Mawaziri wenye PhD Feki hawa hapa!

Mawaziri wenye PhD Feki hawa hapa!

WC, Hii nchi ngumu sana...

Tumeshaona wasomi feki
Bidhaa kibao feki
mikataba feki
kesi feki
dhamana feki
Raia feki
ahadi feki
Mitihani feki

Sasa subiri utasikia
Mashtaka feki
makaripio feki [kutoka kwa mkuu]
ahadi feki


sijui tumebakiza nini tena feki

Kenya ni nchi ya kitu kidogo... Tanzania iwe nchi ya mafeki tu!
Wazili mwenyewe inawezekana akawa feki...........Maana pengine anayemdhania kuwa ni baba yake, naye siye. Hata huyo mama yake amemnunu kwa nesi hospitali akiwa mchanga.........

Unanunua cheti feki........... Mchine iliyotengeneza hicho cheti nayo ni feki.........

Nafasi ya uwazili umepewa kwa documents feki..................

Naibu waziri wako naye ana vyeti feki..................

Unapelekwa mahakamani nako jaji ana vyeti feki.....................

Polisi aliyekukamata ana vyeti feki vya CCP Moshi.................

Askali magereza anayekulinda huko gerezani ana vyeti feki vya pale Ruanda magereza mbeya.....................

Unapelekwa mahakamani kwa hati feki...................

Upelelezi unacheleweshwa ili utengenezwe ushahidi feki....................

Kesi yenyewe ni feki, yaani umebambikiwa....................

Mahakama imejengwa na mkandarasi feki.........................

Unafungwa kifeki feki tuuuuuuuu.....................

Yaani kila kitu feki.........................

..............feki.....feki .........feki ..........

Hao inabidi wapelekwe mahakamani feki ili wakashindwe kutaja hata monita au classmates wao..........
 
Mimi sijaelewa kwamba hawa waheshimiwa wamenaswa (kukamatwa) au "redhanded" na hivyo vyeti au wamegundulika kuwa na vyeti visivyotambulika Tanzania.

Nafikiri kichwa cha habari kingebadilishwa na kuwa "mawaziri sita wagundulika kuwa na na vyeti visivyotambulika Tanzania".

Huo ni mtazamo wangu.
 
Wanaume wote wana zana juu ja lips za mdomo. Yaani wote wana Muche aka mustachi. Kiboko yao ni Mbunge wa Sikonge, yeye ni kama Mugabe aka Black Hitler hahaaaaa haaaaa, Sikonge tuna .....

10001132.jpg


Weka mkono juu na vidole viwe mbele na unasema 'Hail Nkumba".
 
kisha najishangaa kwa nini ninasota kutafuta Phd wakati wenzetu wanambinu za kupata bila ya kusota, na kupongezwa kwao kupewa uwaziri!

Utajiju shosti aliyekuambia bongo ukitaka kutoka lazima uwe na Ph.D ni nani?! Huku ni akili kumkichwa tu!
 
The funny part of this debate is that many if not most people fail to separate wheat from chaff. How do you put a forgery case in the same page with presenting genuine but unrecognized certificates?
...Mhhh! jamani vitu vingine humu jamvini hebu tumwachiye yule mrithi wa 'Pundit'-Blue ray
 
The funny part of this debate is that many if not most people fail to separate wheat from chaff. How do you put a forgery case in the same page with presenting genuine but unrecognized certificates?

Wanahabari, Wanasheria, Wasomi wasio feki, Wanasiasa wa Upinzani na wa CCM, Watanzania wote: Tuungane tukatae huu uongo na wakutufanya sisi sote wajinga! Let us act now! Let us bring them to justice! Tuwafungulie mashtaka...
 
Nimeshasema mara nyingi, jitihada zozote za kupambana na hawa watu ni kupiga upepo! Watanzania huwa tunalalamika sana vitu mabavyo hatuna msingi navyo.

