Mawaziri wanane watakiwa kung'oka...!

Kaka Tatizo siyo hilo Tatizo watendaji wote wamekaa kimasilahi nyerere aliye baki sisiem ni hawa watu watatu 1. samweli sita
2.mwakyembe 3.dk magufuli wapeni uwaziri mkuu hawa muone
 
Mawaziri saba wajiuzulu.


Mkuchika, Ngeleja, Maige, Nundu,Dk Mponda, Magembe na Chami
headline_bullet.jpg
Mkulo aambiwa atafakari naye atoke
headline_bullet.jpg
Ni shinikizo la wabunge wa CCM



Fulku(1).jpg

Mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe (kushoto) akisaini kwenye orodha ya wabunge wanaotafuta idhini ya Bunge ya kusudio la kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Mbunge huyo alitia saini kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana. Kulia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, (Chadema) Zitto Kabwe akishuhudia.


Mawaziri saba wameandika barua za kujiuzulu nyazifa zao kwa kile kinachodaiwa ni shinikizo kutoka kwa wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao unatokana na udhaifu katika utendaji wao wa kazi.

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka ndani ya kikao cha wabunge wa CCM, kilichoketi katika ukumbi wa Piusi Msekwa mara baada ya kuahirishwa kwa shughuli za Bunge usiku, waliojiuzulu ni Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi),George Mkuchika na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.


Wengine ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami.

Hata hivyo, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo aliyetuhumiwa kuwa ni kiongozi wa ubadhirifu bungeni juzi na Mbunge wa Ludewa(CCM), Deo Filikunjombe, ameambiwa atafakari kwa sababu hayupo nchini.

Taarifa hizo zilisema wabunge hao waliishambulia serikali kuwa pamoja na mambo mbalimbali imekuwa haiwajibika katika mambo mbalimbali na hivyo kusababisha kadri siku zinavyoendelea chama kupoteza mwelekeo.

Chanzo hicho kilisema utendaji usioridhisha wa serikali ndio uliowafanya wabunge wa chama hicho kufikia hatua ya kushinikiza mawaziri hao wajiuzulu nyazifa zao.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa hali hiyo imechochewa na taarifa zilizowasilishwa na Kamati mbalimbali za Bunge kati ya juzi na jana.

Kamati zilizowasilisha ripoti zao juzi ni Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma POAC, inayoongozwa na Zitto Kabwe, Kamati ya Hesabu za Serikali PAC ya John Cheyo na ile ya Serikali za Mitaa LAAC, inayoongozwa na Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema.

Kamati zilizowasilisha ripoti zake jana zilikuwa ni pamoja na Kamati ya Nishati na Madini inayoongozwa na Januari Makamba, Kamati ya Miundombinu inayoongozwa na Peter Serukamba na Kamati ya Fedha na Uchumi ambayo mwenyekiti wake ni Dk Abdallah Kigoda.

Kamati zote hizo zilikuja na ripoti kadhaa zilizoonyesha udhaifu katika utendaji hali iliyolazimisha Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Kabwe Zitto, kuanzisha zoezi la kuandaa hoja ya kumtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ajiuzulu.

Hadi kufikia jana mchana wabunge 62 wakiwemo wa CCM, waliweka sahihi katika hoja hiyo inayotakiwa kusainiwa na wabunge wasiopungua 70.


Hali ndani ya Bunge imeanza kuwa ya moto kwa sababu matarajio ya Watanzania hajafikiwa na hakuna kiongozi wa serikali anayejali kuhusiana na hilo.


Katibu wa wabunge wa CCM, Jenister Mhagama jana usiku aliwaita waandishi wa habari katika ofisi za Bunge lakini hata hivyo hakukataa wala kuthibitisha kuandika barua za kujiuzulu kwa mawaziri hao.


“Wabunge wa CCM wametekeleza wajibu wao mkubwa wa kikanuni na kikatiba wa kuona namna gani wanaishauri serikali na maamuzi yaliyotokana na kikao chetu yatatolewa na viongozi waandamizi…kiongozi wetu mwandamizi aliyepo hapa Dodoma ni Mwenyekiti wetu (Mizengo Pinda),”alisema ikiwa ni muda mfupi mara baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuondoka katika ukumbi wa Pius Msekwa.


Licha ya waandishi wa habari kuhoji mara kadha kwanini amewaita usiku kama walikuwa hawajafikia hatua ya kusema maamuzi yao, Mhagama alisisitiza kuwa kwa mujibu wa kanuni na taratibu msemaji ni mwenyekiti wa wabunge wa CCM na kwamba taarifa itatolewa kwa umma na Pinda.


Hata hivyo, Mhagama aliitaka serikali ijitathimini upya kuanzia kwa mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri hadi katika ngazi ya kijiji na kuchukua uamuzi.


Awali Spika Makinda, amesema zoezi linalofanywa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, (Chadema), Kabwe Zitto linalolenga kuwasilisha bungeni hoja ya kumwondoa waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ni batili.

Makinda aliyasema hayo jana jioni wakati wabunge wakiendelea kuchangia ripoti za kamati mbalimbali zilizowasilishwa bungeni jana.

Alitoa maelezo hayo baada ya kuombwa mwongozo na Mbunge wa Bumbuli (CCM), Januari Makamba ambaye alitaka kufahamu kama zoezi hilo utaratibu ukoje.

Alisema azma ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu imeelezewa katika kifungu cha 133 cha kanuni na kwamba imepewa nguvu katika katiba ibara ya 53 A kifungu kidogo cha tatu.


Alisema anafikiri Zitto alitaka kuwasilisha hoja hiyo, kwa sababu ibara ya 51 kifungu kidogo cha B kinasema Waziri Mkuu anateuliwa na Rais lakini kabla ya kuwa waziri mkuu anaapishwa na Bunge.


“Naye hatashika madaraka yake hayo mpaka hapo uteuzi wake utakapothibitishwa na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na wabunge walio wengi,”alisema.


Alisema ndio msingi wa Zitto kwamba huyo ni mtu waliyempitisha wenyewe na kwamba wabunge wanamamlaka naye kwasababu wamemthibitisha.


Alisema wakati huo huo ibara ya 52 ya Katiba inatamka kuwa Waziri Mkuu ndiye atakayekuwa kiongozi wa shughuli za bunge bungeni.

Alisema kuwa vifungu vya Katiba vinafanana na kanuni za Bunge ambapo kifungu cha 53 ibara ndogo ya pili inasema serikali ya Jamuhuri ya Muungano Tanzania chini ya mamlaka ya Rais, ndiyo itakayokuwa na itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera ya serikali kwa ujumla.
“
Mawaziri chini ya uongozi wa Waziri Mkuu watawajibika kwa pamoja bungeni kuhusu utekelezaji wa shughuli za serikali ya jamuhuri ya muungano hivi vifungu ndivyo vinatupa nguvu kwamba tunauwezo na waziri mkuu,”alisema.

Alisema lakini kifungu cha ibara ya 53 A na 63 ibara ndogo tatu kinaeleza kuwa wabunge hatapiga kura ya kutokuwa na imani na waziri

mkuu ikiwa, “Taarifa ya maandishi iliyotiwa sahihi na kuungwa mkono na wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote itatolewa kwa Spika angalau siku 14 kabla ya siku ambayo inatakiwa kuwasilishwa bungeni.”


Alisema kipengele B kinatamka kuwa Spika atajiridhisha kwamba masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja yametimizwa na kwamba masharti yenyewe yapo katika ibara ya 53 A kifungu kidogo cha pili.


Alikinukuu kifungu hicho kidogo cha pili kinasema bila ya kuathiri masharti mengine ya ibara hii hoja yoyote ya kutaka kupitisha kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu haitatolewa bungeni ikiwa haina uhusiano na utekelezaji wa majukumu ya waziri mkuu kwa mujibu wa ibara ya 52 ya Katiba.


Alifafanua kuwa katika kifungu hicho kidogo cha pili B kinasema hoja hiyo haitatolewa bungeni ikiwa hakuna madai kwamba waziri mkuu amevunja sheria ya maadili ya uongozi wa umma.


Pia alisema kipengele C kinatamka kuwa hoja hiyo haitawasilishwa ikiwa haijapita miezi sita tangu ameteuliwa.

Alisema katika kipengele cha D kinaeleza kuwa kura hizo hazitapigwa ikiwa haijapita miezi tisa tangu hoja ya namna hiyo ipotolewa bungeni na mbunge na ikakataa kupitishwa.

Alisema la msingi hapo ni zile sahihi zinazotakiwa kuwepo, taarifa ipelekwe kwa spika kwa maandishi siku angalau 14 kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa.


“Sasa hiyo ya habari ya mheshimiwa wakati anachangia jamani njooni njooni hiyo utaratibu akitumia hiyo hiyo haikubaliki kwa sababu mimi sijapata hoja kabisa hadi sasa,”alisema na kuongeza:


“Maanake hili bunge linaahirishwa tarehe 23 maanake Jumatatu …haikidhi siku 14 sana sana anaweza kuzikusanya labda Bunge lijalo na zenyewe ziwe sio chini ya siku 14 kwa hiyo zoezi linaloendelea au kama linafanywa ni batili kwa maana hiyo,”alisema na kwamba siku tatu zilizobakia yatakuwa haina msingi.
CHANZO: NIPASHE

 
Kujiuzulu ni ishara ya uwajibikaji, kama ni kweli CCM imeonyesha dhamira ya dhati kushughulikia matatizo ya watanganyika.
 
Confirmed. Waliojiuzulu ni Mkullo, Mponda,Nundu na Chami.

Mkullo alikuwa Washington, je ameleta e-mail ya kujiuzulu? Kikwete hawezi kuridhia Mkullo kujiuzulu kwani yote anayoyafanya ni kwa maelekezo ya Kiwete mwenyewe!!Sinema ya Jairo inajirudia , hatachukua maamuzi yeyote juu ya ubadhirifu wa Mkullo na huyu waziri ataendelea kumdharau Spika pamoja na bunge lake!!
 
Hivi makamu wa rais ye hawez kuidhnisha hao mambwa wajiuzuru,au yeye kaz yake ni nin?
 
KUJIUZULU KWA HAWA MAWAZIRI HAITOSHI, KUNA HAJA YA KWENDA MBALI ZAIDI NA KUWASHITAKI KWA UHUJUMU UCHUMI, MH. MKULO UKIISOMA HII NAOMBA UNISAMEHE KWANI HUU NDIO MTAZAMO WANGU.....IWE KAMA ILIVYOKUWA KWA DANIELI YONA PAMOJA NA PESAMBILI MRAMBA WALIVYOWAJIBIKA.....KATIKA THREAD YANGU "NITAISHITAKI CCM MAHAKAMANI" UKIIPITIA UTAONA MFANO WA KESI AMBAYO SENETA WA JIMBO LA NEBRASKA, USA JINSI ALIVYOMSHITAKI MUNGU MAHAKAMANI....MALIZIA MAJIBU YAKE KWA WAANDISHI WA HABARI KWANINI ALIAMUA KUFANYA HIVYO.....bARAZA LA MAWAZIRI NI KWELI LIMEOZA PERIOD!!


Haya bana. This is going the to be the missed opportunity.
 
Picha zimeonyesha vizuri kazi zake - si kukata tepe tu, bali pia kupanda miti ya kumbukumbu, kuweka mawe ya msingi/kuzindua miradi. Kumbe hata mimi naweza tu kuwa Makamu wa Rais!
 
Jamani, Watu wengi sana especially wale akina "tutaneemekaje bila kuwa puppets" enzi za ubaguzi SA waliaswa vizuri na YVONNE MACHAKA (Yvone Chakachaka) kwa njia ya wimbo "LET HIM GO" Japo ilikuwa inauma kwa lakini walielewa somo.Na sisi leo hadi tuimbiwe "MWACHE AENDE?" Big NO, mimi nasema, "let THEM go" to avoid more confusion in CAPITAL L.
 
Hivi wakuu kwa mfano hili kichwa cha nazi likawagomea jamaa kujiuzulu tutafanyaje? Tunao ubavu?
 
Back
Top Bottom