Mawaziri hawa watano utumishi wao haujatukuka

Stuka

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
214
686
Wana Bodi,

Kuna Mawaziri 5 ambao sina uhakika sana na rekodi zao katika Utumishi wa Umma hivyo mambo mengi yanayohusu Public Fund hawayajui na wanadhani wakiwa Mawaziri wanaweza kufanya maamuzi yoyote kuhusu fedha za Umma bila kufuata sheria za nchi.

1. Mwigulu Nchemba sijui rekodi yake kama aliwahi kuajiriwa Serikalini kama mtumishi wa umma ninachosikia ni kwamba aliwahi kuwa BOT kwa muda mfupi sana baadaye akatumbukia kwenye siasa sina uhakika na uzoefu wake kwenye eneo la utumishi wa umma na sasa ni Waziri wa Fedha.

2. Januari Makamba, yeye historia yake siijui imekaaje na sijui hata kama aliwahi kuajiriwa kama Mtumishi wa Serikali zaidi niliwahi kusikia alifanya kazi kwenye kambi ya wakimbizi kwenye Shirika la UNHCR na baadae akatumbukia kwenye siasa na kuwa msaidizi wa Rais na sasa Waziri. Sijui uzoefu wake katika utumishi wa umma na ufahamu wake wa kutosha kuhusu mambo ya Serikali. sasa ni Waziri wa Nishati.

3. Hussein Bashe, yeye hata historia yake ya haieleweki zaidi niliwahi kusikia alikuwa akifanya kazi kwenye gazeti la Mtanzania na baadaye akatumbukia kwenye siasa na sasa ni Waziri sijui hata aliwahi hata kuajiriwa serikalini na kujua mambo ya Serikali yanavyokwenda. Sasa ni Waziri wa Kilimo.

4. Nape Nauye, yeye historia yake hata ya elimu haijulikani lakini baadaye akatumbukia kwenye siasa mara akapewa Uenezi wa CCM mara DC na sasa Waziri wa Wizara kubwa ya TEHAMA sijui kama aliwahi kuwa mtumishi wa Serikali na kufahamu mambo ya Serikali.

5. Prof. Makame Mbarawa 'Mzee wa Mkataba wa Bandari' yeye sijui hata historia yake ya elimu na hata sijui aliwahi kufanya kazi wapi zaidi tulimuona kwenye siasa kwa kuteuliwa kuwa Waziri na Jakaya na sasa ni Waziri wa mambo ya Reli, Bandari na ANGA sijui hata kama aliwahi kuwa mtumishi wa Serikali.

Na ndiyo maana Mawaziri hawa kutokana na kutokuwa na ufahamu wa kutosha wa utumishi wa Serikali na namna ya usimamizi wa Fedha za Umma ndiyo sababu wizara zao zinakubwa na kashfa lukuki kila siku kuhusu matumizi ya fedha za Umma.

Ninachokiona mimi Siku Rais Samia Suluhu Hassan atakapoondoka madarakani ambaye ndiye wanayemtegemea kama Kinga yao hao Mawaziri 5 waitashia kufungwa gerezani kwa makosa makubwa waliyofanya wakiwa kwenye nafasi zao za uwaziri. vinginevyo labda waamue kukimbia nchi na kuishi ughaibuni.

Taarifa zilizopo wengine wameshaanza kuhamishia familia zao kwenye makazi yao mapya huko Dubai.

mwigulu-nchemba-2841c64b-6f08-4e77-bbdd-4b133d07a4e-resize-750.jpeg

Mwigulu Nchemba

gettyimages-494328416-612x612.jpg

Januari Makamba

Hussein-Bashe.jpg

Hussein Bashe

nape-.jpg

Nape Nauye

P45A1658.JPG

Makame Mbarawa
 
Sijui kama kuna uhusiano gani wa kuwa mwanasiasa lazima utokee utumishi wa umma...ila nachojua hao ni wapiga dili wote,WABINAFSI
Uhusiano upo Mkuu ukiwa umewahi kuajiriwa serikalini Sheria nyingi za utumishi na mambo ya usimamizi wa fedha za umma utazijua mfano mtu aliwahi kuwa Mwalimu, akaja akafanya kazi Halmashauri hata Mkuu wa Idara, akaja akawa DC, akafanya kazi Wizarani hata leo akiwa Waziri atamudu majukumu yake vizuri atakuwa na upeo mkubwa wa mambo ya Serikali.
 
