Mimi namjua Nyaga vizuri kutoka wakati wa Ilboru na si fisadi. Ni kweli kwamba ni mtu ambaye si wa bei nafuu na kama akifanya kitu ata toa bill kubwa kwa kazi yake lakini kazi yake ni nzuri na haina usirisiri hata kidogo. Ni business lawyer mzuri na nilivyoongea na wafnaya biashara na mikataba ya biashara ni mtu wa uwazi. Nyaga ni mfano mzuri kwa vijana wa Kitanzania ni jinsi gani unaweza kufanya kazi kwa maadili mema.
Kama unamjua ni vizuri sana na inaelekea unamjua toka shule pia ujue kwamba unavyomjua mtu kwa nje ni tofauti kabisa na alivyo na anachofikiri, Kimsingi mimi simkubali huyu jamaa kwa haya yafuatayo:
Kutumiwa na Singita Grumeti Reserve: Jamaa huyu amekuwa akitumiwa na Singita Grumeti Reserve ili achukue maeneo kule Serengeti ili wao waweze kuongeza Camps zao na pia kufanya watu wengine wasianzishe Camps kule. Ameleta mzozo mkubwa sana kule kwenye vijiji vya Motukeri na nata kwa kuwahonga wenyeviti wa vijiji na madiwani pesa ambazo wao wanaona ni nyingi ili wampe shamba kubwa kama hekari 1000 ili afugie mifugo yake akiwa na kampuni yake ya kisanii yenye jina mbele then inaishia na Holdings. Hii imesababisha watu kuvurugana na kugombana kutokana na Ngawira anazopewa na Grumeti kuwahadaa wanakijiji kujiongezea maeneo
Gomba Estate na Burka. Kwa nini jamaa huyu anaonekana kwenye mikataba ya mashamba makubwa kama haya akiwa kama consultants? Nachokijua ni kwamba mashamba haya yakiisha muda wake huwa mali ya serikali na muwekezaji huyarudisha kwa Serikali. Yeye anakuwa nani hapo katikati in between Serikali na muwekezaji? na mbona baada ya ugawaji yeye hubaki na plot nyingi sana ambazo huwagawia rafiki zake including pilosi ambao humsaidia kwenye mambo yake?
Mawala Private Road:Huyu jamaa ana barabara yake ambayo kila anayepita hulipia except watu wanaokaaa jirani. makampuni kama Sokwe, Thomson, African environments hutozwa zaidi ya $1000 kwa mwaka kwa ajili ya kutumia barabara hiyo. Na kuna ushahidi mkubwa sana kuwa eneo hilo lote wamegawana na nywele nyeupe utadhani wao tu ndo wanastahili kupata hayo maeneno
In short huyu jamaa ni mbinafsi na pia anatuona sisi Watanzania ni wajinga sana kiasi cha kutumiwa kama Carl Peters kutufanyia mikataba ya kilaghai