1. Nani anajua standard requirements za PhD zilizowekwa na serikali ya Tanzania?
Kuwa ichukue muda gani na ufanye nini?
2. Je wale walio na PhD Tanzania je wanasajiliwa? wakishasajiliwa wanatakiwa wafanye nini ili kutete PhD zao?
3. Je wale walio na PhD ambazo ni genuine do they have any remarkable achievements kiasi cha kupelekea kuanza kulalamia kuna vihiyo

Nijuavyo

1. Lazima yawekwe malengo na standard kuwa hawa PhD holders wawe wanafanya nini, mathalan, watakwe kufanya publication kila mwaka, na ikitokea mtu hatafanya hivyo basi asijulikane kama ana PhD.
2. Iwekwe sheria kuwa mtu hatakiwi kujiita Dr. mpaka apitie hatua kadhaa.

Matatizo

Katika dunia hii ya globalisation, people can study anyhwere katika chuo chochote , na sahau kuhusu accredition , e.g chuo cha AIU(Atlantic int. university) hakina accredition) lakini chuo cha MUST university ambazo wanatoa degree kuwamuda mfupi kina accredition AIO!

Sipati picha nchi kama ya Nigeria wanaishi vipi na vyeti vyao feki, au taifa kama USA lenye watu mil.300 wanaishi vipi na wenye vyetii feki.

UKija kwenye survival of fittest, basi wenye nguvu tu, I mean wenye PhD genuine ndio watakaosurvive.

Ukiona taifa lenye wenye vyeti feki wanatamba, basi tatizo ni kuwa serikali haiwathamini wenye degree genuine! na ya kuwa elimu yetu imetawaliwa na kuajiliwa zaidi na kuwa na vyeti vizuri, why bother then to pass through painful process of four years to get PhD that no one gonna use you! hata kukupa fund ya reserach haupati!

Let go to work
 
Wanaume wote wana zana juu ja lips za mdomo. Yaani wote wana Muche aka mustachi. Kiboko yao ni Mbunge wa Sikonge, yeye ni kama Mugabe aka Black Hitler hahaaaaa haaaaa, Sikonge tuna .....

10001132.jpg


Weka mkono juu na vidole viwe mbele na unasema 'Hail Nkumba".

Hail Nkumba

Hail Nkumba

Hail Nkumba


ohh mbavu zangu jamani. Hii JF itanipeleka ER one of these days
 
No wonder nchi inaendeshwa kizembe zembe kama viongozi wenyewe ni wa vyeti vya kugushi maendeleo yatatoka wapi. kazi kweli kweli
 
Wakuu, hawa jamaa HAWANA vyeti FEKI bali elimu waliyonayo NDIYO FEKI,

Siku hizi unaweza kusoma PHD on line three weeks na jamaa wanakutumia cheti chako, sasa wewe unategemea nini kutoka kwa hawa MAZUZU.
 
Bunduki bila risasi ....... na msumeno butu utakataje !!!
 
Mimi hawa walio fib resume zao n.k. wala siwalaumu sana. Wakubeba lawama hapa ni yule anayewapa hizo nafasi.
 
Kama kweli viongozi hawa wamepata vyeti bila kustahili..siwaelewi kwa maana nyadhifa zao hazihitaji PhD. Wangeingia darasani tu na kusoma.Kuna hata Open Uni na distance learning programmes kutoka Uni za kueleweka.Pia ninaowajua kwenye hiyo list iliyowekwa hapo..mfano Mary Nagu ni mtu anayejiweza sana kiakili -she is very smart. intelligemt and sharp. I can say with confidence that she is above average hivyo kufaulu isingekuwa ishu.Kutumia short cut kama hivi ndio mwanzo wa kujidhalilisha.Serikali inastahili lawama kwa kushindwa kuweka STOP to this PhD madness! U dont need a PhD TO BECOME A POLITICIAN.
 