Kweli wajinga mnazidi kuwa wengi hivi ni lazima uwe mtumishi ndo uwe mwanasiasa?
Soma maudhui uelewe acha UCHAWA, mfano mtu kama George Huruma Mkuchika huwezi kumkuta kwenye tuhuma za ufisadi au ukosefu wa maadili ya utumishi wa umma kwa sababu amepita kwenye mifumo yote ya kiserikali hadi kufikia ngazo ya Waziri. Hata Samia mwenyewe amepita kwenye utumishi wa Serikali
 
Kwani kikatiba waziri anatakiwa kuwa na sifa zipi?
 
Wana Bodi,

Kuna Mawaziri 5 ambao sina uhakika sana na rekodi zao katika Utumishi wa Umma hivyo mambo mengi yanayohusu Public Fund hawayajui na wanadhani wakiwa Mawaziri wanaweza kufanya maamuzi yoyote kuhusu fedha za Umma bila kufuata sheria za nchi.

1. Mwigulu Nchemba sijui rekodi yake kama aliwahi kuajiriwa Serikalini kama mtumishi wa umma ninachosikia ni kwamba aliwahi kuwa BOT kwa muda mfupi sana baadaye akatumbukia kwenye siasa sina uhakika na uzoefu wake kwenye eneo la utumishi wa umma na sasa ni Waziri wa Fedha.

2. Januari Makamba, yeye historia yake siijui imekaaje na sijui hata kama aliwahi kuajiriwa kama Mtumishi wa Serikali zaidi niliwahi kusikia alifanya kazi kwenye kambi ya wakimbizi kwenye Shirika la UNHCR na baadae akatumbukia kwenye siasa na kuwa msaidizi wa Rais na sasa Waziri. Sijui uzoefu wake katika utumishi wa umma na ufahamu wake wa kutosha kuhusu mambo ya Serikali. sasa ni Waziri wa Nishati.

3. Hussein Bashe, yeye hata historia yake ya haieleweki zaidi niliwahi kusikia alikuwa akifanya kazi kwenye gazeti la Mtanzania na baadaye akatumbukia kwenye siasa na sasa ni Waziri sijui hata aliwahi hata kuajiriwa serikalini na kujua mambo ya Serikali yanavyokwenda. Sasa ni Waziri wa Kilimo.

4. Nape Nauye, yeye historia yake hata ya elimu haijulikani lakini baadaye akatumbukia kwenye siasa mara akapewa Uenezi wa CCM mara DC na sasa Waziri wa Wizara kubwa ya TEHAMA sijui kama aliwahi kuwa mtumishi wa Serikali na kufahamu mambo ya Serikali.

5. Prof. Makame Mbarawa 'Mzee wa Mkataba wa Bandari' yeye sijui hata historia yake ya elimu na hata sijui aliwahi kufanya kazi wapi zaidi tulimuona kwenye siasa kwa kuteuliwa kuwa Waziri na Jakaya na sasa ni Waziri wa mambo ya Reli, Bandari na ANGA sijui hata kama aliwahi kuwa mtumishi wa Serikali.

Na ndiyo maana Mawaziri hawa kutokana na kutokuwa na ufahamu wa kutosha wa utumishi wa Serikali na namna ya usimamizi wa Fedha za Umma ndiyo sababu wizara zao zinakubwa na kashfa lukuki kila siku kuhusu matumizi ya fedha za Umma.

Ninachokiona mimi Siku Rais Samia Suluhu Hassan atakapoondoka madarakani ambaye ndiye wanayemtegemea kama Kinga yao hao Mawaziri 5 waitashia kufungwa gerezani kwa makosa makubwa waliyofanya wakiwa kwenye nafasi zao za uwaziri. vinginevyo labda waamue kukimbia nchi na kuishi ughaibuni.

Taarifa zilizopo wengine wameshaanza kuhamishia familia zao kwenye makazi yao mapya huko Dubai.

View attachment 2718757
Mwigulu Nchemba

View attachment 2718758
Januari Makamba

View attachment 2718760
Hussein Bashe

View attachment 2718762
Nape Nauye
View attachment 2718764
Makame Mbarawa
we amka usingizini hizo ni ndoto za hovyo, inaonekana ulikula maharage mengi na umevimbiwa ndio sababu ya hiyo ndoto ya hovyo
 
Ongezea hapo:

6. Saa100
7. Prof Kitilia Mkumbo
8. Spika wa bunge
9. Kinana
10. Wassira
12. Aweso
13. IGP
14. Chogolo
 
Kwani hizi ni hasira baada ya kijana mdogo, Diamond, kuonyesha umma wa watanzania kuwa yeye ni mkubwa kuliko nyumbu woteee au?
 
Back
Top Bottom