Mawaziri wenye PhD Feki hawa hapa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri wenye PhD Feki hawa hapa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, Oct 19, 2009.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mawaziri sita wanaswa na vyeti feki

  • Vyeti vyao vya elimu vyadaiwa vina utata
  • Yumo Mkuu wa Mkoa na wabunge watatu
  • Orodha yawasilishwa kwa Spika wa Bunge
  [​IMG]
  Dk. Mary Nagu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko.

  [​IMG]
  Dk. Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa-JKT)

  [​IMG]
  Dk. Makongoro Mahanga, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana.

  [​IMG]
  Dr. David Mathayo David, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika.

  Mawaziri sita na wabunge wanne, wametajwa kuwamo katika orodha ya watuhumiwa 19 wa walighshi vyeti vyao vya elimu.

  Utafiti huru uliofanywa na Mwanaharakati, Kainerugaba Msemakweli kwa msaada wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), katika kipindi cha mwaka mmoja; umebaini kwamba wanasiasa hao wametumia vyeti vya kughushi na kuwasilisha katika ofisi za umma kwamba wana elimu hiyo, kitu ambacho si kweli.

  Utafiti huo ulianza kufanyika Juni 25, mwaka jana hadi Oktoba 9, mwaka huu katika nchi za Marekani, India na Uingereza, ambako vigogo hao wanadaiwa kuwa walisoma na kupata shahada hizo.

  Baada ya kubainika kwamba hawana sifa za elimu wanazodai kwenye wasifu wa elimu zai, ripoti hiyo imekabidhiwa kwa Ofisi ya Spika wa Bunge.

  Kuwasilisha nyaraka za kughushi katika ofisi ya umma ni kinyume cha Katiba na sheria za nchi.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Msemakweli aliwataja mawaziri hao kuwa ni Dk. Mary Nagu (Viwanda, Biashara na Masoko), na Dk. Diodurus Kamala (Ushirikiano wa Afrika Mashariki) kuwa miongoni mwa vigogo wanaohusika na kashfa hiyo.

  Pia, kuna waziri mwingine mmoja ambaye jina linahifadhiwa kwa sababu hatukuweza kumpata kuzungumzia tuhuma zake jana.

  Mbali na hao, pia Msemakweli aliwataja manaibu waziri, Dk. Makongoro Mahanga (Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana), Dk. David Mathayo David (Kilimo, Chakula na Ushirika) na Dk. Emmanuel Nchimbi (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa-JKT) kuhusika na kashfa hiyo.

  Wabunge, ambao wametajwa na ripoti hiyo, ni pamoja na William Lukuvi (Ismani-CCM), ambaye pia, ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Victor Mwambalaswa (Lupa-CCM) na Dk. Raphael Chegeni (Busega-CCM).

  Kuna mbunge mwingine ambaye pia alitajwa kwenye kashfa hii na kwa kuwa jana hatumpata kuzungumzia suala hilo, jina lake tumesitiri kwa sasa.

  Vigogo hao wanadaiwa kuwa walighushi taaluma kwa baadhi yao kujiwasilisha kuwa wana shahada za masuala ya kimataifa na diplomasia, biashara na utawala, wengine shahada za uzamili, udaktari wa falsafa, na wengine dhahada za ualimu nakadhalika, wakati si kweli.

  Msemakweli alisema katika taarifa aliyowasilisha kwa ofisi ya Spika aliomba iwawajibishe vigogo hao kwa kashfa hiyo.

  Alisema vigogo hao waliwaghilibu wananchi wa majimbo wanayoyawakilisha na kuwafanya wapate ubunge na kwamba, kwa kutumia shahada hizo za kujipachika, wameweza kuaminiwa na kupewa nafasi za kisiasa na kiutawala.

  Alidai ana ushahidi wa kutosha juu ya madai anayoyatoa dhidi ya vigogo hao kwani ameyafanya utafiti wa uhakika na kwamba, kigogo yeyote atakayehisi kuwa ameonewa aende kwenye vyombo vya sheria na yuko tayari kwenda kuthibitisha madai yake.

  Alidai Lukuvi alighushi sifa za taaluma kuwa ni msomi mwenye shahada ya masuala ya kimataifa na diplomasia wakati elimu yake ni darasa la saba na ualimu wa shule ya msingi.

  “Hajawahi kuingia darasa lolote la digrii (Shahada) wala kufanya mtihani wowote wa digrii wala kusoma digrii yoyote, wakati wowote, katika maisha yake yote na mahali popote duniani,” alidai Msemakweli.

  Alisema wakati anaiwakilisha Tanzania nchini Namibia katika mkutano wa wabunge wa Jumuiya ya Madola, Lukuvi aliwasilisha taarifa za kuhusu taaluma yake kwa kudanganya kuwa yeye ni msomi mwenye shahada ya uzamili katika masuala ya biashara na uongozi.

  “Taarifa za kweli ni kwamba baada ya kumaliza elimu ya msingi na kuishia darasa la saba mwaka 1975 Mheshimiwa Lukuvi alienda kusomea ualimu wa shule za msingi katika Chuo Kikuu cha Ualimu, mkoani Tabora,” alisema Msemakweli.

  Alisema Dk. Mahanga “…ameghushi sifa za kuwa ana shahada ya uzamivu (daktari wa falsafa) wakati hajawahi kusoma shahada hiyo wakati wowote na mahali popote duniani”.

  Msemakweli alidai Mwambalaswa ameghushi sifa za taaluma kwamba ana shahada ya uzamivu ya biashara na utawala (MBA) wakati hajawahi kusoma shahada hiyo.

  Alidai Dk. Nagu ameghushi sifa za taaluma na kujiwasilisha kwamba ana shahada ya udaktari wa falsafa wakati hajawahi kusomea udaktari wowote na mahali popote.

  “Yeye amesoma na kuishia shahada ya pili kwa kutumia shahada hiyo ya kujipachika ameweza kuaminiwa na kupewa nafasi za kisiasa na kiutawala wakati… Katika maisha yake hajawahi kusomea udaktari wa aina yoyote,” alidai Msemakweli na kuongeza:

  “Amefanya …kumdanganya Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Taarifa katika Ofisi ya Mheshimiwa Spika na ambayo Mheshimiwa Spika anazo zinaonesha kuwa Mheshimiwa Mary Nagu ni msomi mwenye digrii ya daktari wa falsafa wakati hajawahi kusoma udaktari wowote katika maisha yake yote.”

  Msemakweli alidai “Dk. Nchimbi ameghushi sifa za taaluma na kujifanya kuwa ana digrii ya Uzamivu (Ph.D). Hivyo kujipachika sifa za udaktari,” alisema.

  Alidai Chegeni ameghushi sifa za taaluma na kujiwasilisha kwamba ana digrii ya uzamivu (Ph.D) na hivyo kujifanya dokta wakati hajawahi kusoma digrii yoyote ya udaktari au uzamivu, wakati wowote na mahali popote duniani na vyeti alivyonavyo kuhusu elimu hiyo ni vya kughushi.

  Msemakweli alidai: “Dk. Mathayo ameghushi sifa za taaluma kwamba ana stashahada ya juu katika masuala ya mahusiano ya kimataifa wakati hajawahi kusoma stashahada au diploma hiyo wakati wowote na mahali popote pale duniani.”

  Kwa upande wa Dk. Kamala, Msemakweli alidai: “Ameghushi sifa za taaluma kwamba ana digrii ya uzamivu (Ph.D) wakati hajawahi kusoma digrii hiyo, wakati wowote na mahali popote duniani.”

  Nipashe iliwasiliana na vigogo hao, jana kupata maelezo yao na kwanza alikuwa ni Lukuvi ambaye alikanusha vikali kuwahi kusomea au kudai kwamba, ana shahada ya biashara na kusema kuwa: “Mtu anayedai hivyo ametia chumvi.”

  Alisema aliyonayo ni diploma ya sayansi ya siasa kutoka Urusi na shahada ya taaluma ya Kimataifa kutoka Marekani.

  “Sijawahi kusoma biashara na wala sina Masters (shahada ya pili) ya biashara. Kama ana ushahidi athibitishe,” alisema Lukuvi.

  Dk. Mahanga alisema hayuko tayari kusema lolote kwa vile mtu aliyetoa madai hayo ahamjui.

  Kwa upande wake, Dk. Nagu alipoulizwa na Nipashe, alisema: “Ngoja kesho niongee na mtu huyo kwani sasa hivi niko Morogoro, nitawasiliana naye kisha tutaongea Jumanne (kesho) .”

