Mawaziri wa jk mna nini???

peck

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
220
27

Binafsi nawashangaa MAWAZIRI hawa wa jk walivyo na majibu rahisis kwa hoja zinazoonekana kuwanufaisha watanzania wengi, Mfano:-

  • Hoja ya KATIBA mpya waziri Kombani alisema kuandaa Katiba mpya ni Gharama kubwa serikali HAIWEZI kuandika katiba mpya.
  • Jana tumemsikia waziri kawambwa amewaambia wanafunzi wa UDSM kuwa madai yao HAYAWEZEKANI.
  • Lakini Kwenye suala la kuilipa DOWANS waziri wa wizara husika HATUKUMSIKIA akisema HAIWEZEKANI japokuwa inaonekana dhahiri hakuna uhalali wa kuilipa. Waziri mkuu, rahisi wa JMT, nao HAWAKUONA kuwa HAIWEZEKANI, wakidai ni vigumu kutowalipa DOWANS.
    nawashangaa sana mawaziri hawa wa jk.
 
wanajipendekeza, si unajua tena ile hela ya dowans bosi wao ndio steringi, ndio kala fungu kubwa....sasa hawawezi kumlipua, lazima waseme inawezekana na ni lazima
 
Tatizo si mawaziri ndugu zangu. Tatizo mbona mnajifanya kama hamlioni? Tatizo ni la mwenye nyumba!! Mwenye nyumba dhaifu - na hajui la kufanya hivyo kila mtu anajifanyia atakalo. Mawaziri wote wanajua kufanya usanii hivyo kuiga ya kiranja wao......
 
Binafsi nawashangaa MAWAZIRI hawa wa jk walivyo na majibu rahisis kwa hoja zinazoonekana kuwanufaisha watanzania wengi, Mfano:-

  • Hoja ya KATIBA mpya waziri Kombani alisema kuandaa Katiba mpya ni Gharama kubwa serikali HAIWEZI kuandika katiba mpya.
  • Jana tumemsikia waziri kawambwa amewaambia wanafunzi wa UDSM kuwa madai yao HAYAWEZEKANI.
  • Lakini Kwenye suala la kuilipa DOWANS waziri wa wizara husika HATUKUMSIKIA akisema HAIWEZEKANI japokuwa inaonekana dhahiri hakuna uhalali wa kuilipa. Waziri mkuu, rahisi wa JMT, nao HAWAKUONA kuwa HAIWEZEKANI, wakidai ni vigumu kutowalipa DOWANS.
    nawashangaa sana mawaziri hawa wa jk.

Unajua ukielewa jinsi dunia inavyoendeshwa,hutamshangaa Kikwete wala mawaziri wake mambo wanayofanya.Wametumwa na mabwana zao to do just that. In fact sisi tunavyo washangaa na wao wanatushangaa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom