Naibu Waziri Kigahe: Anzisheni Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwenye mazao mengine.

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

Kigahe: Anzisheni Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwenye mazao mengine.

Naibu Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe ameitaka Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi kuzingatia maagizo ya Serikali ya kukamilisha taratibu za kuanzisha Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwenye mazao mengine.

Ameyasema hayo Juni 28,2023 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Stakabadhi ya Ghala mwaka 2023 yaliofanyika katika Viwanja vya Nanenane Mkoani Tabora.

"Ninaielekeza Bodi kuzingatia maagizo ya Serikali ya kukamilisha taratibu za kuanzisha Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwenye mazao mengine kama Chai, Pamba, Tumbaku, Mbaazi, Dengu, Choroko, Mahindi na bidhaa nyingine kama Mbao, Ngozi, na Asali ili kuwawezesha Watanzania wengi zaidi kunufaika na ushindani wa haki sokoni". Amesema Mhe.Kigahe.

Aidha, Amesema Mafanikio yameanza kuonekana kutokana na jitihada za Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala za kusimamia utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwenye mazao ya korosho, kakao, kahawa na ufuta kwenye Mikoa mbalimbali nchini na kusababisha upatikanaji wa bei zenye tija na ongezeko la mapato ya Wakulima Wadogo ikilinganishwa na hali kabla ya matumizi ya Mfumo huo".

Mhe.Kigahe ameendelea kwa kusema kuwa Maadhimisho ya Siku ya Stakabadhi za Ghala yana umuhimu mkubwa katika kukuza sekta ya biashara na masoko ya bidhaa nchini pamoja na kuwezesha biashara na kuipunguzia Sekta Binafsi gharama za kufanya biashara nchini kwani kwa kufanya hivyo ni utekelezaji wa maelekezo na dhamira ya dhati ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kuwahakikishia masoko ya uhakika Watanzania hasa Wakulima Wadogo kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala.

Aidha Mhe.Kigahe amewashukuru Wadau wote walioshiriki katika maadhimisho hayo na kupongeza ushirikiano uliojengeka miongoni mwa wadau wote muhimu wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala na kusema kuwa Ushirikiano huo ni muhimu katika kufikia malengo ya Serikali ya kuongeza ushindani wa soko kwa mazao na bidhaa za Watanzania.​

 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-06-29 at 13.18.57.jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-29 at 13.18.57.jpeg
    57.7 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-06-29 at 13.18.57(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-29 at 13.18.57(1).jpeg
    49.3 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-06-29 at 13.18.59(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-29 at 13.18.59(2).jpeg
    69.1 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-06-29 at 13.19.00(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-29 at 13.19.00(1).jpeg
    57.9 KB · Views: 3
Back
Top Bottom