Maxence Melo: Pole sana Tundu Lissu, Mungu akuponye!

Status
Not open for further replies.
Nawalaaniwe wote walimpiga risasi wao na vizazi vyao wafe kwa kupigwa risasi za vichwa tu..

Malipo watayapata hapa hapa duniani haijalishi unacheo gani au mkatili kiasi gani. Mungu habagui atasikiliza huzuni ya watanzania na kilio chao. Atawalipa tu.
 
Nakumbuka ambavyo mwaka 2008 nilipokamatwa ikidaiwa mimi ni GAIDI ulijitoa na kuja kuwa wakili wangu bila kuombwa na hata hukuniomba senti. Wakati huo hukuwa katika "active politics".

Maisha yakaenda mbele, ukawa mwanachama wa JamiiForums kwa jina halisi (verified Tundu Lissu) na kuniambia unataka kuonesha support kwa huduma tunayoitoa.

Disemba 2016 nilipokamatwa kwa madai ya kutotoa 'ushirikiano' kwa vyombo vya dola, hukuniacha ukaja hata bila kuitwa. Ulinisisitiza "Max, tumetoka mbali hata kabla sijaingia kwenye siasa, leo unanikimbia? Sikuachi uumie, nitakutetea bure na hata kufunga safari toka Dodoma kila kesi yako itakapotajwa." Tukacheka na kutiana moyo!

View attachment 583487

Ni wiki mbili zilizopita tulipopiga picha hii, hapa ulikuwa unarekebisha kalenda yako kuhakikisha tarehe ya kesi yangu unakuwepo ili kuhakikisha sizamishwi na walionipania (na nakumbuka ulithubutu kuwaambia usoni mbele zangu).

Habari ya wewe kushambuliwa kwa risasi (ni wazi waliutaka uhai wako) imeniumiza sana, imenitia simanzi kuu na kunifanya nikose la kufanya zaidi ya kupata japo dakika kadhaa kukuombea (the best I could do).

I happen to know you Tundu, nje ya siasa wanazoona walio wengi! Mungu akusaidie upone haraka na kukurejeshea afya yako hata kuyaponya majeraha yako.

Mungu wetu ni mwingi wa huruma; kama amekuepusha na kifo leo - atakuponya!

Get well soon brother...

Amen
 
Nimeamua nikugonge li like mwanangu mello

Hakika yesu ni mwema mpambanaji wetu atapona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
- Jambo kubwa ambalo huwa linanishangaza ni kwamba:

. Wapinzani siku zote ni watu wenye haki na wala hawajawahi kukosea hata siku moja. Kila kitu kwao ni sahihi na wao huwa wanaonewa tu

. Huwa wanaamini kuwa siku zote Mungu ni wa kwao tu !

. N.k
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom