Salaam;
Nimepata habari kuwa Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Bashe ametoa maelekezo kwa vyama vya ushirika nchini kusimamia uzwaji wa mpunga na mahindi upitie kwenye vyama hivyo kwa utaratibu wa stakabadhi ghalani kama ilivyo kwa kwa mazao ya korosho na pamba.
Amesema utaratibu huo utasaidia kuongeza thamani ya mazao hayo na kuwanufaisha wakulima na kuwaepusha na unyonyaji wa wafanyabiashara wa mazao hayo.
Kwa maoni yangu naona utaratibu huu unaweza kuleta usumbufu katika upatikanaji wa chakula hasa tukizingatia kuwa mazao hayo ndo muhimu zaidi kwa nchi yetu (staple food).
Lakini nahofia utaratibu huu unaweza kuleta matatizo kwa wakulima wenyewe kama ilivyotokea katika uuzwaji wa korosho, kahawa na pamba.
Kiufupi sioni manufaa ya kutumia utaratibu huu kwa mpunga na mahindi kwa vile haya ni mazao ya chakula na si ya biashara hata kama yanauzwa.