Alichoongea Mbowe Ndio Wasifu wa Lowassa na Serikali iliwasilisha Historia ya Utumishi wa Hayati Lowassa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,975
141,986
Ndio sababu maeneo mengine akifariki kiongozi Wasifu wa Marehemu husomwa na Wanafamilia baada ya kukusanya taarifa za maisha yake binafsi kuanzia alipozaliwa na Historia ya Utumishi wake husomwa na Taasisi husika

Kwa kawaida Wasifu unaweza kubeba taarifa zote za muhusika lakini historia ya Utumishi itajikita kwenye Utumishi wake tu

Historia ya Utumishi wa Lowassa imeandaliwa na kusomwa na Serikali na siyo CCM hivyo kukosekana baadhi ya taarifa za Utumishi wa Lowassa kwenye Siasa siyo jambo la kushangaza sana

Na ndio sababu familia waliliona hilo na kulifanyia Kazi

Lakini kuna mambo mengi Lowassa amelifanyia Kanisa hayajasemwa, aliwafanyia Wasanii hayajasemwa nk..nk na yalipaswa kuwemo kwenye Historia ya Utumishi japo Mbowe aliyagusia alipozungumzia Wasifu wa Lowassa

Edward Lowassa RIP
 
Back
Top Bottom