peck
JF-Expert Member
- Dec 20, 2010
- 220
- 27
Binafsi nawashangaa MAWAZIRI hawa wa jk walivyo na majibu rahisis kwa hoja zinazoonekana kuwanufaisha watanzania wengi, Mfano:-
- Hoja ya KATIBA mpya waziri Kombani alisema kuandaa Katiba mpya ni Gharama kubwa serikali HAIWEZI kuandika katiba mpya.
- Jana tumemsikia waziri kawambwa amewaambia wanafunzi wa UDSM kuwa madai yao HAYAWEZEKANI.
- Lakini Kwenye suala la kuilipa DOWANS waziri wa wizara husika HATUKUMSIKIA akisema HAIWEZEKANI japokuwa inaonekana dhahiri hakuna uhalali wa kuilipa. Waziri mkuu, rahisi wa JMT, nao HAWAKUONA kuwa HAIWEZEKANI, wakidai ni vigumu kutowalipa DOWANS.
nawashangaa sana mawaziri hawa wa jk.