  Dk. Nchimbi alisema: “Mimi sijamsikia (huyo mtu). Wewe mwenzangu umepata kumsikia. Mimi mpaka nipate bahati ya kumsikia.”

  Dk. Chegeni alipoulizwa na mwandishi wa Nipashe juu madai ya elimu yake, naye alimuuliza mwandishi kuwa: “Mtu akikuuliza mimi ni mume wa mama yako utajibu nini?” Lakini mwandishi alipomtaka ajibu swali aliloloulizwa, aliongeza: “Kama mtu huyo amesema ana haki ya kusema.”

  Mwambalaswa alisema watu wanaomhusisha na kashfa hiyo kama si katika kundi la mafisadi, basi watakuwa ni watu ambao walioshindwa kufuatilia kuhusu ukweli wa elimu yake.

  Alisema shahada anayodaiwa kughushi aliipata kihalali katika nchi za Uholanzi na Uingereza.

  Naye Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah alipoulizwa kama barua ya Msemakweli imefika katika Ofisi ya Spika, alisema kwamba, bado hajaiona.

  “Nimesikia suala hilo leo asubuhi kutoka kwa waandishi wa habari. Mimi barua sijaiona. Sina uhakika, hivyo siwezi kusema lolote,” alisema Kashilillah na kuongeza kuwa Spika amesafiri.

  Source: Nipashe.

  Mie niliwahi kusemaga nyuma sasa hivi ulimwengu wa mtandao ni mpana huna haja ya kudanganya mtu akigoogle atapata details zako zote sasa nao wazee wanaumbuka. PhD za miezi sita, masters ya miezi miwili wapi na wapi???
   
 2. W

  WildCard JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  "Dr" Mzindakaya vipi?
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hili suala tumelijadili mara nyingi sana hapa JF. Kuna haja ya kutenganisha kati ya kugushi vyeti na kusoma vyuo visivyotambulika.

  Labda kama mwandishi ndiye kaandika vibaya; kwa aliyechunguza kama atasema hawa jamaa wameforge vyeti, wanaweza kumshinda kirahisi. Walichofanya wao ni kutumia titles ambazo hazilingani na elimu yao kama inavyotambuliwa na taasisi mbalimbali za elimu.

  Yule wa wilaya moja, nafikiri ni mkoa wa Mara, yeye ndiye ka forge cheti maana ni kweli hajawahi kusoma popote. Pia huenda Lukuvi naye kama ni kweli hajawahi kusoma popote.

  Hao akina Kamala wanavyo hivyo vyeti na vimetolewa na institutions ambayo zipo kihalali lakini tu elimu wanayotoa haikidhi requirements zinazotakiwa kwenye elimu zao.

  Sidhani kama spika Sitta anaweza kufanya lolote kwenye hili; wanaoweza kufanya jambo ni wananchi ambao baada ya kujua ukweli huu wanaweza kuwawajibisha wabunge wao. Pia kwa rais aliyewapa kazi, anaweza kuona hawana sifa tena na kuwaondoa kwenye hizo nafasi zao.

  Amenifurahisha Mwambalaswa anayekimbilia kwamba ni mafisadi ndio wanamtuhumu. Kwanini ashindwe kujibu swali la wazi kama hilo?
   
 4. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hawa kwa nyadhifa walizo nazo kwenye jamii hawahitajii kusukumwaa kuwajibikaa kwa hilii..

  kama elimu yao inatiliwaa shakaa wanawajibikaa kujitokeza na kujiteteaaaa....
   
 5. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  sasa vijana na form four walifoji vyeti wakaingia BOT mkawapeleka mahakamani,why not these big potatoes? uwajibikaji ni muhimu incase wameforge,yani kila mtu Dr, Dr thats why, hatuoni hata UPhd katika kazi za maPhd's wengi nchini?
   
 6. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hao mafisadi wa elimu mbona wanafahamika siku nyingi na wameshasemwa sana lakini hakuna hatua iliyochukuliwa. Kuna mwingine Moses Warioba alifoji PhD, akapewa hadi uprofesa na ukuu wa chuo Mzumbe kwa cheti cha kughushi, na amekula bata kwa kwenda mbele hadi amestaafu, kudadadeki! Nchi hii bwana! Kama kuna maprofesa wa kughushi katika vyuo vikuu, unategemea nini katika sehemu nyingine?

  Nafikiri hii nchi inahitaji jitu kama Benito Mussolini au Adolf Hitler.
   
 7. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huyo anaeleweka ni dr wa university ya kijadi ya Lyamba Lya Mfipa
   
 8. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hapo kwa Lukuvi hata mie nna shaka. But anyway ngoja tuhuma hizo zithibitishwe kwanza may be that is the reason why our country always is having unsound decisions
   
 9. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Kuelekea uchaguzi mkuu mwakani tutaona na kusikia mengi. Utetezi wa walio wengi utakuwa 'MAFISADI WANANIANDAMA, ama WABAYA WANGU WANANYEMELEA JIMBO LANGU" Hawatajibu hoja/swali
   
 10. W

  WildCard JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Naona wote mmewapa UWAZIRI! Wenye vyeo wakiliona hili patakuwa hapatoshi humu. Hapo WAZIRI ni "Dr" Nagu tu wengine ni manaibu.
   
 11. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Unajua ishu inakuja hivi credibility ya nchi inashuka kwasababu ya watu kama hawa imagine mtu anajiita Dr. halafu anaalikwa kwenye Global Forum au mkutano muhimu anaanza kuzungumza kitu hakieleweki unadhani yeye ndio anaaibika bali ni sie tunaoaibika ni afadhali mtu aseme sina hicho cheti watu watasema inawezekana elimu yake ndogo sio kusema vitu havina mwelekeo.

  Pili vitu kama hivi ndio vinasababisha nchi kuingia katika hasara kwani mikataba mtu hafahamu hili wala lile anasign tu akijua baadae ana kitu kidogo sasa unategemea uadilifu utapatikana? Hamna accountability kwasababu mtu hajali na wala hatojali kwasababu yeye reputation kwake sio ishu kuliko maslahi binafsi.
   
 12. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kamala pia ni waziri kamili.
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Nina maana ya hao waliotundikwa picha zao hapo juu.
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 542
  Trophy Points: 280
  kama huyu nae ndo hivo akina sie itakuwaje
  [​IMG]
  Dk. Makongoro Mahanga, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana.
   
 15. W

  WildCard JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Huyu ni msomi mzuri tu kwa viwango vyetu hapa Nchini. Ana CPA na CSP. Sijui huo udaktari feki aliutaka wa nini wakati kuwa MBUNGE au WAZIRI hakuhitaji elimu kuubwa kiivo!
   
 16. JS

  JS JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2009
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  kaaazi kwelikweli.....watu wanaoshika dhifa za juu ndo kama hivyo na wachini wafanyeje??lakini bado wako innocent till proven guilty by the law of the land of Tanzania.ila ndo wameshachafuliwa tayari
   
 17. O

  Omumura JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ni vema veme rungu la TCU likamulika baraza zima la mawaziri jamani!
   
 18. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #18
  Oct 19, 2009
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hii sasa kali!
  Tanganyika Law Society, Haki Elimu, Tamwa na wanaharakati wengine watusaidie kuwafungulia mashtaka hawa ili wakajitetee mahakamani na hivyo vyeti vyao!!! Najua ofisi ya Bunge haitafanya lolote!! Watanzania tuwe offensive now! Rais, watazania kwa hili la ufisadi wa kielimu tuwe wakali.
   
 19. W

  WildCard JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Zed,
  Huko Mahakamani nako utakuta JAJI anayepelekewa kesi hizi ana cheti feki cha kidato cha sita! Mambo ni magumu NCHI hii, we acha tu.

  BTW, yale ya Mbunge Chitalilo yaliishia wapi?
   
 20. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Namshangaa huyu Msemakweli anavyojaribu kupambana na rais! Hawa wote wameteuliwa na rais, na kabla ya uteuzi kama huo lazima anaangalia CV zao.

  Hakuna mwenye nia ya kuwafanya chochote hawa hata ingekuwa ni kweli wamevunja sheria yoyote ya nchi. Si mpaka serikali ipate ushahidi kamili? Hebu acheni bana.

  Tofauti ya msingi (Tanzania tu) kati ya private sector na public service ni kwamba private sector ina 0% tolerance to fraud, theft, inefficiency, poor performance, ufisadi, na ujinga ujinga wote wakati serikalini wao ni 100%. The more you damage the more you are safe guarded.
   
Loading...