SoC01 Mawazo huru kwetu wote

Stories of Change - 2021 Competition

AnonymousAlbin

New Member
Sep 16, 2021
1
0
Nina mashaka juu ya haya ambayo sisi binaadamu tunavyozidi kukua,kubadilika,kughadhabika na utu pia kututoka.

UBINAAMU
Tunaishi katika hali ambazo jamii ndio tunayo-iogopa zaidi kuliko hali zetu za afya. Ninayo mengi sana ambayo nitayazumgumzia ningependa pia kwa sisi wote ambao tunahisi utu una uthamani kuliko vinginevyo tukae tujifakari ni namna gani ambayo tunaweza kuongoza vijana,wazee pamoja na watoto kuhusu masuala ya utu wetu

Kilio changu cha kwanza ninakipeleka kwa watoto,vijana pamoja na wazee ambao ni walemavu wa ngozi zao(albino).Hivi ni kwamba ya siri na ya chini yanayofanyika bado waja wanaamini hawastahili kuishi maisha wanayoyaishi binaadamu kama wao.Watoto wetu wanasoma wapo mashuleni ila wanakumbana na kutengwa kutokana na hali za ngozi zao je hakuna umuhimu wa sisi watu wazima kuwaelewesha watoto wetu kwamba hata wale ni wenzetu.

Sio mashuleni hata majumbani mzazi upendo kwa mtoto wako huna ni kwa vile tu hayupo sawa na wewe yule au wanao wengine; tumeshawahi kuwaza wana maumivu kiasi gani mioyoni mwao kwasababu ya matendo yetu.
Tukae tujitafakari tutafute njia za kuwasaidia waondokane na unyanyapaa wanaopata wanetu,wazazi wetu pamoja na jamaa zetu wenye ualbino.

WAZAZI
Kuna mabinti tunaowafahamu,binaadamu kufanya makosa ni kawaida ila tu alitambuae kosa lake ni yule ambae ataomba msamaha kwa alilofanya.Dada zetu wanaojifungua kabla ya ndoa;wazazi mnakaa kifua mbele kumfukuza mwana,hamuoni tabu?

Wapi anatakiwa aende binti,kuna msemo unaosema mtoto akinyea kiganja hukikati unakiosha.Kama ni makosa yameshatokea je hatuwezi kuwa na misamaha tukawasaidia mabinti zetu kwa uwezo wowote tulionao?Athari ambazo angepata angewaza kutoa mimba wote tunazijua basi tukae nae vizuri,tusiwapotoshe na kuona wamefanya kosa kubwa sana katika jamii maana hata ndoa zina siri nyingi,natumai mnanielewa.

DADA ZETU
Kilio changu kipo nanyi,munapopata nafasi ya kusoma,kujishughulisha basi nawaombeni mtumie hio nafasi vyema.
Kuna ndugu zenu waliitamani ila hawakuifikia.Hakuna mteremko katika kufanikiwa juhudi zako ndizo huleta matunda hata ziwe ndogo vipi kuna siku zitakufikisha tu.

Msiparamie waume za watu wamefunga ndoa zao na wake zao,mkawaumiza wa undani wao wanaowavumillia shida zao kwa matakwa yako binti ya kupita na dunia.

Jiheshimu, heshima yako ni kitu kikubwa sana katika maisha yako na kwa mwenza wako pale mungu atakapokubariki.
Musikurupuke mda huwa hausubiri ila kama una malengo pia hauchelewi,muinuane musaidiane hvyo ndivyo mbele mutasonga. Yale ya vibarazani mara kapita nani kafanya nini kwa mwafulani hayatawatoa ubayani kuwapeleka pemani mujichunge mwili,akili pamoja na ndimi zenu.

KUSAIDIANA
Iwe mwanaume ama la mwanamke kutoa ni moyo na wala si utajiri.Ukitoacho leo huenda ndio nuru ya kukuangazia mambo yako kesho,tujitahidi kusaidia kwa mawazo,kwa fikra kwa uwezo ili wote tusimame imara,wenye afya na maendeleo kwenye jamii zetu.

Ni hayo tu kwa uchache niliowasilisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom