Mawakili walilia ndevu za Sheikh Farid

Mawakili walilia ndevu za Sheikh Farid

Sheria za Tz yaani zinanitia mashaka makubwa sana. Hivi ni kwa nini waliwanyoa ndevu?, ni sababu gani muhimu ambazo zimeonyesha kuwa ndevu zinaleta risk either kwa mtuhumiwa mwenyewe au watuhumiwa wengine walio ndani?. Na je hii kweli ipo ktk kuzingatia haki za bin-adamu??
 
Duh,awa mawakili au?sheria imepata watu,hivi kwa mfano mahakama ikikubali kuhusu ndevu wao wasema mteja wao kasuffer kitu gan?na fidia itakuwa nin?ili kufidia hasara ipi?hahahaha..
 
'
Mimi binafsi sikumbuki kama Mchungaji Mtikila alinyolewa nywele zaki akiwa rumande! Mwenye ushuhuda alete hapa

Mchungaji Mtikila ni kiongozi wa Taifa wa chama chake sio gaidi. Hata kumkamata tu sio ila askari anaweza kumkamata. Ni lazima ofisa wa ngazi fulani.

Nikukumbushe kuwa Mtikila hachanganywi na mahabusu wengine kwa usalama wake na hadhi yake. Hata mimi leo nikifungwa, siwezi kuwekwa na wewe kwa kuwa nina karatasi nyingi zenye sahihi ya gavana tofauti na wewe muuza bata. Farid amechezea Wapemba wenzake, sasa atanyolewa hadi uwani
Majibu yanajitosheleza.. tunasubiri na wale waheshimiwa sana wenye nchi watakapokutwa majanga tuone nini kitafanyika. na hapo ndipo tutakuja na hoja na maamuzi.
 
Back
Top Bottom