Mawazo kwa vijana mtapotoshwa kuwaangalia wasanii kwa maendeleo yenu

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,606
8,744
Nawapa mawazo ya bure wadogo zangu wa miaka 18-35. Kwasababu wasanii wetu hasa wa musiki wanafanya vizuri jamii hasa wanasiasa watawatumia wenyewe kwa manufaa yao binafsi. Lakini kwa mawazo yangu acheni kuwafuata wasanii na kushinda mitandaoni kuangalia maisha yao na kutaka kuiga badala yake angalieni zaidi vijana waliofanikiwa kwenye biashara, elimu na hata ajira.

Kuna vijana wengi wana mafanikio kwenye biashara na kufungua biashara tofauti, wengine ni viongozi kwenye makampuni hao ndio wakuwaiga na sio wasanii ambao maisha yao wengi ni fake na vilelevile yanategemea vipaji maalumu. Msiko kuwa makini na kuwa vijana wa kulishwa maneno na youtube videos mtapotea kizazi chenu.

Kizazi chenu mnashindana na dunia nzima kwa miaka hii unaweza kufanya kazi popote duniani kama una ujuzi na mtandao. Tumieni muda huu kujaribu kufanikiwa kibinafsi, kuwa wabunifu na kujifunza vitu mbalimbali ambavyo mna weza kupata hata kwa bure kwa dunia hii ya mitandao. Jiulize kila siku umejifunza nini, msiwe watu wa kulalamika kila siku, na msiache kufikiria kufanikiwa kwa njia za ubunifu.

Nakumbuka wakati wetu tuliweza kutafuta shule nje kizazi chetu na kuwa waangaikaji sana lakini hatukuwa na watu wa kutudanganya kama siku hizi. Kama sisi tuliweza wakati ule miaka ya 1997-2003 kutafuta shule bila mitandao, vyuo vichache n.k inawezekana kabisa nyie mna weza kwenda mbali zaidi lakini tatizo macho yenu yako pabaya. Msiache kujiuliza je familia yako binafsi inahitaji nini na unatakiwa kufanya nini kufanikiwa. Msisubiri serikali kwa maendeleo yenu binafsi.

Tanzania siku hizi mambo ni rahisi kuliko zamani. Barabara zipo siku hizi nendeni kafanye kilimo, jifunzeni sofware kwa wasomi ili muweze kufanya kazi hata za nchi nyingine kama India wanavyofanya, unaweza siku hizi ukafanya order ya vitu online kwa maduka yenu, unaweza ukawa dealer...

Lakini acheneni na fikra za maisha ya wasanii na kujidanganya kila siku badala yake tafuta mtu ambaye unaweza kumuiga na ukiomba kuelekezwa kuna wengi watakusaidia
 
Back
Top Bottom