Wala sishanga kwani hata maamuzi yao bungeni ni ya zimamoto.Ndio maana Taifa linarudi nyuma kielimi na Kiuchumi baada ya kusonga mbele.Chaajabu zaidi serikali inafanya kazi gani kuhakikisha viongozi hawagushi vyeti kwa kuwahakiki vyeti vyao kabla ya kuwa viongozi.

Hahahahahahahahha Mungu ibariki Tanzania na usiwabariki viongozi wala rushwa mafisadi na wanaofoji vyeti
 


Dk. Chegeni alipoulizwa na mwandishi wa Nipashe juu madai ya elimu yake, naye alimuuliza mwandishi kuwa: “Mtu akikuuliza mimi ni mume wa mama yako utajibu nini?” Lakini mwandishi alipomtaka ajibu swali aliloloulizwa, aliongeza: “Kama mtu huyo amesema ana haki ya kusema.”

Huyu naye ni Doctor of Phylosophy au, Maneno gani haya yanatoka katika kinywa cha Waziri jamani ee
 
Serikali inastahili lawama kwa kushindwa kuweka STOP to this PhD madness! U dont need a PhD TO BECOME A POLITICIAN.

Hawa ndiyo wanatakiwa kuwa Role model, Kwa nini basi tuwalaumu wanaoiba mitihani ya Taifa kama Viongozi wao wanatafuta U-PHD kwa njia za Mkato hivi, ndiyo maana tunajenga Taifa linalopenda Njia Rahisi na Fupi kuelekea katika Mafanikio
 
Wengine walisomea degree za usalama kule ulaya mashariki ENZI ZA MWALIMU, na vyuo vyenyewe vilifungwa sasa sijui tutathibitisha vipi.
 
Hili suala tumelijadili mara nyingi sana hapa JF. Kuna haja ya kutenganisha kati ya kugushi vyeti na kusoma vyuo visivyotambulika.

Labda kama mwandishi ndiye kaandika vibaya; kwa aliyechunguza kama atasema hawa jamaa wameforge vyeti, wanaweza kumshinda kirahisi. Walichofanya wao ni kutumia titles ambazo hazilingani na elimu yao kama inavyotambuliwa na taasisi mbalimbali za elimu.

Yule wa wilaya moja, nafikiri ni mkoa wa Mara, yeye ndiye ka forge cheti maana ni kweli hajawahi kusoma popote. Pia huenda Lukuvi naye kama ni kweli hajawahi kusoma popote.

Hao akina Kamala wanavyo hivyo vyeti na vimetolewa na institutions ambayo zipo kihalali lakini tu elimu wanayotoa haikidhi requirements zinazotakiwa kwenye elimu zao.

Sidhani kama spika Sitta anaweza kufanya lolote kwenye hili; wanaoweza kufanya jambo ni wananchi ambao baada ya kujua ukweli huu wanaweza kuwawajibisha wabunge wao. Pia kwa rais aliyewapa kazi, anaweza kuona hawana sifa tena na kuwaondoa kwenye hizo nafasi zao.

Amenifurahisha Mwambalaswa anayekimbilia kwamba ni mafisadi ndio wanamtuhumu. Kwanini ashindwe kujibu swali la wazi kama hilo?
Ramadhani Kihiyo aliwajibishwa na hawa wanatakiwa kuwajibika.wamemdanganya Rais,Bunge na wananchi.
Mathayo David hana PhD.
 
Wengine walisomea degree za usalama kule ulaya mashariki ENZI ZA MWALIMU, na vyuo vyenyewe vilifungwa sasa sijui tutathibitisha vipi.

Wazungu si kama sisi. Wanatunza kumbukumbu wale wee acha tu. Utashangaa chuo hakipo ila document zake zote bado zipo.

Mie nilisoma Mazengo miaka hiyo. Sijui kama kumbukumbu zake zimetunzwa au wameshazichoma moto.
 
Back
Top Bottom