Maximo anastahili mkataba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maximo anastahili mkataba mpya

Discussion in 'Sports' started by Sahiba, Mar 16, 2009.

 1. S

  Sahiba JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza kabisa natoa pongezi zangu za dhati kwa muheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania kwa kufanya maamuzi yha busara ya kumuongezea Maximo mkataba mpya wa mwaka mmoja.I think he is well deserve so far ameibadilisha sana timu yetu ya taifa mbali na mizengwe mingi isiyo na msingi anayokumbana nayo katika jitihada zake kikazi.Amethibitisha kuwa anatufahamu vilivyo tabia za wachezaji wa nchi yetu na I believe amedetermine kubadilisha namna soka linavyoendeshwa Tanzania.Matokeo na faida za mafunzo ya Maximo yatachukua muda kuonekana hususan kwa wachezaji wetu kwa kuwa wamezoea kudekezwa.Again Hongera muheshimiwa Rais.


  SAHIBA.
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Taarifa iluyotolewa na leodgar tenga leo inanyesh kuwa maxino ameongeza mkataba kwa mwaka mmoja zaidi, kwa hiyo ataondoka 2010 Julai
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Mar 16, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,751
  Likes Received: 4,973
  Trophy Points: 280
  ..sioni umuhimu wa kumlipa mapesa yote hayo halafu tunafungwa na timu ya taifa ya Somalia.
   
 4. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,273
  Likes Received: 4,258
  Trophy Points: 280
  Wale waliojitoa Stars wakitegema ataondoka sasa wataula wa chuya
   
 5. S

  Sahiba JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Tatizo sio kufungwa na Somalia tu ni system nzima ya uendeshaji soka kwetu kuanzia makocha na wachezaji hadi uongozi.Maximo analeta nidhamu ya kimataifa na wachezaji wetu wanaresist.Kwenye nudhamu ya mpira mchezaji hawezi kukurupuka tu akasema analotaka bila nidhamu lakini baadae wataona manufaa ya kile Maximo anachopreach hope watamshukuru.Mpira sio lelemama.

  SAHIBA.
   
 6. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Hapa naona giza tu. Hiyo extension ya mwaka mmoja ni kwa ajili ya friendlies? Maana hakuna mashindano (ukitoa ya CECAFA-challange cup)!
   
 7. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Maximo ni kocha bora katusaidia sana stars ila wabongo hatuna shukrani inaonekana kama vile kachukua ulaji wa watu......
  ....sahiba ningekupa thanks ila mwishoni umeharibu kwa kutoa hongera kwa jk....hapo tu umeharibu saaana kwenye post yako ya kwanza
   
 8. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  We still need Maximo.

  Ninaishauri TFF pindi utakapofika wakati wa kuchagua kocha mwingine, kigezo cha kusimamia nidhamu bila ya kutetereka kiwe ni kimoja kati ya vigezo muhimu.

  Hatutaki watovu wa nidhamu.
   
 9. S

  Sahiba JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Nimempongeza kwa sababu angesikiliza zengwe la wachezaji kama tulivyozoea asingemuongezea mkataba Rais ametathmini uwezo wa timu na ndio sababu ya maamu zi haya na hivi ndivyo mataifa makubwa yanavyoendelea tumezoea kuleta uyanga na usimba kwenye timu ya taifa Maximo amebadilisha.


  SAHIBA>
   
 10. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,273
  Likes Received: 4,258
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo kama hakuna mashindano ,unataka timu isiwe na kocha?
   
 11. M

  Middle JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2009
  Joined: Feb 7, 2007
  Messages: 243
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kesha fikia point of diminishing Maximo.aondoke zake watafute mwingine kwa miaka mitatu kwa ajili ya mashindano na cyo friend match.
  hana jipya tena sana sana ataleta siasa tu hapa Bongo
   
 12. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mkuu hiyo pointi yako hapo juu siafikiani nayo hata kidogo. Timu iliyofungwa na Somalia ni ile ile iliyoifunga Sudan, Uganda, Kenya na kwa kiasi kikubwa Ivory Coast, je hii pia ni matunda ya mfumo wa uendeshaji wa soka letu?

