Kikwete asema mifumo mipya mitatu ya Utumishi itasaidia kupima utendaji na kujibu kero za wananchi

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amesema mifumo mipya mitatu iliyobuniwa na kufungwa kwenye utumishi wa umma itasaidia kwa kiasi kikubwa sana kupima utendaji kazi wa mtumishi yeyote aliyepangiwa majukumu na kuona kiwango cha utekelezaji wa majukumu yake huku ikisaidia kujibu kero na kutoa majawabu ya shida za wananchi.

Mifumo mitatu iliyobuniwa hivi karibuni kwa ajili ya kupima utendaji wa watumishi ni ule wa PEPMIS, PIPMIS pamoja na HR ASSESSMENT ambayo yote itahakikisha inafuatilia utendaji kazi wa mtumishi katika majukumu yote aliyopangiwa.

Naibu Waziri Kikwete ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma wakati akieleza utekelezaji wa ufungaji wa mifumo hiyo na tija yake kwa Taifa na wananchi.

"Sisi kama Wizara tumetengeneza mifumo ya PEPMIS, PIPMIS na HR ASSESSMENT. Yote ikisomeka pamoja inasoma utendaji kazi wa mtumishi kutoka kwenye mahitaji ama mapungufu ya kiutumishi. Mifumo hii inalenga kufanya tathmini ya kiutendaji kwamba huyu mtumishi wa umma aliyepewa majukumu fulani, Je anayafanya vizuri na anayafanya kwa kiasi gani? Kwahiyo itatusaidia serikali kujua mtumishi anafanyaje kazi. Kwenye mfumo huu tumeweka utambuzi kwa rangi ambapo kijani itaonyesha mtumishi anafanya kazi vizuri, njano itaonyesha mtumishi anafanya kazi vizuri lakini kuna ulegevu sehemu na nyekundu itaonyesha hapa kuna hatari na kazi hazifanyiki. Na hizi rangi zimewekwa ili kumwezesha msimamizi wa ofisi namna taasisi yake inavyofanya kazi na kwenye mapungufu hatua zichukuliwe"

Kikwete ameongeza kuwa ujio wa mifumo hiyo haina lengo la kufukuza watu serikalini bali ina lengo la kutaka utumishi wa umma uweze kutoa tija kwa wananchi kama ilivyo dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anayesisitiza kila mara kero za watu zitatuliwe.
 
Attachments

  • ofisi_ya_rais_utumishi_1704885929390777.mp4
    8.4 MB

Vipi, Watumishi wameandaliwa na kuielewa mifumo hiyo ikiwa ni pamoja na namna ya kuitumia?
 
Tatizo la utumishi wa umma wa katika nchi hii haliwezi kutatuliwa kwa njia za kuweka hiyo mifumo cha muhimu boresheni maslahi ya watumishi huku mkikumbuka kuwalipa malimbikizo ya mishahara yao wanayopigwa danadana miaka na miaka.Muone watumishi kama hawataanza kuchapa kazi kwa nguvu zote
 
Back
Top Bottom