Bei ya mahindi yaporomoka ghafla, wakulima wapigwa butwaa

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,114
49,840
Bei ya mahindi Kwa gunia la kilo 100 imeshuka ghafla Mikoa ya Nyanda za Juu kutoka wastani wa sh. 80,000 Hadi sh.65,000.

Serikali nayo imesitisha kununua mahindi Kwa Sababu imenunua Tani za kutosha na pesa imeisha.

Sababu zikizotajwa za bei kushuka ni kukosekana Kwa wanunuzi kutoka Nje.

Mahindi Yataendelea kushuka zaidi maana Kenya ambayo ndio mteja mkubwa wa Tanzania wamepata mazao mengi mwaka huu ambapo na huko kwao Rift Valley bei zimeporomoka pia.

Na bei zitazidi kushuka miaka ijayo Kwa sababu Wazungu wa Zimbabwe wamerejea na Zimbabwe iliwahi kuongoza Afrika Kuzalisha mahindi.
---

Wakulima wapigwa butwaa bei ya mahindi kushuka ghafla​


Songwe. Bei ya mahindi katika masoko mbalimbali katika Mkoa wa Songwe imeporomoka katika kipindi cha mwezi mmoja ikilinganisha na bei zilizokuwepo mwezi Juni na Julai mwaka huu.

Mmoja wa wakulima aliyehojiwa na Mwananchi ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Sumbaluwela, Kata ya Ihanda wilayani Mbozi, Irine Nahaonga amesema amekuja kuuza kiasi kidogo cha mahindi ili aweze kutatua shida ndogo za nyumbani mwake, lakini amekuta bei imeshuka ghafla kutoka Sh85000 hadi 66,000 kwa gunia la kilo 100.

"Wanunuzi wenye stoo ambao wananunua mazao wametaka wanunue mahindi yangu kwa bei ya Sh66,000 badala ya Sh85,000 niliyokuwa nimeitarajia awali," amesema Nahaonga.

Aidha katika kipindi cha miezi Juni na Julai mwaka huu mahindi yalikuwa yakiuzwa kwa bei ya kati ya Sh80,000 na Sh84,000 kwa gunia lenye ujazo wa kilogramu 100.

Kutoka katika soko la mazao Mlowo wilayani Mbozi Tumaini Enson amesema katika kipindi cha mwezi Agosti mwaka huu bei ya Mahindi ilishuka kufuatia wanunuzi kutofika hivyo kusababisha mahindi kurundikana.

"Kuanzia juzi walau bei imeanza kuongezeka kidogo kutoka Sh66,000 hadi Sh72,000 siku ya leo hivyo kuna nafuu kidogo,” amesema Tumaini.

Meneja wa Soko la kimataifa la mazao katika Halmashauri ya mji wa Tunduma, Edward Silwimba amesema katika soko hilo bei ya Mahindi kwa siku ya leo ni kati ya Sh72,000 na Sh78,000 kwa gunia lenye uzito wa kilogramu 100.

Kuhusu sababu za kushuka bei katika soko hilo kipindi hiki tofauti na miezi ya Juni na Julai, mwaka huu amesema hali hiyo inafuatia kukosekana kwa wanunuzi wanaoingia hata hivyo kwa sasa amesema wameanza kuja mmoja mmoja.

My Take
Njia pekee ya kuwa na uhakika wa soko la mahindi ni kukuza ufugaji wa Kisasa Ili mahindi yatumike kama chakula Cha mifugo badala ya kutumia kama chakula Cha binadamu pekee.
 
Wazungu wa Zimbabwe ndio waliwafanya watu wa Zimbabwe kuwa mabonge kama watu wa Mbeya, wanawake wa Zimbabwe wamejaza kama wanawake wa Mbeya sababu kuu ni uhakika wa lishe.

Baada ya Mugabe kuwafukuza wazungu na mashamba Yao kubakia vichaka vya kufugia panya na nyoka wakaanza zaliwa generation ya watu wasio na lishe wenye miili ya njaa kama watu wa pwani.

