tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 18,086
- 11,908
Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kumchosha mtu yeyote. Kwa utafiti binafsi niliofanya hivi karibuni, ndoa nyingi hapa nchini, na katika nchi nyingine za kiafrika, huingia migogoro au kuvunjika kabisa kwa sababu ya wanawake kuwa na uhakika wa ndoa ya kudumu, hasa hizi ndoa za mke mmoja (one wife, one husband). Mwanamke akishajua kwamba ndoa yake ni ya kudumu anakosa utii kwa mume wake.
Kumbuka hata biblia imeandika Enyi wanawake watiini waume zenu (Wakolosai 3:18-19). Lakini wanawake wa siku hizi wamekuwa na ngebe na ujuaji mwingi jambo linalopelekea ndoa nyingi kuvunjika, kuzalisha watoto wa mitaani na kuongezeka kwa uhalifu nchini. Na ukizingatia biblia pia inakataza kuvunjika kwa ndoa hadi kifo kiwatenganishe, hili pia huchangia kuwapa wanawake jeuri na kupelekea utovu wa nidhamu na utii kwa waume zao. Kila siku wanawake wanawaumiza waume zao bila sababu za msingi.
Wanawake wengi sasa hivi wanashindwa kuishi maisha ya ndoa, wengi wao wamekuwa wanaharakati zaidi katika ndoa kuliko kuwa walezi, hali ambayo imesababisha migogoro na kuvunjika kwa ndoa nyingi. Hawawasikilizi waume zao bali wanajisikiliza wao wenyewe na mashoga zao.
Kwa mujibu wa Wizara ya Sheria na Katiba wakati wakitoa taarifa yao bungeni mwaka jana ilibainisha kuwa idadi ya ndoa 26953 na talaka 122 zilisajiliwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA). Hii ina maana kuwa kila mwezi kuna taraka 14 zilizosajiliwa nchini sawa na talaka moja kila baada ya siku mbili. Kwa mkoa wa Dar es Salaam pekee ndoa zaidi ya 300 huvunjika kila mwezi.
USHAURI
Nakuomba mama Samia chondechonde uruhusu kufanyika marekebisho ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ili kuruhusu uwepo wa ndoa za mkataba. Hii itasaidia kuboresha nidhamu ya wanawake (vivuruge) katika kudumisha ndoa kwa kuepusha migogoro, kuvunjika kwa ndoa na uwepo wa watoto wa mitaani na kuongezeka kwa uhalifu nchini.
Mwanamke akishajua kwamba ndoa yake ni ya mkataba, madhalani mkataba wa miaka 3, lazima ajitutumue kuwa na nidhamu kwa mumewe kwa kuchelea kutoongezewa mkataba mpya pindi mkataba wa sasa ukifika tamati. Tunaona mfano kwa ndoa za wenzetu waislamu, wanaoruhusiwa kuoa wake wanne, ndoa zao ziko imara kwa kuwa wanawake wanakuwa na ushindani wa kumpenda mume tofauti na wakristo ambao wanabanwa kuwa na mke mmoja hadi kifo kiwatenganishe. Suluhisho pekee kwa tatizo hili ni kuruhusu ndoa za mkataba wa miaka mitatu mitatu ili kutuliza ngebe za wanawake wanaosbabisha ndoa kuvunjika ovyo.
Sote ni mashahidi kwa wachezaji wa mpira wanaoajiriwa kwa mkataba. Kila wakati mchezaji anajituma kwenye mazoezi ili awe fit aongezewe mkataba pindi mkataba wake wa sasa utakapoisha. Hata ndoa za mkataba zitakapoanza kuunguruma hapa nchini wanawake watajitahidi kulinda mikataba yao hivyo kupunguza idadi ya ndoa zinazovunjika. Naamini mama yetu Mh Rais Samia wewe ni msikivu. Hebu sikiliza kilio cha wanawake wenzako uruhusu ndoa za mikataba ili kuwanusuru na janga la uvunjivu wa ndoa na Allah atakulipa.