Mbunge Condester Sichalwe: Tunauhitaji wa kinu cha kuchakata na kuyaongezea thamani mazao yetu

galimoshi

Member
Aug 5, 2023
9
6
Na Laudence Simkonda -Momba

Mbunge wa Jimbo la Momba Mheshimiwa Condester Sichalwe (Mundy) ameiomba Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko(CPB) kuanza kuona uwezekano wa kujenga kinu cha kuchakata mazao ili kuyaongezea thamani ndani ya wilaya hiyo.

Momba ni Halmashauri mkoani Songwe, ambayo wanakazi wake ni wakulima wa mazao kama vile Mpunga, Mtama, Mahindi, Ufuta, Ulezi na Alizeti.

Akizungumza na wananchi katika mikutano mbalimbali ya kutoa elimu ya kilimo biashara na chenye tija inayotolewa na timu ya wataalam kutoka wizara ya kilimo, Mheshimiwa Sichalwe, amesema kutokana na wilaya hiyo kuwa na wakulima wengi na uzalishaji mkubwa wa mazao kuna kila sababu CPB kama tasisi ya Serilika kuwa na kinu cha kuyaongezea thamani mzao kabla ya kupelekwa sokoni.

"Tuna sifa zote za kuwa na mashine za kuchakata mazao hapa, maana asilimi karibu 70 ya mazao yanayolisha miji ya Mlowo, Tunduma, Vwawa na Mbeya pia yanatokea Momba, sasa kama ni hivyo kwanini tusiwe na mashine zetu huhuhuku ili kuwasaidia wakulima kupata vipato" Mhe. Sichalwe.

Kwaupande wake Meneja wa uendelezaji wa CPB Joel Mwanga amesema mpango wa Serikali ni kuona wakulima wananufaika na nguvu zao, na ndiyo maana CPB imejenga vinu vya kuchakata mazao mbalimbali katika mikoa ya, Mwanza, Arusha, Iringa na Morogoro.

"Tuna kinu cha kusaga unga Iringa, kinu cha mafuta ya alizeti na kusaga unga Dodoma, kinu cha kukoboa mpunga Mwanza, Arusha tuna kinu cha kuchakata unga wa mahindi na ngano, pia tuna kinu cha Siagi mkoa wa Dar es salaam na kinu cha Mhogo Tanga" Mwanga.

Kwaupande wake afisa mwandamizi wa CPB Michael Ndonde amewakata wakulima kuunda vikundi ili iwe rahisi kukusanya mazao yao kwa pamoja na kuweza kukopesheka kwa urahisi.

"Ninachoweza kuwashahuri wakulima ni kujiunga katika vikundi, hii itatupa urahisi sisi CPB kuwakopesha kwa urahisi zaidi badala ya kusimama mtu mmojammoja" Ndonde.

Mwisho
 
M

mmojammoja inapendeza pia.
 
Back
Top Bottom