  Kama kocha wa taifa mwenye uhuru kwa kufanya atakacho, Maximo pia ni mdau mkubwa wa mfumo wa uendeshaji wa soka letu. Pindi timu inapochaguliwa na mpira kuanza kudunda, kocha mkuu ndiye mwajibikaji namba moja. Na hii ndio sababu timu nyingi hufukuza makocha badala ya wachezaji pindi mambo yakienda mrama.

  Mchezaji kusema kitu ni kitu kimoja, jinsi timu inavyocheza ni kitu kingine. Katika michezo nidhamu ina maana nyingi zaidi ya kukaa kimya na kufuata masharti. Nidhamu pia inahusisha jinsi gani timu inavyocheza, mbinu, majukumu ndani na nje ya uwanja n.k
   
 13. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Maximo kajitahidi kwa kweli, kafanikiwa (kwa msaada pia wa JK na wadau mbalimbali wa soka nchini) kuwaunganisha Watanzania katika kuishabikia timu yetu ya taifa. Kafanikiwa kufundisha mfumo wa soka ya haraka haraka na pasi fupi fupi. Kapata pia matokeo mazuri. Kwa ufupi wadau pamoja na Maximo wamerejesha heshima ya timu ya taifa kwa kiasi fulani.

  Tatizo langu mimi na Maximo ni kwamba, hana Plan B. Soka lake analolitaka ni pasi fupi fupi na mashambulizi ya kasi, kuna wakati kutegemeana aidha na uwezo wa wapinzani, uwanja, mahitaji ya matokeo, wachezaji gani tulionano, uchezaji huu hauwezekani.

  Tactically we are still naive, we have no shape, defensively we are a mess, the midfield all too often is non existent, and we still are hopeless in the air.
   
 14. E

  Endaku's JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2009
  Joined: May 25, 2007
  Messages: 322
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Watu niliowasikia binafsi wanamponda Maximo , Lakini tuangalie ukweli wa mambo nchi yetu bado tuna tatizo la washambuliaji (stikers) ndio maana timu ina uhaba wa magoli ya
  kufunga hilo binafsi nahisi si tatizo hasa la maximo moja kwa moja bali tuibue vibaji vya wachezaji toka chini ili kuwa na mfumo wa soka endelevu ,sio tu kutegemea maximo maana yeye anakaa na wachezaji muda mfupi saana , na hakuna mtu perfect tutaita kocha na kufukuza kila mwaka bila kuwa wavumilivu !
   
 15. S

  Sahiba JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kwa muda mrefu makocha wetu wa soka hawapewi nafasi za kuwa na final say katika timu wanaingiliwa na viongozi kiasi cha kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.Kwa kiasi kikubwa viongozi wa soka hawako too comfortable na Maximo kwa sababu hawakumuajiri wao ni mwajiriwa wa serikali.Hawa wachezaji yawezekana wanapata support kutoka kwa baadhi ya viongozi lakini the truth is timu inaonekana kuwa na hope in future hivyo individual players feelings if they are not productive they don't matter.Maximo hayuko pale kubembeleza penzi yuko kutusaidia sysy katika soka.Na inaonekana ametustudy akatujua kabla ya kuchukua kazi and to me kama tutamsikiliza tutabenefit sana.Kina Ally Bushiri wakitulia pale watajifunza mengi na Maximo akiondoka wanaweza kuwa katika makocha wa kutegemewa nchini.


  SAHIBA.
   
