Mawazo yenu wakuu

Mawazo yenu wakuu

Amon Lisa

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2018
Posts
464
Reaction score
1,169
Natumai ni wazima wakuu zangu

Ni siku mpya tumeweza kupata zawadi ya uhai na uzima, ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ndio mpaji wa vyote.

Kuna wagonjwa mahospital, wafungwa magereza, vita, majanga ya asili, vifo nk.. ukiona umeamka huna changamoto hizo, inakupasa kushukuru sana. Hakuna hajuae kesho.

Turudi kwenye lengo la uzi, kijana wenu nimeamua kupandisha uzi kutokana na masaibu ninayopitia mara kwa mara ( uchumi wangu mbovu sana) kupiga dash kwa siku ishakuwa kawaida.

Hivi ninavyongea mtungi wa gesi umenikatikia ilikuwa ndio mkombozi wangu nikizama kwa mangi nikakopa nina uhakika wa kuishi siku kadhaa. Sasa utambi umekata na sina namna nyingine kwa sasa.

Jinsi mtakavyoguswa kwenye hii changamoto yangu nitashukuru.

Ahsante wakuu zangu, karibuni kunishika mkono 🙏🏾
 
Wakati mwingine hali ngumu tunazopitia kwenye maisha yetu si kwa sababu tunastahili, hapana. Wakati mwingine ni kwa ajili ya kutujenga, kutufundisha, na kutuandaa kwa kile kinachokuja mbele yetu.
 
Wakati mwingine hali ngumu tunazopitia kwenye maisha yetu si kwa sababu tunastahili, hapana. Wakati mwingine ni kwa ajili ya kutujenga, kutufundisha, na kutuandaa kwa kile kinachokuja mbele yetu.
Ahsante mkuu kwa kunipa moyo kwenye nyakati zangu hizi.

Nime screenshot haya maneno mazito kwa matumizi ya baadae
 
Wewe mtungi wa gesi umeisha unawaza

Wale wanaotumia mkaa mbali na donee ya kitaa kwa wahuni ili maisha yaende.?

Mdogo wangu kwa nia njema kabisa pendelea kujishusha hutosumbuka.!

Kweli hata dhoruba ipige kiasi gani juu ya baharia walio chini wayo sio shida zao

Hii ni kanuni ya kujipata na mafanikio

Usijihesabu kabla hujahesabiwa
 
Ninashukuru kwa ushauri
hapa nilipo hawaruhusu jiko la mkaa
Nimekuwa natumia gesi, hata jiko la mkaa sina kutokana na masharti ya wenye nyumba
 
Back
Top Bottom