We check kaburu huwezi kuta kaburu aliyesinyaa wote ni mabonge yaani two in one sababu ya lishe na Sio kujaza tumbo makapi.
 
Wazungu wa Zimbabwe ndio waliwafanya watu wa Zimbabwe kuwa mabonge kama watu wa Mbeya, wanawake wa Zimbabwe wamejaza kama wanawake wa Mbeya sababu kuu ni uhakika wa lishe...
Sasa wewe mkuu naona unaleta utani,ukisema lishe maana yake ni ugali,maharage na ngano ndio ilikuwa inalimwa sana na hao wazungu, kama ni hivyo mbona huku pwani tunatafuna sana hivyo vitu lakini hatunenepi,wakati kule mbeya wanapiga sana wali lakini mabonge?
 
Sasa wewe mkuu naona unaleta utani,ukisema lishe maana yake ni ugali,maharage na ngano ndio ilikuwa inalimwa sana na hao wazungu,kama ni hivyo mbona huku pwani tunatafuna sana hivyo vitu lakini hatunenepi wakati kule mbeya wanapiga sana wali lakini mabonge...?
Mbeya ni ndizi, kitimoto,viazi vya Mbeya, maharage, maziwa hapa lazima uwe bonge.
Ndo maana kina malafyale niangusage sambi zako wameshiba
 
Biashara ya mahindi ni biashara kichaaa angalau ya mchele
Mahindi Yana ushindani mkubwa,Kwa mfano juzi nimesoma makala kwamba Brazil imeipiku Marekani na kuwa Muuzaji mkubwa wa mahindi Duniani(corn au mahindi Lishe au mahindi ya yanga) Sasa unategemea bei itaacha kushuka?

Japo wao Marekani soko lao in terms of value limebakia vile vile Kwa sababu wanategemea sekta ya mifugo lakini pia uzalishaji kwao uliathiriwa na ukame.

Ndio maana nashauri bila kufanya value addition na kukuza sekta zinginezo basi hakuna siku bei ya mahindi itakuwa stable Kwa miaka hata 3 mfululizo, yaani tunategemea majanga.
 
Mahindi Yana ushindani mkubwa,Kwa mfano juzi nimesoma makala kwamba Brazil imeipiku Marekani na kuwa Muuzaji mkubwa wa mahindi Duniani(corn au mahindi Lishe au mahindi ya yanga) Sasa unategemea bei itaacha kushuka?
...
Kufa kufaana mahindi yakishuka Bei sisi wafugaji wa kuku chakula kinashuka Bei maana products kuu ni mahindi na soya.

Kiroba chakula Cha kuku kilo 50 ni elf 80 inazidi Bei ya gunia la mahindi.
 
Kiukweli hata mimi nimeshangaa kusikia juzi kuna mahali debe(kg 17) linauzwa 18,000 wakati lilikuwa limeshafika 22,000

Hii kazi ya kutunza mahindi eti tutauza bei ikipanda naona inataka kunishinda
Kilimo kinatabirika sana kwenye masoko, sema tumekuwa tukifanya vitu kimazoea bila mipango. Inabidi tubadilike ili tuliwin game
 
Kinachonishangaza hii serikari inawabana wakulima kwa kila sehemu,soko huru kwanini ummyime mtu fursa kuuza mahindi nje? Serikari ilipaswa kuangalia Kodi yake inapatikana basi mengine iyaache yakiwa huru.Huyu mkulima akigoma kulima next season sababu ya hasara nini kitatokea?
 
leo wanazuia mahindikuuzwa nje.
Kesho wanaruhusu mahindi kuuzwa nje.
Mkulima wanamfanya mpira wa kona

Wanasiasa ni wajinga sana hawana nia njema na kumuinua mkulima
Hakuna anaezuia mahindi kuuza Nje ya Nchi Bali Kenya kwenye soko wamevuna vizuri mwaka huu maana mvua ilinyesha na mbolea ya ruzuku walipata.
 
Back
Top Bottom