naelewa vijanaume vya dar vikoje
 
Hii ndio shida ya kuleta uzi huku akifikiri wote tunatoka dar/kawe.

Hata mimi zaman nlikuwa kama ninyi nlikuwa very judge-mental ila nikajifunza taratibu nikaelewa, anyways mmesema hivyo sababu hamjui, huyu jama jana alikuja na story ya huyo minyembe ni nani na leo kaleta mwendelezo wake na nadhan target audience wake sijui niseme reader ni wale walosoma jana alichoandika kuhusu minyembe.... kama unataka kujua minyembe ni nan kasome post kama sio moja au mbili za huyu bwana za nyuma
 
Hata mimi zaman nlikuwa kama ninyi nlikuwa very judge-mental ila nikajifunza taratibu nikaelewa, anyways mmesema hivyo sababu hamjui, huyu jama jana alikuja na story ya huyo minyembe ni nani na leo kaleta mwendelezo wake na nadhan target audience wake sijui niseme reader ni wale walosoma jana alichoandika kuhusu minyembe.... kama unataka kujua minyembe ni nan kasome post kama sio moja au mbili za huyu bwana za nyuma
Angeweka hadidu rejea maana sio wote tulisoma hiyo jana. Kuhusu watu kudhani habari maarufu kwake ni the same kwa kila mtu ni tatizo pia.
 
Hao polisi mnawaamini sana? Kwa nini mtaani msiamue kutofungua maduka na watu wawaachie ndugu zake msiba wao. Anakwenda wakati mnajua kuna uwezekano wa kugeukiwa na kuporwa?
 
Back
Top Bottom