SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 43,703
- 60,825
Sawa mtoto wa kikopoWewe ni taira vuta bangi uliye athirika.
Sawa mtoto wa kikopoWewe ni taira vuta bangi uliye athirika.
Simchukii ila tabia yake ni haaminiki kwa yeyote mwenye akili Timamu.Una kila dalili za kumchukia tu TAL au kwa kifupi tuseme una roho mbaya tu 😂 dhidi yake binafsi!
Basi tuishie hapa maana aliyempiga Lisu risasi bado anatafutwa usije ukajitowelea kauli 😂😂Simchukii ila tabia yake ni haaminiki kwa yeyote mwenye akili Timamu.
Hivi unajihesabu una akili timamu?Simchukii ila tabia yake ni haaminiki kwa yeyote mwenye akili Timamu.
Unamuitaje mtu muongo kabla ya kuangalia ushahidi? Tabia mbaya sana hii.Acha uongo wewe. Thibitisha kama umekisema hiko.
Post in thread 'Dkt. Mpango Muogope Mungu, Wanasiasa wanazika na kukuacha! Umetegwa ukategeka' Dkt. Mpango Muogope Mungu, Wanasiasa wanazika na kukuacha! Umetegwa ukategekaWeka ushahidi
Nimesoma maoni ya watanzania kuhusu viongozi naona wameanza kutambua kuwa wao ndio waajiri wa viongozi.Hii ni hatua Moja kubwa ya kujitambuaMelo
Wananchi ni mabosi wa ukweli!Nimesoma maoni ya watanzania kuhusu viongozi naona wameanza kutambua kuwa wao ndio waajiri wa viongozi.Hii ni hatua Moja kubwa ya kujitambua
Tumwanini vipi PM na alishawahi kutudanganya kuhusu marehemu Magufuli?! Mazingira yanafanana na yaliyotokea juu ya VP.
Good.View attachment 2840103
Akizungumza East Africa Radio asubuhi hii, Disemba 12, 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo amesema Haki za wananchi zinazopatikana nje ya mtandao zinapaswa kutolewa pia ndani ya mtandao kwa kuwa ni haki za msingi zinazogusa maisha ya watu.
Kuhusu kutokutolewa kwa taarifa za alipokuwa Makamu wa Rais Dkt. Mpango, Melo amesema Makamu wa Rais ni kiongozi wa umma, analipwa kwa pesa za umma. Hata kama alienda kwa kazi maalum ni lazima wananchi waambiwe kwa kuwa analipwa kwa kodi zao. Hata kama hawatasema kaenda kufanya kazi gani lakini wananchi wanapaswa kujua kaenda wapi, kwa siku ngapi.
Akitoa maoni yake kuhusu hatua ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye kuwashughulikia waliotoa Taarifa za uzushi kuhusu kifo cha Makamu wa Rais, Melo amesema "Nimesikia Waziri atachukua hatua, ni sawa. Lakini wewe pia ukiguswa sheria hii ichukue mkondo wake, isionekane ipo kwa ajili ya kulinda viongozi pekee. Kuna ushahidi wa matukio mengi yametokea kwa wananchi na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa"
Ameongeza "Sheria ya Makosa ya Mtandao (Kifungu cha 16) inasema anayetoa taarifa za uongo kwa makusudi atashughulikiwa. Kazi ipo kwenye kuprove kama mtu alifanya kwa kusudi, lakini sheria hizi hazitumiki zikivunjwa kwa wananchi wa kawaida lakini zikivunjwa kwa viongozi ndio zinafanya kazi. Kuna "impunity"
Katika hatua nyingine, amebainisha kuwa kwenye matukio muhimu yanayohusisha viongozi wa kitaifa taarifa sahihi zinapaswa kutolewa. Kama kuna uzushi taarifa sahihi zitolewe kuondoa uzushi huo maana kukaa kimya huendeleza kusambaa kwa uzushi.
Melo aliulizwa pia ni kwa nini habari za uzushi kuhusu afya ya Makamu wa Rais ziliendelea kusambaa hata baada ya Waziri Mkuu kutoa taarifa. Alisema watanzania wana haki ya kutokumwamini Waziri Mkuu, yaliwahi kutokea enzi za Uongozi wa Hayati Magufuli, mazingira ya wakati huo na sasa kwa kiasi fulani yalikuwa yanafanana.
Mkuu uko sawa kabisa achilia mbali kiongozi kukaa nje siku 40 eti kwa kazi maalum...uko sahihi kabisa.
..Na kuongezea, hata kama PM Majaliwa angekuwa hajawahi kudanganya kuhusu Jpm bado unayo haki ya kutokumuamini kuhusu VP Mpango.
..VP kusafiri bila wananchi kupewa taarifa ni makosa. Na mimi sijawahi kusikia VP wa nchi yeyote ametumwa " kazi maalum. " Majukumu ya namna hiyo kufanywa na agents wasiojulikana, na sio VP ambaye dunia nzima inamjua.
Pia aliyekuwa makamu wa Rais wakati huo alikuwa bize akifanya ziara ili kutoa picha potofu kuwa Hali ya Rais haiko mashakani!!Max amezunguka tu, ila anachosema ni kwamba serikali haiaminiki
Hiyo hadhara ndo imewapa dhamana ya uongozi, kama hawataki kuwajibika kwa hadhara iliyowapa jukumu hilo wakaongoze misukule.Siyo kila kitu cha kusemwa hadharani nyie mabwege