Paul Christian Makonda anza na Dotto Biteko maana hivi sasa Tanesco ni kama imesimamisha maisha ya wapiga kura

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,213
3,596
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Kamaradi Paul Christian Makonda tunakuomba katika jitihada zako za kukaa na watendaji wa mhimili wa serikali wakiwemo Mawaziri kuhimizana kuhusu utekelezaji wa ilani ya CCM UANZE NA WAZIRI WA NISHATI ili kunusuru taifa na laana ya upungufu wa nishati ya umeme inayofanya taifa lisiwe na mvuto kwa wawekezaji toka nje.

Nishati ya umeme inabeba hatima ya maisha ya watu kwa 90%. Hivi sasa idadi ya wasiotumia umeme JMT imeongezeka (kufuatia upungufu na tozo kwenye ankara)

Mwaka 2018 Watz 36% walikuwa hawajafikiwa na ugavi wa umeme, taifa likiwa miongoni mwa nchi 15 zenye idadi kubwa ya watu wasio na huduma hiyo ambapo wastani wa dunia ilikuwa ni 90. www.statista.com/statistics/1134587/ho

Wapigakura wanapandishiwa ankara ya umeme na kero zifuatazo:-

1. Tozo (REA, TRA, TANESCO-Service Charge, EWURA, KODI YA MAJENGO)

2. Upungufu wa umeme.

3. Siasa za nishati (wauza majenereta na mafuta na wafua umeme wa binafsi na kuiuzia Tanesco).

4. Gawio kwa serikali.

Abracadabra ya siasa za nishati za kuteteana na kutupiana zigo:

Nukuu.
"Baadhi ya wabunge walitaka kuonesha kuwa tatizo la kukatika kwa umeme lilikuwa limekwisha ila limerudi tu baada ya waziri Makamba kuanza kuongoza wizara ya Nishati, suala ambalo si kweli.

Ilivyo bahati, takwimu alizotoa mbunge wa Viti Maalam, Jesca Kishoa wakati akichangia bungeni zilionesha kuwa tatizo la kukatika kwa umeme halijawahi kwisha.

Mbunge Kishoa alisoma bungeni taarifa ya mwaka 2018 ya Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura) iliyoonesha kuwa mwaka 2017 umeme ulikatika mara 2,844 nchini Tanzania.

Hii inamaanisha mwaka 2017 umeme ulikatika takribani mara saba kwa siku. Hiki ndiyo kipindi ambacho baadhi ya wabunge wanadai umeme ulikuwa haukatiki" mwisho wa nukuu.

Tangu awamu ya 1 kila serikali imejinasibu kuwa ndani ya awamu yake ingefanya tatizo la umeme kuwa historia.

Mwl. Nyerere aliamini umeme wa maporomoko ya maji ya mto Rufiji Stiegler's Gorge kumaliza tatizo la umeme JMT.

Mzee Ruksa aliamini katika umeme wa mafuta wa kufuliwa kwa jenereta baada ya Stiegler's Gorge kumshinda Mwl kwa hoja za uhifadhi wa ikolojia uliofanya mbuga ya Selous kuwa urithi wa dunia. Mzee Ruksa akatengeneza sera ya nishati kusisitiza juu ya umeme wa majenereta.

Big Ben Mkapa aliamini katika mgodi wa makaa ya mawe Kiwira kumaliza tatizo la umeme JMT na akabadili sera toka kuwa umeme wa mafuta kuwa wa makaa ya mawe.

Kama watangulizi wake, JK naye akaja na ndoto yake ya umeme wa gesi-asilia kuwa ndiyo suluhu ya kudumu, tafiti zikaanza, uzalishaji ukafuatia lakini ndoto ya awamu hiyo IKAISHIA KUONDOKA NA WAZIRI MKUU na kuandika historia mpya JMT.

Magufuli maono yake yakagongana na imani ya Mwl Nyerere ya Stiegler's Gorge. Akavaa uso wa Simba-dume na kuingia vitani na wanaharakati wa mazingira, mapapa wa biashara za mafuta na jenereta, wafua umeme binafsi, wanazuoni wa uchumi, sera na nishati na kuibuka mshindi.

Chini ya maono ya awamu ya 5 taifa likaanza kubuni miradi mikubwa ya kuhitaji umeme wa uhakika na kujenga njia za ugavi na za export ya umeme kuvuka mipaka kwenda masoko ya nje Mbeya hadi Namanga.

Miradi hii ya fedha nyingi inachagiza ujenzi wa Stiegler's Gorge penda usipende maana imebuniwa kimkakati kuzifanya zitegemezane kama kuku na yai.

Katika awamu za 3 na 4 TANESCO lilikuwa shamba la bibi la wajukuu DOWANS, SYMBION, RICHMOND, AGGREKO, IPTL, NetGroup Solutions. Awamu ya 6 TANESCO inadai wateja wake 244 MMM (Tshs.244 bl) na makampuni 2 ya kukusanya madeni yanatafutwa, nao hawa wanatarajia kula kwenye shamba la bibi.

Mwaka 2021 Tanesco ilikuwa inazalisha MW 1605.86.

Taarifa isiyonishawishi kabisa kwa jinsi ya upungufu huu wa umeme ni hii:

Mwaka 2023 takriban MW 1,900 zinazalishwa kwa mujibu wa Gissima Nyamohanga Mkurugenzi mpya wa Tanesco akisema gesi inachangia takriban 65% ya uzalishaji jumla.

Inasemekana kuwa MW zinazotumika hivi sasa nchini zinaweza kutumiwa zote na SGR huku watumiaji wengine wakabaki bila nishati. Na hii ndiyo sababu JNHPP lazima ijengwe.

Paul Christian Makonda anza na Dotto Biteko maana hivi sasa Tanesco ni kama imesimamisha maisha ya wapigakura (Watz) kwa 99%.

Nadhani mshauri mteuzi wako amrejeshe Dr. Medard Kalemani kwenye wizara ya nishati, hii pia itasaidia kurejesha imani ya watu wa Kanda ya Ziwa kwa ajili ya 2024 na 2025 maana JMT umeme ni siasa.
 
Back
Top Bottom