 16. senator

  senator JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2009
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133

  Watathimini wa soka wanaweza kumjudge maximo throug hizi game alizoiongoza stars.katika mechi 47 ilizocheza Stars chini ya kocha maximo mchanganuo wake ni kama ifuatavyo

  Taifa Stars imeshinda mechi...........21 sawa na 44%
  imefungwa mechi..........14 (30%)
  na imetoka sare mechi.................12 (26%)


  Mie kwa mtazamo wangu naona maximo anafaa kuendelea na kazi aliyoianza ingawa kwa mtazamo wa hapo juu kidogo sio picha mzuri ukichukulia maximo anachukua kitita cha $20,000/- kwa mwezi ni hela ndefu sana kama tukipata kocha mbadala mwenye qualities za zaidi ya macio maximo!!
   
 17. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Bwa Mkubwa, labda hiyo ndiyo conclusion yako - siyo yangu. Bado sijachoka kufikiri "i.e. Conclusion is the place where you got tired of thinking".
   
  Last edited: Mar 17, 2009
 18. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2009
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0  Tatizo hapa sio Maximo, tatizo ni kuanzia viongozi wa TFF hadi wa vilabu. si TFF wala vilabu wenye vitega uchumi ambavyo vingewezesha kupatikana kwa fedha za kuendesha programmes mbalimbali kama training za makocha, viongozi wa kisasa wa mpira na ligi kama ilivyokuwa Taifa cup enzi zile. kupata vipaji vipya TFF ingeazisha mashindano mfano wa kombe la FA, zamani kulikuwa na kitu kama hicho kama sijakosea. hapa wangeruhusu vilabu hata vya kijini kabisa kushiriki, nina hakika tungepata vipaji vipya vya kutosha,, tatizo fedha na viongozi hawako craetive kupata vyanzo vya hela wote wnasubiri mechi za simba/yanga waweke viingilio vikubwa au wapate hela za wahisani na zile za FIFA kwa stahili hii kamwe huwezi kuwa na timu ya taifa imara.
  Vilabu vingi havina viwanja wala majengo ya vitega uchumi,hakuna register ya wanacha, huwezi kuwa na vilabu vikubwa kama yanga/simba ambapo wanachama wanaopiga kura hawazidi 500!
  vilabu kamwe havitaendelea kwa fedha za wafadhili,sbb hao wafadhili wana agenda yao ya siri wao si wajinga wapoteze hela za burebure tu, viongozi wa vilabu wanategea kuendesha maisha yao kutumia vilabu, katika mazingira kama hayo unategemea nini, hasa katika nchi ambayo viwanja vyote vya ni vya aidha serekali au CCM?
  Klabu kama simba au Yanga wangeweza kabisa kuwa na majengo yao, achana na yale magofu ya kariakoo, wangejenga viwanja ili yale mapato wanayolipia gharama za uwanja pale taifa zingeingia kwao moja kwa moja, wangesini mikataba na makampuni ya nguo kutengeneza jezi/t-shrt/lesso/raba/kandambili/mikanda/skarf n.k zenye nembo yao na wangepata mamilioni ya kutosha ya kuwawezesha kuwa na academic schools za kuzalisha wachezaji na kuwauza na kupata a lot of money tatizo lilelile wako pale kwa maslahi yao sio ya klabu/taifa.
  katika nchi kama hii usitegemee maajabu kwa timu ya taifa wakati vilabu ni vibovu. TFF ilitakiwa igenerate fedha za kutosha kustimulate vyama vya mikoa na sio koconcentrate dar peke yake,sidhini hata kama wana plan ya next five years to come. Hata website hawana unategemea nn hapo.
  //
   
 19. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ingawa Maximo ni kocha mzuri hasa kwa mazingira ya TZ, wakati umefika wa kuacha matumizi yasiyo na lazima kwa serikali.

  Kama TFF (FAT) wana pesa yao na sio ya serikali basi wambakishe, otherwise pesa ya serikali itumike kupeleka vijana wetu huko huko Brazil, Ulaya n.k., kujifunza ukocha na sio kungojea vilivyokwishapikwa.

  Tuache utegemezi wa mpaka ubongo wa kusakata boli.
   
Loading...